Ndugu Mbowe, ambaye anahamasisha maandamano haya, ana watoto lakini hajawahi hata siku moja kuwaweka mbele kwenye harakati hizi.
Kwa nini nyinyi mufanye hivyo? Vijana, kumbukeni kuwa Tanzania yetu ni nchi moja tu, na hatuna nyingine. Maandamano haya hayatatufaidisha, bali yataharibu taswira nzuri ya nchi yetu.
Tuchukue jukumu la kuyapinga kwa nguvu zetu zote, na tuachane na wanasiasa wachache wanaotaka kutuweka bize na maandamano ili wafurahishe mabosi wao huko nje, kama vile Ujerumani, kwa malengo yao binafsi.