Range Rover liheshimiwe

Noma sana!
 
Mtoto wa kiume unataka upewe gari siku ya birthday?! Duuh!
Kwanza mwanaume unatoa wapi muda wa kusherekea birthday achilia mbali hayo mawazo ya kutaka kupewa Range Rover?!
James Delicious wapo wengi. vijana hawapendi kazi halali. Mimi vijana kama Hawa nawahitaji Sana, Nina kazi ya kuwapa. Napatikana 0754515646
 
Range ni nzuri kimuonekano ila ukija kwenye reliability hamna kitu Ndio maana watu wanayapotezea.
Halafu resale value yake inashuka mapema sana compare to LC
Umeongea ukweli nilikuwa nayo moja nimeiuza bei ya chini sana

Nimeendesha zote ila niliipenda Autobiography ya Range ni kali sana nilikuwa nampelekea mchezaji mmoja wa Rugby
Wachezaji huwa wanapewa bure ili kuitangaza

Likija suala la SUV napendelea Volvo zaidi na Audi kama Q5 na Q7 lile kubwa

Nimeyaendesha yote yakiwa mapya nikiwapelekea customer wanao test drive
 
Sikuzote nakataa hii point ya v8 eti gari inachoka haraka umaskini wetu ndio unasababisha gari kuchoka. Unaposema big for nothing umeziona card chav au lincoln za mwaka jana tu zina vitu standard gari za bongo hazina
 
Sababu ya kupenda Volvo na Audi ni ipi?
 
Guys poleni na majukumu

Range ni gari ambayo haina mpinzani ni gari zuri sana na la heshima natamani sana kumiliki kama inatokea mtu ananiambia nichague gari basi nitachagua range 🤗🤗🤗 my dream car
Mafundi na bei za spare zake na upatikanaji ni pasua kichwa

Usione wachache huzimiliki.Omba Mungu lisikuletee fyoko Mafundi wanaoziwezea vizuri wachache na bei za spea ni moto wa kuotea mbali

Na ukitaka kuliuza hata bei ya kutupwa kupata mteja shida kubwa

Gari kabla kununua Tanzania jiulize je kuna mafundi na gereji za kutosha za kumudu kutengeneza hilo gari likileta fyoko popote Tanzania ikiwemo mijini na wilayani? Sababu zote hizo zina gereji maalumu huwezi pelekea fundi yeyote atengeneze hawaziwezi zina specialised garages .

Pili jiulize upatikanaji wa spea zikihitajika na je bei iko ndani ya uwezo wako wa kumudu?

Gari kama Range Rover na Mercedes Benzi ukiona mtu anayo mheshimu

Daladala katika magari hawayafanyii fujo kuwaendeshea hovyo barabarani kwa woga ni Rangerover na Benzi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…