Kichuguu
Platinum Member
- Oct 11, 2006
- 17,048
- 22,790
Na wewe unasumbuliwa ugonjwa wa kuamini na jina kwa historia yake bila kuwa na uhakika wa unalosema. Umeijua Land Cruiser kwa siku nyingi sana tangu Marehemu Lowasa alipopitisha mpango wa kuwa yawe magari ya viongozi wa serikali na wabunge zaidi ya miaka 30 iliyopita umebaki kuamini kuwa Land Cruiser ndiyo kila kitu.Mkuu acha kabisa kuivunjia Heshima Toyota Land Cruiser linapokuja swala la reliability
Ungeweza kabisa kuisifia hiyo jeep bila kujaribu kuiponda Toyota LC
Toyota LC wanauzia jina?
Hivyo vyeti vyako vya veta visikudanganye mkuu
Basi kuanzia leo elewa kuwa kuwa Jeep Grande Cherokee Limited L ya mwaka 2024 ni zaidi ya Land Cruiser. Elewa pia Jeep inapatikana katika model nyingi sana kama vile Cherokee, Grand Cherokee Laredo, Compass, Renegade, Liberty, Wrangler,. Gladiator, Meridian, Commander na kadhalika. Linaloongelewa hapa ni Jeep Grand Cherokee Limited L sIyo Jeep ya aina yoyote.
Kama unadhani leseni yangu ni ya veta, bado kuna independent evaluation niliyoweka hapo huko nyuma sijui pia utaikataa kuwa ni ya veta. Nitaikopi tena hapa kwa faida yako na ya wasomaji wako. jeep hiyo inapata score ya 8.9 wakati Land Cruiser ina score ya 8.7 tu. Kuna sababu kadhaa za kiufundi zinazoifanya jeep iipiku Land Cruiser; mimi nimezungumzia uwepo wa parts za plastic nyingi kwenye land Cruiser ukilinganisha na Jeep. Kama una ujuzi mwingi zaidi ya cheti cha VETA, sema tuongee technical comparison kati ya hayo magari mawili kwa vile mimi nilishayafungua yote na nayajua vizuri sana