Mayu
JF-Expert Member
- May 11, 2010
- 7,621
- 12,505
Mkuu labda hatujaelewana argument yangu ni niniNinaelewa arguments zako za uzoefu, ila kuna mambo ambayo pia hujaweka kuweza kusema kwa nini Toyota Land Cruiser zinatumika sana kama official cars katika nchi za kiafrika (siyo nchi nyingi duniani bali ni Afrika tu); siyo reliabiliy kwani hakuna metric iliyotumiwa kwa mfano na serikali ya Tanzania kuachana na Landrover pamoja na Nissan Patrol ambazo zilikuwa na technicial features zinazolingana na pia bei ikiwa ya chini, bali wakachukua Land Cruiser ambayo bei yake ilikuwa ya juu; marehemu Lowassa angekuwapo, angetuambia hilo.
Kuhusu maeneo korofi, basi hujui kuwa Jeep ilitengezwa kwa mara ya kwanza kabisa kwa ajili ya matumizi ya kivita wakati wa vita ya kwanza ya dunia. Lilikuwa gari la kijeshi kabla ya kufanywa la kiraia. Hakuna eneo korofi ambako jeep ya aina yoyote ile itashindwa leo. Kama unaijua gari inayoitwa Hummer, basi elewa kuwa hiyo ni offspring ya Jeep baada ya jeep zile za kijeshi kubadilishwa design na kuitwa Humvee na Hummer ikatokea huko.
UN Kutumia magari ya Land Cruiser hutokana na serviceability ya magari hayo kwenye meneo husika. UN hutumia gari yoyote inayoweza kuwa serviced kwa urahsi huko inakotumika.
Argument yako ya Reliability na durability ya Land Cruiser inawezekana kuwa ni sahihi historically ila kwa sasa hivi tuaongelea mwaka 2024 na tunaipambanisha na Jeep Grand Cherokee Limited L la mwaka huu 2024.
Mimi sijaishindanisha TLC Vs Jeep....... HAPANA
Mimi nime argue uliposema TLC sio magari mazuri ila yanauzia jina tu(Hapa unakua unamvunjia heshima mjapani)
Mkuu naiheshimu sana JEEP, hiyo ndio nembo ya ubora wa off road za magari ya USA
Kimsingi Land Cruiser ni matokeo ya Jeep
Wakati wa vita ya pili ya Dunia Wajapani walipoanza kupiga na kuteka kambi za USA na washirika wake walikamata na gari za Jeep(Willys MB) za kivita enzi hizo.
Emperor wa japan alipoziona akatoa order gari zipelekwe Toyota watengeneze gari kama hiyo kwa sababu ya uwezo wake mkubwa kuhimili kazi na njia mbovu
Na baada ya vita kwisha Toyota wakaendelea kuzalisha kibiashara hadi tunavyo ziona leo kwa ufanisi mkubwa
So ukiniuliza leo hii kati ya TLC na Jeep Grand Cherokee ipi ni zaidi basi nitachagua Jeep....... lakini hiyo haifanyi kwamba Toyota Land Cruiser ni gari mbovu zinazo uzia jina
Hata ikiwa Messi atakua bora kuliko Ronaldo hakufanyi kuwa Ronaldo ni mchezaji mbaya
Issue ni kwamba umeshindanisha vitu BORA kabisa viwili
BTW ulikua mjadala mzuri sana 🙏