Zack Abdul
JF-Expert Member
- Mar 9, 2026
- 1,194
- 911
Msanii maarufu wa Marekani, William Leonard Roberts II, anayefahamika kwa jina la Rick Ross, ameendelea kuonyesha kuvutiwa na Tanzania akitamani kufanya ziara hivi karibuni.
Katika mazungumzo yake, Rick Ross ameisifu Tanzania na kueleza nia yake ya kuitangaza Tanzania pamoja na fursa zake kwa soko la kimataifa. Aidha, ameonyesha heshima kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, akimtaja kama sehemu muhimu katika kuiweka Tanzania katika jukwaa la kimataifa.
Kwa upande mwingine, Rick Ross ameeleza kuwa amefanya mazungumzo na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Paul Makonda, ambaye amesema alimweleza kuhusu Tanzania na mipango mbalimbali inayohusisha fursa na maendeleo ya Tanzania.
Kauli ya Ross juu ya Tamzania imeongeza mvuto wa Tanzania kimataifa, hususan kupitia ushawishi wa watu maarufu katika sekta ya burudani na utamaduni, huku ikifungua nafasi ya Tanzania kujitangaza kama eneo la utalii, uwekezaji, biashara na utamaduni wenye kuvutia watu wa mataifa mbalimbali.