Issue yake ya kukamatwa iko hivi, miaka minne ilyopita rapper king von ambaye ni swahiba wa durk aliuawa kwa risasi huko Atlanta akiwa anamletea usela mavi rapper mwenzake wa chicago wa kuitwa quando rondo wakamshoot
mwaka 2022 lil durk alituma member wa kundi lake la OTF (Only the family) kulipiza kisasi cha king von wenyewe wanaita (slide for von) kutoka chicago mpka los angeles kwenda kumuua quando rondo akiwa kwenye kituo cha mafuta lakin ikashindikana wakamuua binamu yake na Rando
Mapolisi wakaanza kufuatilia hii ishu wakaweza kumbananisha moja wa member wa kundi la OTF awe amamsnichi Lil Durk, Mapolisi wakamwambia awe anawasha recoeder anapozungumza na Lil Durk wakiwa kwenye Gari, Nyumbani kwake, Party, n.k. sasa hapa itakuwa Lil Durk kapayuka mara kadhaa ile ishu ya kutaka kumuua Rando na kumuua binamu yake na pengine kutaka kujaribu tena kumuua Rando, Hakuna mtu anaeaminika mtaani, Huyo member wa OTF itakuwa alitishwa atafungwa maisha jela kwa kesi ya mauaji halafu akiangalia pembeni ana famili, cha kufia nini ? akaamua amchome tu Lil Durk.
sasa week kadhaa zilizopita majamaa waliotumwa na durk kumuua quando wamekamatwa, lil durk alikua zake Miami anaskia jamaa zake wamekamatwa aka book ndege mbili kutoka miami kwenda Dubai na nyengine ya kwenda Uswiswi, inasemekana ilikua ni mikakati ya kukimbia nchi ila alikamatwa kabla ya kuanza safar.
Miziki mingi ya Lil Durk inahamasisha mauaji, Uhalifu na matumizi ya madawa ya kulevya na yeye pia anapenda kuishi maisha hayo, mitaa ya Chicago anasifika kwa kuwa rapper aliye ua watu wengi,
Aina ya muziki wanaoimba marapa wa Marekani umeathiri sana wamarekani weusi, Chicago ni jiji lenye wamarekani weusi wengi, jiji hilo linasifika zaidi kwa kuwa na kiasi kikubwa cha uhalifu ikiwemo mauaji baina ya watu weusi, wasanii vioo vya jamii wanahamasisha mauaji, watu weusi wanamiminiana sana risasi.
Achana na movies, hivi ndivyo mambo yalivyo chicago, Hili ni shambulizi la kisasi cha genge