Ras Mtimanyongo: Kimsingi Kariakoo ni eneo la sokoni (Wamachinga) tangia Uhuru, Wafanyabiashara kwao ni Samora na Kitumbini

Ras Mtimanyongo: Kimsingi Kariakoo ni eneo la sokoni (Wamachinga) tangia Uhuru, Wafanyabiashara kwao ni Samora na Kitumbini

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Msanii Ras Mtimanyongo anasema kamwe Wamachinga hawawezi kuondoka Kariakoo kwa sababu ndio sokoni kuanzia nchi hii ijitawale.

Mtimanyongo anasema Wafanyabiashara kwao ni Samora zamani Independence avenue na Kitumbini na ndio maana hadi sasa hata vijiduka vya kariakoo ni vya ujanja ujanja tu.

Mtimanyongo anasisitiza kuwa kifuatacho kiwe TRA kusaka maghala ya hao wajanja wajanja wa Kariakoo huko Vingunguti na Buguruni kama kweli wanataka kukusanya kodi.

Mungu ni mwema wakati wote!
 
Tuweke kumbukumbu sawa.

Kariakoo kama SOKO lilianza baada ya wajerumani kuondoka na sisi kuwa chini ya waingereza.

Mwaka 1960 ndio soko lilianza rasmi na hakukuwa na hao "maching guys", wakijumuisha "wanaozunguka na bidhaa mojamoja mikononi kama CHENI na SAA"
 
Tuweke kumbukumbu sawa.

Kariakoo kama SOKO lilianza baada ya wajerumani kuondoka na sisi kuwa chini ya waingereza.

Mwaka 1960 ndio soko lilianza rasmi......na hakukuwa na hao "maching guys"....wakijumuisha "wanaozunguka na bidhaa mojamoja mikononi kama CHENI na SAA".
Kwahiyo kimsingi unakubaliana na Ras kwamba Kariakoo ni Sokoni
 
Kwahiyo kimsingi unakubaliana na Ras kwamba Kariakoo ni Sokoni
Sikubaliani naye kusema kuwa hao wamachinga ndio asili ya hapo sokoni....

Mwanzo WAFANYABIASHARA walikuwa "WANAPANGA BIDHAA CHINI"....baadaye Serikali chini ya hayati Mwalimu Nyerere ikalitengeneza hilo soko jipya lenye "VIZIMBA".....

Lengo la VIZIMBA ni kuziboresha biashara zenyewe...USALAMA WA KIAFYA NA USAFI WA MJI....

Na ndiyo yanayofanyika kwa hizi siku 12 kwa Serikali kuwataka WAFANYABIASHARA HAO kuhamia maeneo RASMI KIBIASHARA.......
 
Msanii Ras Mtimanyongo anasema kamwe Wamachinga hawawezi kuondoka Kariakoo kwa sababu ndio sokoni kuanzia nchi hii ijitawale.

Mtimanyongo anasema Wafanyabiashara kwao ni Samora zamani Independence avenue na Kitumbini na ndio maana hadi sasa hata vijiduka vya kariakoo ni vya ujanja ujanja tu.

Mtimanyongo anasisitiza kuwa kifuatacho kiwe TRA kusaka maghala ya hao wajanja wajanja wa kariakoo huko Vingunguti na Buguruni kama kweli wanataka kukusanya kodi.

Mungu ni mwema wakati wote!
Wakati wa mwendazake mlikuwa mnawadanganya wafanye biashara popote leo mnawapiga virungu.
 
Sikubaliani naye kusema kuwa hao wamachinga ndio asili ya hapo sokoni....

Mwanzo WAFANYABIASHARA walikuwa "WANAPANGA BIDHAA CHINI"....baadaye Serikali chini ya hayati Mwalimu Nyerere ikalitengeneza hilo soko jipya lenye "VIZIMBA".....

Lengo la VIZIMBA ni kuziboresha biashara zenyewe...USALAMA WA KIAFYA NA USAFI WA MJI....

Na ndiyo yanayofanyika kwa hizi siku 12 kwa Serikali kuwataka WAFANYABIASHARA HAO kuhamia maeneo RASMI KIBIASHARA.......
Wapangwe hapo hapo Sokoni Kariakoo wakati wanasubiri Machinga complex ya mchina pale Ubungo!
 
Wakati wa mwendazake mlikuwa mnawadanganya wafanye biashara popote leo mnawapiga virungu.
Hawakudanganywa mkuu....

Ardhi ni mali ya dola....na biashara hufanyiwa juu ya ardhi.....dola imeamua waondoke kwa faida pana ya kila mmoja wetu......

#Zama Mpya
 
Swali langu nauliza wale jamaa wanawapeleka wapi?

Kwa Dar es salaam ni maeneo gani ya wazi wametengewa kufanya shughuli zao?
 
Wapangwe hapo hapo Sokoni Kariakoo wakati wanasubiri Machinga complex ya mchina pale Ubungo!
Vizimba vinatosha hapo sokoni Kariakoo?!!

Ama waendelee kuweka bidhaa barabarani Jambo ambalo mwaka 1971 lilikoma kwa kutengenezwa hivyo VIZIMBA?!!!!
 
Vizimba vinatosha hapo sokoni Kariakoo?!!

Ama waendelee kuweka bidhaa barabarani Jambo ambalo mwaka 1971 lilikoma kwa kutengenezwa hivyo VIZIMBA?!!!!
Vizimba vitatosha tu square meter moja moja.

Hakafu mzee Mgaya kaniambia CCM inapiga chini lile jengi la DDC na kushusha Machinga complex matata sana!
 
Tuweke kumbukumbu sawa......

Kariakoo kama SOKO lilianza baada ya wajerumani kuondoka na sisi kuwa chini ya waingereza.....

Mwaka 1960 ndio soko lilianza rasmi......na hakukuwa na hao "maching guys"....wakijumuisha "wanaozunguka na bidhaa mojamoja mikononi kama CHENI na SAA"........
Machinga kazi yao ilikuwa ni kuzunguka hasa vile bidhaa vya wizi kwenye maduka ya wahindi ndio vilikuwa vinapatikana kwaurahis kwa bei nafuu. Sasa hawa wameweka makazi hadi wamelala.
 
Back
Top Bottom