Ras Mtimanyongo: Kimsingi Kariakoo ni eneo la sokoni (Wamachinga) tangia Uhuru, Wafanyabiashara kwao ni Samora na Kitumbini

Ras Mtimanyongo: Kimsingi Kariakoo ni eneo la sokoni (Wamachinga) tangia Uhuru, Wafanyabiashara kwao ni Samora na Kitumbini

Serikali na wananchi ni lazima tushirikiane katika kuyatafuta majawabu......

Ni siku za karibuni CHIFU MKUU HANGAYA alipoongelea TOZO ZA MIAMALA YA SIMU kuwa zinakwenda KUJENGA NA KUBORESHA BARABARA ZIELEKEAO mashambani ili kuzidi kukiinua KILIMO alipingwa na baadhi yetu wananchi.......
Kwahiyo serikali imeshirikiana na machinga kuwaondoa.
 
Wasukumwe...
Wagombezwe...
Waangushwe...
Wapigwe.....
Wagongwe na maguta/magari
Wakabwe/waibiwe
Watoto,wazee na wagonjwa wao wapate shida...

Kweli hiyo ndio STAHIKI ya wakazi wa K/KOO....

Haya mkuu 🤣
Bwashee kukaa karibu na soko kuu kuna faida na hasara zake!
 
Kwahiyo kimsingi unakubaliana na Ras kwamba Kariakoo ni Sokoni
Kariakoo kama soko au eneo? Maana mfano tu, mahali zilipo zile fremu za jengo la Simba ni Kariakoo pia kama ukizungumzia eneo, lakini ni barabarani wala sio sokoni
 
Waende masokoni wakalipie vizimba kama wafanyavyo wafanyabiashara wengine, walipe na kodi pia! Watengewe maeneo kwa umaalumu gani walionao? Ni kundi gani hapa TZ limepangiwa eneo maalumu la kufanyia mambo yao? Wao ni vilema hadi wadekezwe hivi?
Vizimba vingekuwa vinapatikana kirahisi hivi kama ulivyotype kusingekuwa na mtu barabarani🤓!!!

Pia upepo wa biashara wa kariakoo huwezi fananisha na wa mtaani! Mtaani kuipata elfu 50 kwa siku kama uipatavyo kariakoo lazima uwe na mganga mkali sana😂😂😂
 
Kariakoo kama soko au eneo? Maana mfano tu, mahali zilipo zile fremu za jengo la Simba ni Kariakoo pia kama ukizungumzia eneo, lakini ni barabarani wala sio sokoni
Bwashee soko siyo jengo ni ule mkusanyiko wa wauzaji na wanunuaji!
 
Masaki hakuna hasara bwashee!
Uswazi mathalani Mbagala Rangi 3 unaweza kuzurura.... kunywa kahawa usiku mnene na hata kupata FEGI ,MKUBWA na RIZLA ZAKE na "za kupima" muda wowote ule saa 9 usiku ama laa ..vipi Kichanga Chui Masaki ?!!🤣🤣
 
Vizimba vingekuwa vinapatikana kirahisi hivi kama ulivyotype kusingekuwa na mtu barabarani🤓!!!

Pia upepo wa biashara wa kariakoo huwezi fananisha na wa mtaani! Mtaani kuipata elfu 50 kwa siku kama uipatavyo kariakoo lazima uwe na mganga mkali sana😂😂😂
🤣
 
Vizimba vitatosha tu square meter moja moja.

Hakafu mzee Mgaya kaniambia CCM inapiga chini lile jengi la DDC na kushusha Machinga complex matata sana!
Wapige chini lile jengo la Lumumba ndio mali ya ccm.

Jengo la DDC ni mali ya Jiji.
 
Hahahaaaa...... ....Kwanza muulize Amos " machinga" ni nani?

Usilete mambo yako ya kinyantuzu!
Baada ya uhuru nchi hii iliendeshwa kistaarabu sana.
Kitu machinga, chapati barabarani na kupanga nyanya havikuwepo kabisa.
Wanasiasa washamba washamba toka vijijini ndio wamelea huu uozo.
 
Vizimba vingekuwa vinapatikana kirahisi hivi kama ulivyotype kusingekuwa na mtu barabarani🤓!!!

Pia upepo wa biashara wa kariakoo huwezi fananisha na wa mtaani! Mtaani kuipata elfu 50 kwa siku kama uipatavyo kariakoo lazima uwe na mganga mkali sana😂😂😂
Hakuna namna mkuu, and haiwezekani watu wote tukafanye biashara Kariakoo, hata ingekuwa kubwa vipi haiwezi kucontain kila mfanyabiashara anayetaka kwenda pale, aliyewahi ameshawahi, watafute maeneo mengine ya kutafuta mkate wao wa kila siku!!
 
Msanii Ras Mtimanyongo anasema kamwe Wamachinga hawawezi kuondoka Kariakoo kwa sababu ndio sokoni kuanzia nchi hii ijitawale.

Mtimanyongo anasema Wafanyabiashara kwao ni Samora zamani Independence avenue na Kitumbini na ndio maana hadi sasa hata vijiduka vya kariakoo ni vya ujanja ujanja tu.

Mtimanyongo anasisitiza kuwa kifuatacho kiwe TRA kusaka maghala ya hao wajanja wajanja wa kariakoo huko Vingunguti na Buguruni kama kweli wanataka kukusanya kodi.

Mungu ni mwema wakati wote!
Hata kama tangu zamani wapo, basi ndiyo kusiwe na mpangilio na utaratibu? Tufike sehemu tukubali kwamba mipango na taratibu nzuri zitumike katika hili la machinga
 
Baada ya uhuru nchi hii iliendeshwa kistaarabu sana.
Kitu machinga, chapati barabarani na kupanga nyanya havikuwepo kabisa.
Wanasiasa washamba washamba toka vijijini ndio wamelea huu uozo.
Mzee Majambo wa mwananyamala na mzee Samaki wa Msasani walikuwa wanafanya nini kama siyo Umachinga?
 
Hata kama tangu zamani wapo, basi ndiyo kusiwe na mpangilio na utaratibu? Tufike sehemu tukubali kwamba mipango na taratibu nzuri zitumike katika hili la machinga
Ndio maana wanapangwa " vizuri " bwashee.

Chadema wameliharibu sana jiji la Dar es salaam!
 
Back
Top Bottom