Rashid Makwiro (Chid Benz) hali yake ni tete kutokana na matumizi makubwa ya madawa ya kulevya

Rashid Makwiro (Chid Benz) hali yake ni tete kutokana na matumizi makubwa ya madawa ya kulevya

Kama sio mwanzoni mwa mwaka huu basi mwaka jana, alikuwa anaenda ktk shoo mbeya kama kumbukumbu yangu ipo sahihi, akadakwa na dawa pale dar airport. Nadhani kuna wadau walifanya wawezavyo kumuondosha ktk kadhia ile
upo sawa mkuu
 
Kuna kitu huwa kinanisaidia sana kwenye maisha yangu , tabia zangu zile nilizokuwa nazo toka utotoni mbaya niliziacha na hakuna tabia mbaya nilizoiga ukubwani.

Ulimbukeni wa mtu kujaribu kitu ili aone matokeo yake yatakuwaje ni ujinga.

Pia polisi na hao wanaosema wapo kwa ajili ya wanyonge kwanini wasimtumie chid benz awaambie hayo madawa alikuwa anayanunua wapi (sijasikia hata serikali ikiuliza lolote).

Mambo ya hatari namna hii tunayaongea bila kuchukua hatua ili tusaidie wengine ambao bado hawajazama kwenye dimbwi la Madawa ya kulevya !!!
 
Ni rahisi sana kumlaumu Chidi kwa hali aliyofikia ila tujue kabisa kuna wakati na yeye anajiskia na kujuta kutumia.Addiction na dependence sio mchezo.unaangamia unajiona.Muda aliotumia kule sober house ni mdogo sana ukilinganisha na kipindi alichotumia madawa i mean tangu alivyoanza mana dependence haijengwi kwa mda mfupi.Kila mtu hulichukulia hili swala si lake na ndo mana hata waliompeleka hawakuweka mkakati wa kumsaidia baada ya kutoka.Kuna wakati mazingira,upweke na mawazo ukiongezea na watu wanaokuzunguuka tu hutosha kumrudisha mtu kwenye madawa.Dependence ni ugonjwa wa akili kama kuna anaejitolea kumsaidia asiishie kumpeleka sober house ila pia kusimamie mazingira atakayoishi baada ya kutoka kule mpaka itakaporidhisha kitaalam kwamba amepona.
 
wale wanaokula methadone pale mwananyamala mbona changes naziona? wako smart siku hizi na kazi wanafanya

kama ray c kashindwa nadhani chid kama mwanaume ataweza kula dozi kwa usahihi na kurudi kwenye hali yake

aamue tu
 
Hapo zamani za kale palitokea jamaa mmoja machachari sana aliyejiita Chidi Benzi, ila kutokana na Ungangari wake katika game watu wakamuita Chuma
..........basi Ikaendaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa....................

Na hadithi yetu ikaishia hapo...
 
Dah! masikini, jamaa ana kipaji cha hali ya juu. Imekuwaje kawa hivi?, hata kama ngada, ngada hawezi kupitiliza kuwa kama chizi kama hivi.
 
Ewe Mwenyezi Mungu tenda muujiza kwa kijana huyu apate kukujua na kukutumikia ili siku ya mwisho afike kwako juu Mbinguni
 
Back
Top Bottom