Rashid Makwiro (Chid Benz) hali yake ni tete kutokana na matumizi makubwa ya madawa ya kulevya

Rashid Makwiro (Chid Benz) hali yake ni tete kutokana na matumizi makubwa ya madawa ya kulevya

Mbaya zaidi hawa Jamaa wao wakishapata wanaona wanaendelea na Yale maisha yao ya awali na hapo Jamaa anahisi yupo kwenye sehemu anaonyesha show,ni hatareeee hapo ni kuokoka aanze upya
 
Kunaraisi alikuwa na uswahili mwingi. Ndie alieingiza madawa ya kulevya Tanzania. Tena yalianzai kuingia kwenye kisiwa chenye uswahili mwingi
 
Hivi nyie mnao jidai kumuhurumia Chidy Benz je ni kweli mnamsaidia au mnazidi kumuongezea Stress,maana mnazidi ku tag na ku post picha zake eti mnamuonea huruma kwa kuzidi kumchoresha kwenye Mitandao ya ki jamii ,HIVI KUMTUMA,KUMJADIRI NA KU POST PICHA ZAKE ndio kumsaidia ,utakuta mtu ana tuma picha yake na kuandika chini "dah jembe langu",Hivi amjui kuwa anazidi kukataa tamaaa
Nb:KAMA MUNA HURUMA MBONA MATEJA WAPO WENGI MTAANI WANAANGAMIA NA MUNA WAONA
 
Ni bora kuweka picha za huyu mmoja,ili milioni moja wanaotaka kuingia kwenye huo mkumbo wakishaona hali ilivyokuwa mbaya wataingiwa na hofu na kukaa nayo mbali,kuliko kubaki unasikia watu wanaangamia bila ya kujua uhalisia.
 
Tumsaidieje mtu asiyetaka msaada?si alitoroka Sober House huyo au?
 
Yeye mwenyewe amejipost kwenye wall yake sasa shida iko wap kwa wanaomsaidia kupost
 
Yeye mwenyewe alisema Mama yake mzazi alishindwa, sembuse nyie.
 
KING KONG ( The Rise & Fall)...Part I.
Kumekuwa na Habari nyingi kuhusu CHIDY BENZ lakini je Ukweli ni Upi?...nini Chanzo cha haya yote na Solution yake?..
Personally kuonana macho kwa macho na kuzungumza na Chidy Benz mwenyewe Mwanzoni mwa Mwaka huu 2016 kulinifanya nijue mengi na nishushe Kalamu chini na kuufyata...nikashindwa kuandika tena...lakini hali ilipofikia leo nitaandika Machache tu...sio yote...baadhi tu...
ktk Mahojiano hayo mpaka yanaisha Chidy alinitambua kwa jina moja tu...the fake ID "Eden Hazard".
KING KONG anaanza kunieleza
"Miaka kadhaa iliyopita Baada ya kuwika kwenye Free Styles Battles nilianza kutoa nyimbo zangu...Hakika Mimi nilikuwa msanii niliye juu zaidi pengine kuliko Msanii yeyote kwa wakati wangu..Mimi nimepiga Show India kabla hata ya P-Square tena nikizunguka na Private Jet Mumbai-Delhi -Delhi-Mumbai.
Katika wakati wa Ubora wangu nilikuwa ni Msanii pekee ambaye alikuwa anatembea na Msafara wake wa magari kwenye Show za Fiesta wakati wasanii wengi wakikusanywa na Mabasi (Coaster)....na ukumbuke nilikuwa ni mmoja wa Wasanii wachache ambao hawana Meneja..I was Managing Myself.
Mimi ni Msanii Pekee wa Hip Hop niliyekuwa Hot kiasi kwamba nikashirikishwa mpaka kwenye nyimbo za Bolingo..kumbuka FM Academia....Japokuwa mimi ni Rapper lakini bado ninaamini ninaweza pia kuimba kuliko hata wasanii wengi Waimbaji na kwa kuthibitisha hilo niliachia nyimbo ya "Mashallah" ft Mzee Yusuph...Mtu wa kwanza kuninyooshea mikono kwa pongezi alikuwa Kaka yangu Nyoshi el Saadat....During that time I was Hot.
Hayo yote ninayozungumza si kwa Lengo la kujisifu la hasha!...naumia kuona nipo hivi leo..naumia kwa Ulevi niliouingia...ulevi ambao mara kadhaa nimejaribu kuuacha...leo King Kong Mwili Jumba nimebaki na Mwili huu?niseme tu wazi sisi kama wasanii hujaribu vilevi vingi hasa pale tunapokuwa Hot na fedha inaingia...kumbuka wasanii muda wote ni watu wa safari na show,...wengi tunashindwa kuji-manage na Starehe...Maisha yanayotuzunguka hutulevya..Maisha ya vilevi na wapambe.
Mimi nimewahi kulipiwa Milioni 25 na Diamond ili kutolewa Damu na kusafishwa...nilipopona nikarudi tena kwenye kutumia tena na tena.
Mimi niliwahi kuchukuliwa na Association ya wanamuziki wa Kenya wakiongozwa na Nonini nikatolewa Damu na kusafishwa kwa mara nyingine...lakini nikarudia tena.
Nakumbuka mwanzoni mwa mwaka 2015 siku moja wakati nipo Maisha Club Basement alikuja Mtu Mmoja akaniambia "Chidy hii si sawa...Chidy umekwisha..Afya yako inatisha...tafadhali chukua hii namba kesho nipigie nione namna ya kukusaidia"
Basi kesho yake nikampigia simu yule jamaa,.alichofanya ni kunichukua na kunipeleka Sober House (Pemba)...akalipa Gharama zote.
Sasa wakati nipo Pemba kuna pesa zangu za kazi ya Muziki ziliingia..Millions of Money...kwa kweli ilitaka sana Moyo kwa mtu mwenye Addiction kama mimi kuvumilia kukaa Sober House while huko nje kuna Milioni kadhaa...Nikaondoka Rehab kwa lazima...hii ilikuwa sawa na mgonjwa anatoroka Dozi hospitali....nikarudi Jijini....jijini Dar es Salaam.
[HASHTAG]#Itaendelea[/HASHTAG] .....
 
KING KONG (The Rise & Fall) Part ll (Finale)
Anaendelea:...
"Nilirudi tena Jijini Dar es salam..hapo nina Mamilioni yangu...nikaanza bata...nikarejea kwenye ulevi wa vilevi vyote kikiwemo kile kikuu kinachoniangamiza....nilikaa hotel..nikatumi
a....kiasi cha fedha nilipeleka kwenye Ujenzi ambao haukufika mbali...leo nazungumza na wewe hapa zimekwisha zote...nikimbushe tu kwamba Maisha haya sio sifa bali ni utumwa....utumwa ambao sishauri mtu mwingine ajaribu kijiingiza...Brother hata wewe usije ukajaribu kamwe...huu ni utumwa mkuu kuliko Minyororo ya Mjerumani.
SWALI : Je kuna wasanii wengine wengi wanatumia dawa?
JIBU : Sio wasanii pekee...wapo watu wengi ktk nafasi mbali mbali ziwe za sanaa au jamii wanatumia, wengine nasikia wanatumia hiyo inayoitwa white sugar...kifupi hili ni Janga kubwa.
SWALI : Una dhamira ya kuacha??.
JIBU : Dhamira ninayo..natamani kuacha kabisa, natamani kurudi kwenye Game.
SWALI : Unaonaje ukiacha leo hii..Ukarudi na kwenye ibada?
Hapa alikaa kimya kwa muda, ikabidi nibadili mada kidogo...nikatoa simu yangu na kuweka Nyimbo ya "Dar es salaam Stand Up"
SWALI : Chidy hii nyimbo unaielezea Vipi?
hapa sasa kwa mara ya kwanza kabisa niliyashuhudia machozi ya King Kong..ni dhahiri analia.
CHIDY.. "Hii ni nyimbo ambayo mama yangu Mzazi anaipenda kuliko nyimbo zangu zote...hii ni nyimbo ambayo nikisimama ktk Show hakuna nyimbo itasimama juu yake, ninapoisikia huwa ninakuwa na hisia kali sana"
SWALI: Unaonaje ukiachana na dawa urudi kwenye game?
CHIDY: Ok nimekubali..ila Siwezi kuacha leo kwa mara moja..nitaacha taratibu...leo ni Alhamisi, napunguza dozi kufikia Jumanne nitakuwa niameacha kabisa"
Baada ya hapo ikawa ni stori zingine baadae kila mtu akashika njia yake.
Baada ya wiki moja CHIDY akaanza kuhangaika mwenyewe ili arudi kwenye Game...dawa akasema kaacha, ...First interview akaibukia EAST AFRICA REDIO akatangaza kurudi kwenye Game.
Second Interview akaibukia CLOUDS TV....hapa Clouds sasa ndio zile picha zake za appearance ya kutisha zikaonekana...finally akachukuliwa na Babu tale na kupelekwa Soba House kwa mara nyingine na kuahidiwa kusaidiwa kimuziki.
Picha likaishia hapo.....The Fake ID "Eden Hazard" am off .....mengine yaliyoendelea baada ya hapo Babu Tale anajua zaidi nini kimetokea.
Leo inasikitisha sana kumuona Chidy katika hali aliyonayo...sina lawama juu yake maana huyu ni Muhanga mmoja hadharani lakini kuna maelfu wako Gizani....Tumepata Fursa ya kumuona Chidy kwa sababu ni maarufu na Mtu mwenye impact ktk sanaa yake na Jamii...je vipi kuhusu wale wasijulikana?..
..kupitia Chdiy tuna Mengi ya kujifunza....ye
ye amekiri kwamba kilevi alichokijaribu kimemfunga...anatamani asingewahi kujaribu...amekuwa mtumwa.
Mwisho niseme tu kwamba Kizazi hiki na kijacho vinateketea....hii ni VITA DHIDI ya Madawa ni Vita ambayo inatakiwa kuchukuliwa kama WORLD WAR III...je nani anathubutu?....nani atapiga kelele kama Selikari za Mataifa ya Dunia hii zimekuwa Bubu?...ni Rais Rodrigo Duterte pekee wa Ufilipino pekee amejaribu practically....
wengine ni theoretically...hivi kweli tunaweza kuzuia Drug Dealers kwa hotuba na Maandiko???.
Nami nakuwa Bubu milele, Hii Vita Mentally naiona kama World War III, sie wenye Magobole kamwe hatuiwezi vita hii...Vita ya wenye Fedha na Dola....vita ya mabomu kama Motolov Cocktail na Vifaru....am off Guys...see U next year if God wishes.
CHIDY have a Quick Recorvery Brother
 
Kama kuna siku dunia itafikia tamati basi ukweli wa mambo mengi utadhihirika! Kuna mengi sana yamejificha juu ya kuharibika kwa maisha ya watu!
Mungu pekee ndie mjuzi wa yote!
 
Back
Top Bottom