KING KONG (The Rise & Fall) Part ll (Finale)
Anaendelea:...
"Nilirudi tena Jijini Dar es salam..hapo nina Mamilioni yangu...nikaanza bata...nikarejea kwenye ulevi wa vilevi vyote kikiwemo kile kikuu kinachoniangamiza....nilikaa hotel..nikatumi
a....kiasi cha fedha nilipeleka kwenye Ujenzi ambao haukufika mbali...leo nazungumza na wewe hapa zimekwisha zote...nikimbushe tu kwamba Maisha haya sio sifa bali ni utumwa....utumwa ambao sishauri mtu mwingine ajaribu kijiingiza...Brother hata wewe usije ukajaribu kamwe...huu ni utumwa mkuu kuliko Minyororo ya Mjerumani.
SWALI : Je kuna wasanii wengine wengi wanatumia dawa?
JIBU : Sio wasanii pekee...wapo watu wengi ktk nafasi mbali mbali ziwe za sanaa au jamii wanatumia, wengine nasikia wanatumia hiyo inayoitwa white sugar...kifupi hili ni Janga kubwa.
SWALI : Una dhamira ya kuacha??.
JIBU : Dhamira ninayo..natamani kuacha kabisa, natamani kurudi kwenye Game.
SWALI : Unaonaje ukiacha leo hii..Ukarudi na kwenye ibada?
Hapa alikaa kimya kwa muda, ikabidi nibadili mada kidogo...nikatoa simu yangu na kuweka Nyimbo ya "Dar es salaam Stand Up"
SWALI : Chidy hii nyimbo unaielezea Vipi?
hapa sasa kwa mara ya kwanza kabisa niliyashuhudia machozi ya King Kong..ni dhahiri analia.
CHIDY.. "Hii ni nyimbo ambayo mama yangu Mzazi anaipenda kuliko nyimbo zangu zote...hii ni nyimbo ambayo nikisimama ktk Show hakuna nyimbo itasimama juu yake, ninapoisikia huwa ninakuwa na hisia kali sana"
SWALI: Unaonaje ukiachana na dawa urudi kwenye game?
CHIDY: Ok nimekubali..ila Siwezi kuacha leo kwa mara moja..nitaacha taratibu...leo ni Alhamisi, napunguza dozi kufikia Jumanne nitakuwa niameacha kabisa"
Baada ya hapo ikawa ni stori zingine baadae kila mtu akashika njia yake.
Baada ya wiki moja CHIDY akaanza kuhangaika mwenyewe ili arudi kwenye Game...dawa akasema kaacha, ...First interview akaibukia EAST AFRICA REDIO akatangaza kurudi kwenye Game.
Second Interview akaibukia CLOUDS TV....hapa Clouds sasa ndio zile picha zake za appearance ya kutisha zikaonekana...finally akachukuliwa na Babu tale na kupelekwa Soba House kwa mara nyingine na kuahidiwa kusaidiwa kimuziki.
Picha likaishia hapo.....The Fake ID "Eden Hazard" am off .....mengine yaliyoendelea baada ya hapo Babu Tale anajua zaidi nini kimetokea.
Leo inasikitisha sana kumuona Chidy katika hali aliyonayo...sina lawama juu yake maana huyu ni Muhanga mmoja hadharani lakini kuna maelfu wako Gizani....Tumepata Fursa ya kumuona Chidy kwa sababu ni maarufu na Mtu mwenye impact ktk sanaa yake na Jamii...je vipi kuhusu wale wasijulikana?..
..kupitia Chdiy tuna Mengi ya kujifunza....ye
ye amekiri kwamba kilevi alichokijaribu kimemfunga...anatamani asingewahi kujaribu...amekuwa mtumwa.
Mwisho niseme tu kwamba Kizazi hiki na kijacho vinateketea....hii ni VITA DHIDI ya Madawa ni Vita ambayo inatakiwa kuchukuliwa kama WORLD WAR III...je nani anathubutu?....nani atapiga kelele kama Selikari za Mataifa ya Dunia hii zimekuwa Bubu?...ni Rais Rodrigo Duterte pekee wa Ufilipino pekee amejaribu practically....
wengine ni theoretically...hivi kweli tunaweza kuzuia Drug Dealers kwa hotuba na Maandiko???.
Nami nakuwa Bubu milele, Hii Vita Mentally naiona kama World War III, sie wenye Magobole kamwe hatuiwezi vita hii...Vita ya wenye Fedha na Dola....vita ya mabomu kama Motolov Cocktail na Vifaru....am off Guys...see U next year if God wishes.
CHIDY have a Quick Recorvery Brother