Rashid Othman: Umeshindwa Jiuzulu!

Status
Not open for further replies.

Mkuu FMES,
Hii hoja yako ya kuwa JK hakuyajua haya sikubaliani nayo kabisa, unless kama utakuwa na proof.

Kama ilivyokuwa kwa mbadhirifu mashuhuri Lowassa ambaye anafahamika kabisa kuwa sio safi lakini bado JK alimpa madaraka, tena makubwa, nafikiri JK pia aliyafahamu ya Chenge lakini hakujali na aliamua tu kumpa ulaji zaidi. Ni vema JK tukamjumlisha na hawa wateule wake na sio kumwacha yeye pembeni kama vile ni mtakatifu. He is not.
 
Hii hoja yako ya kuwa JK hakuyajua haya sikubaliani nayo kabisa, unless kama utakuwa na proof.

Mkuu Kubwajinga,

1. Lowassa, alirudishwa kwenye power na Mkapa, Mwalimu akiwepo, sasa anakuwaje good kwa uwaziri wa Mkapa, lakini sio u-pm wa muungwana? It was toka aliporudishwa na Mkapa, lakini uzuri ni kwamba sasa hayupo tena na ndio hivi tunalilia watinge kwenye mikono ya sheria.

2. Ninaamini 100%, kuwa muungwana hakuyajua ya Chenge na hela za nje zilizosemwa kwa mara ya kwanza last week na gazeti la Guardian la UK, na kumfanya Chenge ajiuzulu this week, sasa kama rais alikuwa anyajua hayo Chenge asingejiuzulu, kama vile Mkapa, alivyomtetea Ngasongwa.

Halafu, Besides the ishu hapa ni mkurugenzi wa usalama, sio Chenge, maana kuna ishu ya Chenge kuleee, kama ni proof basi labda wewe unayo inayosema kuwa rais alijua, au?

3. Mimi binafsi bado ninampa rais, the benefit of the doubt kwa sababu so far haijatokea ishu inayomgusa moja kwa moja, lakini itakapotokea kama kawaida yangu itakuwa ni kumkoma nyani!
 
Naomba mwenye listi ya waliowahi kuwa Wakurugenzi wa Usalama wa Taifa tangu tupate uhuru wamwage data..

Nafahamu wafuatao..Mzee Sawaya, Emilius Mzena, Agostino Mahiga, Imran Kombe, Cornelius Apson, Rachid Othman.

Je kuna wengne ambao labda nimewasahau?
 
kama mwambata wetu wa jeshi Col GK aliwahi kuzungumzia hii issue ya radar haingii akilini kuwa iliwapita watu wa TISS....
 
Icadon, sheria ya TISS inasema wapi kuhusu kuwa na wafanyakazi wa TISS kwenye balozi zetu?
 
Icadon, sheria ya TISS inasema wapi kuhusu kuwa na wafanyakazi wa TISS kwenye balozi zetu?

Mkjj, hiyo sheria sijawahi kuiona/soma ....na ndio maana kwenye posts za nyuma niliuliza nini hasa kazi zao hawa watu kwenye balozi zetu na kwenye taasisi nyingine.
 
Mniwie radhi hii habari yangu imaktaa kwenda kwenye ile thread ya Buzwagi nahisi imezuiliwa ... pata habari/ujumbe wangu

Tuwaunge mkono wananchi wa Buzwagi, kwani huo ni mojawapo ya migodi yenye mikataba ya mizengwe. Cha msingi ni kuwapa taarifa muhimu zitakazowawezesha kujenga hoja juu ya madai yao.
Tukumbuke kuwa migodi yote ilikuwa imeshikilwa na vigogo wa RICHMOND hivyo wameteteraka sana kwa sasa na sheria zinawabana ktk kona mbalimbali ikiwepo mitaa ya kodi n.k
Mfano jamaa RA ndiye mwenye contract za kuchimba dhahabu ktk migodi yote na kampuni ianyochimba haina mining license yet akataka kusamehewa kodi ya mafuta ... ila hivi majuzi kibao kimegeuka na kula penalt a kufa mtu!!! hata hivyo wakati Chiligati alipotangaza kupanda kwa kima cha chini kwenye sekta ya madini yeye RAziz na kampuni yake ya Capsian walikataa kuwapa wafanyakazi wachimbaji kwa madai kuwa kampuni yake inayochimba ni industry na siyo ya mining ... hivyo wenzetu wa baadhi ya miigodi bado wanasota hawajpata mishhara mipya!!!

Tujiulize iweje industry ikachimbe wakati huohuo watake kusamehewa kodi ya mafuta wakati hawana mining license??? Halfu itakuwaje kampuni ambayo haina mining license ipewe kazi kubwa kama hiyo??? POLITIC NDUGU!!!

Poleni kwa kuwaletea habari ndefu ila nadhani ina uhusiano mkubwa na kilio cha wananchi wa Buzwagi .... kwani wanolia siyo walio nje tu hadi wafanyakazi wa migodini ... they are going through hell!!!!
 
Icadon, sheria ya TISS inasema wapi kuhusu kuwa na wafanyakazi wa TISS kwenye balozi zetu?

Nadhani kabla ya kujiuliza swali hili tujiulize kwanza, kwa nini TISS kuna Kurugenzi ya Usalama wa nje?( External Intelligence.. whatever they call it!) Bila shaka wafanyakazi wa TISS walioko kwenye balozi zetu ni agents toka idara hii!

Kwa maoni yangu, tatizo ni muundo wa vyombo vyote usalama ukiondoa jeshi!
Hakuna maana ya kuwa na TAKUKURU, Financial Intelligence Unit , TISS na idara zake zote pamoja na Jeshi la Polisi!
Muundo huu umekaa kama bado tuko kwenye Cold War!

Ingekuwa bora kama TAKUKURU, FInancial Intelligence Unit, Internal Intel, na part ya CID-Police wakajumuishwa pamoja then ikaundwa Law Enforcement Agency moja itakayo-deal na Criminal Investigation. Reason kubwa ni kwamba.. no matter what we call it.. Rushwa na shughuli zake ni CRIME.. period!

IN addition, TISS ingeachwa na External Intel pamoja na Idara nyingine zilizobakia. Maana tukizungumzia Ujasusi sio ujasusi wa kukimbizana Manzese.. it is all about Espionage!! Kuiba siri za mataifa mengine via Open Source Data Collections au Covert Operations kwa manufaa ya taifa letu.. ziwe siri za kiuchumi, kiusalama etc!
Ili kuendana na kauli-mbiu ya Economic Diplomacy itabidi tu TISS ibadilike! Makaburu wameshaacha fujo zao.. fujo zimehamia kwenye vita ya kiuchumi!

Mwisho kabisa, jeshi la polisi lifanyiwe mabadiliko lifanye kazi kama majeshi ya polisi ya nchi nyingine.. Policing Community!
Muundo wa sasa ni mgumu.. hauna tofauti na Polisi wa Eastern Bloc wakati wa Cold War! hatuhitaji hii kitu tena.. twende na wakati. Polisi anavaa gwanda wakati hajui hata kuendesha gari?
 
kama mwambata wetu wa jeshi Col GK aliwahi kuzungumzia hii issue ya radar haingii akilini kuwa iliwapita watu wa TISS....

Sawa sawa, unajua ninamuaminia sana mkulu GK maana ni kichwa haswa, sasa kwa yeye kuhoji hivi.....!

Mkuu Brutus,

Maneno mazito sana hayo!
 

HAPA NINAKUBALIANA NAWE KUWA RAIS ANAPASWA AFANYE MAAMUZI BEYOND DOUBTS KINYUME CHA HAPO ATAUA WENGI KAMA SI KUWAFUNGA LILILO LA MBOLEA KWA MFANO WA NGASONGWA MKUU ILIKUWA NI ANDREA NA WALE AMBAO WAKO SERIKALINI NA TAYARI WANATAJWA KWA KUTUHUMIWA KWA JAMBO HILI NA LILE BASI NI VEMA WAREJEE UJASIRI WA NGASONGWA WA KUJIUDHURU NA KUOMBA WACHUNGUZWE,KWA MANENO YAKE NGASONGWA ALIMUOMBA RAIS AJIUDHURU ILI KUMSAIDIA KTK KUFANYA MAAMUZI YENYE FAIDA KWA NCHI,HAWA WATU WOTE JK ALIWATEUA KWA KUWAAMINI NA NI MFUMO HUO HUO WA KUAMINIANA NDIO WANAOPASWA KUUTUMIA KUWA MZEE HAPA TUMESHATAMKWA ,KWA UAMINIFU WAKO KWETU NASI TUNAKUREJESHEA NAFASI ULIZOTUPA ILI SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE,KINYUME CHA HAPO WATAIBUKA KINA KIULA KILA KUKICHA PASIPO SABABU YA MAANA, KTK HILI JK ALITEGEMEA ALICHOFANYA CHENGE JUZI; TUSUBIRI MATOKEO YA UCHUNGUZI. KUHUSU HAWA WAZEE WA MIWANI MYEUSI AU KAMPUNI YA NYASI KUNA WAKATI TUNA HAKI YA KUWALAUMU KWANI SISI TUNATEGEMEA WAO WASIMAMIE UZALISHAJI WA VIONGOZI BORA ,VIONGOZI WASIO NA MAWAA YA UPORAJI WALA DAMU SASA WAO HILO WAMELIACHA NA KUWAACHA PCCB AMBAO KIKATIBA NDIO WENYE MAMLAKA LAKINI SOTE TUNATAMBUA NI CHOMBO KICHANGA KIISICHO NA UZOEFU WALA MABAVU YENYE KUMAANISHA KUPIGANA NA RUSHWA,NILIDHANIA WAKUU WA KAMPUNI YA NYASI WANGELISAIDIANA NA PCCB KUKOMA NYANI GILADI THEN VIJANA WA MWEMA WANGELISIMAMIA SOESI LA KUWAGWARIDISHA WANAOTUHUMIWA KABLA YA PILATO KUWAPATIA MAMLAKA MAGEREZA KUWAPATIA KAZI NGUMU NA MLO MMOJA LAKINI KUNA WAKATI HAWA JAMAA WA KAMPUNI YA NYASI INAJIKUTA INAVULIWA NGUO NA WANASIASA,MAANA NA WAO UHAI WAO NI WANASIASA HAPO KAZI KWELIKWELI,AKINA ANDREA HAWA NI WAWAKILISHI WA WANANCHI SASA UNAPOMVUA NGUO PASIPO HEKIMA NI KUITUKANA SERIKALI HIYOHIYO, NI WATU WENYE SIRI ZA NCHI LAKINI WANAFANYA KAZI KTK MAZINGIRA MAGUMU SANA KULIKO HATA SHETANI. ALL IN ALL WAICHUKUE HII KAMA CHANGAMOTO NA WAANGALIE MBELE KITAALAMU ZAIDI.NINAWASILISHA
 
Mkuu FEMS,
Naomba samahani sana kwa kukushupalia kuhusu kumtetea RO na kisha kumgeuka. Baada ya kusoma kwa makini niligundua kuwa mtu uliyekuwa unamtetea sio RO ni Mzee Malecela.
 

Mkuu,
Umenikumbusha mbali sana na issue ya Vector 21, kuna mtu alikaribia kukata mawasiliano na mimi baada ya kuiona kwenye pc.

Uliyoyasema hapo juu yote tumeyajadili HAPA
Nakubaliana na wewe mia kwa mia.
Tatizo kubwa na nitaendelea kulisema ni wanasiasa kutaka kugeuza kila kitu siasa na kikukiendesha kisiasa.
 
Tanzania Intelligence and Security Service Act (Act no 15 of 1996)

For many years, the Tanzania intelligence service was a mythical entity. Service personnel were feared and shunned by society. They were negatively labelled as ‘flies’, ‘peeping Toms’, and others. They also had unlimited funds to use allegedly in pursuit of ‘enemies of the state’. Yet, they were above all using the taxpayer’s money without being accountable. This was considered to be unfair, hence, the enactment of the Tanzania Intelligence and Security Service Act. This legislation is primarily aimed at demystifying the so-called secret service and making it transparent and accountable to the public.

The Act formally establishes the Tanzania Intelligence and Security Service (TISS) as a government department in the Office of the President, with its main function to ensure security in the country.39

The Service is supposed to collect, analyse and retain information which, on reasonable grounds, is suspected to relate to activities that constitute a threat to the security of the United Republic of Tanzania or any part of it.40 In order to collect information, the Service has the power to investigate any person or body of persons who may cause a threat to the security of the country. In the course of the investigation, the service may enter into arrangements with international organisations to provide the government with security assessments.41 This is in line with article 13 of the Convention. Under this article, state parties are urged to enter into arrangements to establish joint investigation bodies. It is emphasised, however, that in the course of this form of co-operation, respect for the sovereignty of the other country must prevail.

Understandably, the duties of the Service are performed secretively. Information can only be disclosed for investigation purpose and in the public interest.42 Thus, there is protection of officials and employees of the Service, as well as their sources of information.43 In addition, employees of the Service are legally protected for acts bona fide done or omitted in relation to their duties and functions. Sources of information to the Service are protected, and no particulars of a person who is a confidential source of information will be disclosed. This form of protection is also covered by the Convention in relation to witnesses.44 It is an offence to obstruct an employee of the Service in the course of duty.45

The intelligence service in any country, if properly utilised, can play an important part in the war against organised crime.
 

Icadon,

What else do we need to tell Wananchi kuwa TISS has failed to provide security to the country?

Maana suala la IPTL na Richmond pekee pamoja na uhujumu wa kipesa, matokeo ya kugotagota kwa kupatikana umeme ni tishio kwa usalama wa Taifa kwa kutufikisha mahali tunategemea kila kitu kiwe cha kuagizwa kwa kuwa viwanda vyetu havina nyenzo kuu ya kusaidia uzalishaji mali wao.

Ama kuongezeka kwa uagizaji na kuduma kwa mauzo ya bidhaa zetu nje, kunadumaza ukuaji wa nguvu ya sarafu yetu na hivyo kuishia thamani ya pesa yetu kushuka na uchumi kuyumba.

Tukija kwenye mambo ya ufisadi uwe wa ATCL, TRC, Buzwagi, Radar na hata kero nyingine. Usalama wa Taifa letu umewekwa mikononi mwa wachache wenye nia ya kuuchezea na kutudhoofisha kama Taifa.

Sasa kama vitendo hivi ni dhahiri vinadhoofisha afya ya taifa letu na chombo kikubwa cha kulinda Usalama na maslahi ya Taifa kilikuwa kinagota au kinashiriki katika "uhujumu" (Kagoda please!) je kuna faida gani kwa chombo hicho kuendelea kufanya kazi bila kuwajibika?
 

Shhhh!! Angalia wasije kusema una chuki binafsi lol.....I guess we need to define the term usalama wa taifa...maana vitu vingi vinaweza kuhatarisha usalama wa taifa sio lazima iwe uvunjaji wa amani tuu kwa kutumia silaha.
 
Icadon, "usalama wa Taifa" has already been defined, labda useme in light of what is going on.. there is an urgent need to redefine "Usalama wa Taifa".
 
Ukisoma Strategic Intent 2007-2011 ya CIA utakutana na hiki kitu ambacho Tanzania tunakipuuzia.

Open Source. Juzi Simba kasema eti hatuwezi kuanza uchunguzi kwa kusoma magazeti! Hivi leo nikiandika nataka kuzalisha koboko pale jirani na Bunge, watalichukulia kimzaha?

 
Angalia ya wenzetu..

 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…