Rashid Othman: Umeshindwa Jiuzulu!

Rashid Othman: Umeshindwa Jiuzulu!

Status
Not open for further replies.
Mhe, Kinvaba

Inaelewa kuwa Hakuna Taasisi hata moja nyeti hapa Tanzania ambayo vijana wa RO hawajaingizwa, Hii nina maana BOT< TRA< Bandari, Tanesco, wizara zote kubwa zikiwemo za nishati nk.

Sasa hebu tueleze hao vijana huko wanafanya kazi gani na wamepelekwa kwa niaba ya nani?

Sisi tunaelewa kuwa wamepelekwa na RO na kwaniaba ya TISS kufanya kazi zikiwemo za TISS pia. Tueleze sasa wakati KASHFA zote hizi zinafanyiwa wao walikuwa wapi? ama na wao ni miongoni mwao hao MAFISADI.

RO tueleze baada ya kuletewa taarifa na vijana wako ziliichia wapi? na kama Ulizipeleka hazikufanyiwa kazi , KUna maana gani yakuwa na hiyo IDARA. Ukurugenzi wako ni upi hasa ama ni wa kupeleka UMBEA tu.

KAma hujapokea hizo ripoti zi ujiuzulu kwa kushindwa kazi iwe wewe binafsi ama hao WAMBEA wako waliopo huku maidarani.
 
I got a story to tell about Usalama wa Taifa.

In early 80's we had a birthday party at home, Muziki ulikuwa unatwanga kwenye kinu cha wati 100, tumekaa tunaserebuka, ghafla bin vup, likaingia gari wakashuka jamaa wawili. Wakauliza Mzee mwenye nyumba yupo wapi? tukampeleka kwa Mzee Kishoka.

Sikujua kilichotokea mpaka miaka 12 baadaye, wakati Mzee Kishoka tunapiga stori akanikumbusha ile party ya Bafudei! Akaniambia "unajua ni nani wale waliokuja siku ile?" nikamwambia sijui. Akaniambia wale jamaa walikuwa jamaa wa Usalama wa Taifa. Walikuja kuuliza ni wapi Mzee Kishoka alitoa Kinu chenye kutwanga Mziki kwa nguvu kiasi hicho, wakadai mpaka stakabadhi, kisha wakaondoka.

Sasa ikiwa sauti kubwa ya mziki na pati ya watoto iliwaleta Usalama wa Taifa nyumbani kwetu, inakuwaje "vijisenti" vimewapita kando?

..duh! baabu kubwa!

..sasa kama awali walifuata vitu visivyohusika,basi itakuwa wanafuata hivyo hivyo. ndo maana hizo senti hawazioni!.
 
Which tells you that even though it was odd, but UWT was efficient about "Maslahi" ya Taifa that they needed to know where would one have a Sansui amplifier and Garrand turntable with Quadraflex speakers while kila mtu alikuwa anahimizwa awe na Redio ya Neshno kama si Phillips ndiyo yenyewe.

At least there was accountability to follow up on petty things that were considered "luxury", sasa the real Luxury is being minimized as "vijisenti" and UWT feels no obligation to pekua the source of "vijisenti"!

Are they belly full after their own "vijisenti" vya Kagoda?

..umenikumbusha mbali!

..hii kitu ilikuwa inatoa muziki mnene kichizi!
 
Kama kigezo ni hicho basi hata PPRA nao wajiuzuru, maana na wao walitoa ushauri lakini ukapuuzwa na timu ya mzee "Bangusilo".

Jamani haya mambo sio rahisi kama tunavyofikiria. Hivi kujiuzuru kwa yule afisa wa Kilimo wa Arusha kuliweza kuleta mabadiliko ya ufanisi ktk wizara husika?

Kumbukeni kuwa tuna wanasiasa (kazi yao ni kufanya maamuzi) na tuna watendaji (washauri). Ni mara ngapi tumeshuhudia viongozi wakubwa duniani wanafanya maamuzi wayapendayo wao na bila kuzingatia ushauri wa wataalam?

Leo hii Othman akijiuzuru eti kwa kufurahisha "umma" ataenda kuishi wapi? nae kwao ni Tanzania? Ningekubaliana na mtoa hoja kama kujiuzuru kwa OR kungeleta mabadiliko ya kimfumo, lakini eti ajiuzuru halafu arudi kijini kwao kwenda kulima machungwa, mimi sioni kama ni ushujaa huu.

Namshauri Othman ASIJIUZURU bali ajitahidi kusikiliza malalamiko ya watu dhidi ufisadi na pale anapoweza kuliokoa taifa basi afanye hivyo.
 
Kama kigezo ni hicho basi hata PPRA nao wajiuzuru, maana na wao walitoa ushauri lakini ukapuuzwa na timu ya mzee "Bangusilo".

Jamani haya mambo sio rahisi kama tunavyofikiria. Hivi kujiuzuru kwa yule afisa wa Kilimo wa Arusha kuliweza kuleta mabadiliko ya ufanisi ktk wizara husika?

Kumbukeni kuwa tuna wanasiasa (kazi yao ni kufanya maamuzi) na tuna watendaji (washauri). Ni mara ngapi tumeshuhudia viongozi wakubwa duniani wanafanya maamuzi wayapendayo wao na bila kuzingatia ushauri wa wataalam?

Leo hii Othman akijiuzuru eti kwa kufurahisha "umma" ataenda kuishi wapi? nae kwao ni Tanzania? Ningekubaliana na mtoa hoja kama kujiuzuru kwa OR kungeleta mabadiliko ya kimfumo, lakini eti ajiuzuru halafu arudi kijini kwao kwenda kulima machungwa, mimi sioni kama ni ushujaa huu.
Namshauri Othman ASIJIUZURU bali ajitahidi kusikiliza malalamiko ya watu dhidi ufisadi na pale anapoweza kuliokoa taifa basi afanye hivyo.

Nani kasema kuwa Othman atajiuzulu kwa kufurahisha umma? Unarudiarudia maneno yako mwenyewe kwenye hili hadi unaanza kutia aibu sasa!
 
..ngoja tuendelee ku-beat around the bush!

..wote tunajua nani anatakiwa kujiuzulu!

..na kazi itaendelea vile vile!
 
1. Tutumie akili zaidi kuliko jazba ktk kumhukumu Othman jamani.

Mkuu heshima yako mimi nafikiri wewe ndiye uanze kutumia akil;i kwenye kumtetea kuliko kutumia jazba, kwa sababu sisi wa-Tanzania, sio wajinga kiasi hicho, inapofikia waziri S. Simba anasema kuwa hana taarifa za Chenge, kuwa na hizo hela nje, basi ina maana usalama hawana habari hizo au hawakuwa na hizo habari, sisi hapa wengine ni watu wazima sana mkuu, kama umeamua kumtetea basi kuwa makini na hoja zako, kwa sababu hii Tanzania ni yetu sote yeye na sisi wananchi, sasa viongozi kama yeye wasibweteke na kuamini kuwa wao ni semi-Gods,

Mimi ni mwananchi m-Tnazania na sina wasi wasi wowote kwenye kusema wazi hapa JF, kuwa ni wakati muafaka wa Mkurugenzi wa sasa wa usalama, ameshindwa kazi au haelewi kazi yake ni nini, lakini as a nation hatuwezi kuendelea na hii aibu na uzembe, na hasa incompetency, kama hoja yako inatakiwa kusimama basi Lowassa angeeendelea tu maana kilichobadilika ni nini? Hoja kama hiii inaonyesha uwezo mdogo sana wa kufikiri au kuelewa siasa ya taifa laklo wenyewe kwa sababu unapaswa kuelewa kuwa kuna taifa la kesho ambalo litakuja kuongozwa na historia ya siasa za sasa, kwa hiyo kama tunao utamaduni wa kujiuzulu kwa viongozi wetu kunapotokea mapungufu katika uongozi wao, wao taifa la kesho hawatakuwa na wasi wasi wowote ikibidi kiongozi wao ajiuzulu,

Yes, mkurugenzi wa Usalama anahusika moja kwa moja na sio tu hii kashfa ya Chenge, bali hata za Richmond na Radar, pia kwa sababu:-

1. Alitakiwa kumfahamisha rais wa jamhuri mapema kuwa viongozi kama Lowassa, Karamagi, Msabaha, na huyu sasa Chenge kuwa hawafai, kwa hiyo rais asingewapa madaraka, hata kama kuna yaliyofanyika kabla hajaingia, bado zilitakiwa kuwepo ripoti za usalama kwenye mafaili, na Chenge asingepewa tena madaraka na rais kwenye cabinet ya pili.

2. Kama alimshauri rais na rais hakumsikiliza, siku zote kuna njia nyeupe ya kwenda bungeni kusema kilio chake, au kumfahamisha waziri wake, au kamati ya bunge ya usalama, so far viongozi karibu wote wa hivyo vitengo hawana habari za Chenge kuwa na hizo hela nje, hata kwenye fomu za bunge hakusema, rais wa jamhuri hawezi kuwa nchi za nje kwenye ziara za kitaifa, halafu anaanza kuulizwa maswali ya hela za Chenge, nje hana majibu, sasa wa kulaumiwa hapa unasema sio usalama? Hao maofisa wote walioko nje tunaowalipia hela zetu za kodi wanafanya nini? Mbona mambo madogo madogo yasiyokuwa na miguu wala kichwa ya wananchi walalahoi wanaripoti? Kiongozi wa high profile kama Chenge, anwezaje kwenda nje mpaka kufungua accounts za mahela yote hayo bila usalama wetu kujua? hivi huoni kuwa hii ni insane kama sio insanity?

3. Kumshambulia Mwanakijiji as a personal, kwa ishu ambayo ni muhimu kwa taifa kama hiii ni kufukuza hewa, hii ishu inasimama yenyewe, wazi kuwa usalama ume-mfail rais na sisi wananchi wote, halafu cha muhimu zaidi ni kwamba when it is going to stop, yaani taifa ku-focus na mafisadi? Majina yalipotolewa na Dr. Slaaa ya mafisadi, je usalama walifanya nini as far as kufuatilia is concerned? Hivi wewe huwezi hata ukajirudi kidogo na kuona kuwa iwapo wangefuatilia yale majina ya mafisadi, wangeweza kujua haya mapema, badala ya kusubiri kuja kuambiwa na wazungu?

The bottom line ni kwamba makosa siku zote yanahitaji marekebisho, kwenye hili usalama ni 100% responsible, wana maofisa huko nje, waliambiwa na Dr. Slaaa majina ya mafisadi la Chenge likiwemo, kuna msaada wa interpol wangeweza kuomba na wangepewa, viongozi wote wanaotakiwa kuwa walikuwa wanajua katika system yetu kuanzia political mpaka legal, hawajui kuhusu hii habari ya Chenge, sasa ni wakati muafaka kwa usalama wa taifa kuwajibika na huu uzembe, ninauita uzembe kwa sababu kilichotakiwa ni kufuata sheria tu na resources zote wanazo.

Halafu, achana na haya maneno ya eti usalama hawawezi kuja kujibu hapa, mkuu wengine hatukuzaliwa jana hapa, tunajua majibu yaliyotoka usalama na yasiyotoka huko so far kwenye hiii topic, mimi binafsi ninasema haya tena bila wasi wasi wowote, kati ya nyie manojaribu kuandika maneno ya kuwatisha wengine, ninasema hivi haijavunjwa sheria yoyote kwenye mwananchi wa Tanzania, kama mimi na wengine wote hapa tunaodai kwa njia za siasa za kistaarabu kwamba mkurugenzi wa usalama ajizulu, kama kuna anayetaka kunijua au kunishika kwa kuwa nina haya mawazo, asihangaike sana nitafute kwenye pm niambie tukutane wapi, wananchi tunaazna kufika mwisho sasa, enough is enough zile enzi zimeisha za kulindana,

Mkurugenzi wa Usalama ajiuzulu tu kumpa nafasi rais ya kuanza upya tena, ikiwa ni pamoja na Chenge naye kujiuzulu sasa.

Ahsante na Heshima Mbele!
 
Mkulu, I standa by my point, TISS wana power ya kuarrest labda useme inategemea na uzito wa jambo...
Kama "hawana" hiyo power whats the point ya kuwa na kitengo cha Internal Security?
 
Mkulu, I standa by my point, TISS wana power ya kuarrest labda useme inategemea na uzito wa jambo...
Kama "hawana" hiyo power whats the point ya kuwa na kitengo cha Internal Security?

Mimi mwenyewe nilikuwa namshangaa anavyojikoroga kwenye hiyo power ya kuarrest.
 
Othman akiondoka muungwana atateua incompetent mwingine, mradi awe swahiba wake.

Kama kaweza kum reappoint Chenge na frauds wengine kama kina Mkulo na Nchimbi atashindwa nini kwenye hili?.

We need a regime change, nothing less.
 
Icadon na Bimdogo.. ni kweli hawana nguvu ya kukamata... lakini jiulize ni kwanini hawana nguvu ya kukamata... the answer will chill you...
 
Pamoja na kwamba hawana nguvu ya kukamata lakini wamekuwa wakiwaweka watu chini ya ulinzi bila hata ruhusa yeyote kutpka mamlaka zinazohusika, ila wakiona unafahamu kuwa hawana nguvu ya kukamata the wanakuacha na kufuata taratibu, lakini kama hilo ulijui watakuendesha sana.
 
Icadon na Bimdogo.. ni kweli hawana nguvu ya kukamata... lakini jiulize ni kwanini hawana nguvu ya kukamata... the answer will chill you...

I have seen them arresting people..tena kwa mikogo mingi ya kuonyesha vitambulisho...

What is the answer?
 
ukweli ni kuwa hawa jamaa wanaangalia na sura za kuwakamata...hawakurupuki tu
 
Waungwana,
Huu mjadala unakosa utamu, nafikiri tumtafute kwanza Tafit then Jadili.
Maana yaliyosemwa wakatia anateuliwa aliyapinga na sasa ndo sura ya RO imeonekana kweupe
 
Icadon na Bimdogo.. ni kweli hawana nguvu ya kukamata... lakini jiulize ni kwanini hawana nguvu ya kukamata... the answer will chill you...



Kama hawana nguvu ya kukamata, wameipata wapi mpaka wakaweza kumtia nguvuni Kitila baada ya kuulizia habari za EPA?!!
 
Kama hawana nguvu ya kukamata, wameipata wapi mpaka wakaweza kumtia nguvuni Kitila baada ya kuulizia habari za EPA?!!

Kitila hajatiwa nguvuni bwana, yuko as free as a molecule akamatwe kwa kosa gani?
 
...RO ni Head wa Intelligence Tanzania.

...RO kazi yake namba moja ni kuhakikisha usalama wa mafisadi, wewe unategemea nini?

Sidhani kama Rashid Othman ana maagizo ya kuchunguza wizi wa hela. TUKUKURU na Tume Ya Maadili ndio kazi zao. Nadhani Rashid Othman hata majambazi wanaotishia maisha ya watu hawamhusu. Sio maagizo ya kazi yake.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom