1. Tutumie akili zaidi kuliko jazba ktk kumhukumu Othman jamani.
Mkuu heshima yako mimi nafikiri wewe ndiye uanze kutumia akil;i kwenye kumtetea kuliko kutumia jazba, kwa sababu sisi wa-Tanzania, sio wajinga kiasi hicho, inapofikia waziri S. Simba anasema kuwa hana taarifa za Chenge, kuwa na hizo hela nje, basi ina maana usalama hawana habari hizo au hawakuwa na hizo habari, sisi hapa wengine ni watu wazima sana mkuu, kama umeamua kumtetea basi kuwa makini na hoja zako, kwa sababu hii Tanzania ni yetu sote yeye na sisi wananchi, sasa viongozi kama yeye wasibweteke na kuamini kuwa wao ni semi-Gods,
Mimi ni mwananchi m-Tnazania na sina wasi wasi wowote kwenye kusema wazi hapa JF, kuwa ni wakati muafaka wa Mkurugenzi wa sasa wa usalama, ameshindwa kazi au haelewi kazi yake ni nini, lakini as a nation hatuwezi kuendelea na hii aibu na uzembe, na hasa incompetency, kama hoja yako inatakiwa kusimama basi Lowassa angeeendelea tu maana kilichobadilika ni nini? Hoja kama hiii inaonyesha uwezo mdogo sana wa kufikiri au kuelewa siasa ya taifa laklo wenyewe kwa sababu unapaswa kuelewa kuwa kuna taifa la kesho ambalo litakuja kuongozwa na historia ya siasa za sasa, kwa hiyo kama tunao utamaduni wa kujiuzulu kwa viongozi wetu kunapotokea mapungufu katika uongozi wao, wao taifa la kesho hawatakuwa na wasi wasi wowote ikibidi kiongozi wao ajiuzulu,
Yes, mkurugenzi wa Usalama anahusika moja kwa moja na sio tu hii kashfa ya Chenge, bali hata za Richmond na Radar, pia kwa sababu:-
1. Alitakiwa kumfahamisha rais wa jamhuri mapema kuwa viongozi kama Lowassa, Karamagi, Msabaha, na huyu sasa Chenge kuwa hawafai, kwa hiyo rais asingewapa madaraka, hata kama kuna yaliyofanyika kabla hajaingia, bado zilitakiwa kuwepo ripoti za usalama kwenye mafaili, na Chenge asingepewa tena madaraka na rais kwenye cabinet ya pili.
2. Kama alimshauri rais na rais hakumsikiliza, siku zote kuna njia nyeupe ya kwenda bungeni kusema kilio chake, au kumfahamisha waziri wake, au kamati ya bunge ya usalama, so far viongozi karibu wote wa hivyo vitengo hawana habari za Chenge kuwa na hizo hela nje, hata kwenye fomu za bunge hakusema, rais wa jamhuri hawezi kuwa nchi za nje kwenye ziara za kitaifa, halafu anaanza kuulizwa maswali ya hela za Chenge, nje hana majibu, sasa wa kulaumiwa hapa unasema sio usalama? Hao maofisa wote walioko nje tunaowalipia hela zetu za kodi wanafanya nini? Mbona mambo madogo madogo yasiyokuwa na miguu wala kichwa ya wananchi walalahoi wanaripoti? Kiongozi wa high profile kama Chenge, anwezaje kwenda nje mpaka kufungua accounts za mahela yote hayo bila usalama wetu kujua? hivi huoni kuwa hii ni insane kama sio insanity?
3. Kumshambulia Mwanakijiji as a personal, kwa ishu ambayo ni muhimu kwa taifa kama hiii ni kufukuza hewa, hii ishu inasimama yenyewe, wazi kuwa usalama ume-mfail rais na sisi wananchi wote, halafu cha muhimu zaidi ni kwamba when it is going to stop, yaani taifa ku-focus na mafisadi? Majina yalipotolewa na Dr. Slaaa ya mafisadi, je usalama walifanya nini as far as kufuatilia is concerned? Hivi wewe huwezi hata ukajirudi kidogo na kuona kuwa iwapo wangefuatilia yale majina ya mafisadi, wangeweza kujua haya mapema, badala ya kusubiri kuja kuambiwa na wazungu?
The bottom line ni kwamba makosa siku zote yanahitaji marekebisho, kwenye hili usalama ni 100% responsible, wana maofisa huko nje, waliambiwa na Dr. Slaaa majina ya mafisadi la Chenge likiwemo, kuna msaada wa interpol wangeweza kuomba na wangepewa, viongozi wote wanaotakiwa kuwa walikuwa wanajua katika system yetu kuanzia political mpaka legal, hawajui kuhusu hii habari ya Chenge, sasa ni wakati muafaka kwa usalama wa taifa kuwajibika na huu uzembe, ninauita uzembe kwa sababu kilichotakiwa ni kufuata sheria tu na resources zote wanazo.
Halafu, achana na haya maneno ya eti usalama hawawezi kuja kujibu hapa, mkuu wengine hatukuzaliwa jana hapa, tunajua majibu yaliyotoka usalama na yasiyotoka huko so far kwenye hiii topic, mimi binafsi ninasema haya tena bila wasi wasi wowote, kati ya nyie manojaribu kuandika maneno ya kuwatisha wengine, ninasema hivi haijavunjwa sheria yoyote kwenye mwananchi wa Tanzania, kama mimi na wengine wote hapa tunaodai kwa njia za siasa za kistaarabu kwamba mkurugenzi wa usalama ajizulu, kama kuna anayetaka kunijua au kunishika kwa kuwa nina haya mawazo, asihangaike sana nitafute kwenye pm niambie tukutane wapi, wananchi tunaazna kufika mwisho sasa, enough is enough zile enzi zimeisha za kulindana,
Mkurugenzi wa Usalama ajiuzulu tu kumpa nafasi rais ya kuanza upya tena, ikiwa ni pamoja na Chenge naye kujiuzulu sasa.
Ahsante na Heshima Mbele!