Capital
JF-Expert Member
- Oct 12, 2010
- 1,468
- 1,063
Naanza kuwa na mashaka sana na wewe..Ni rahisi sana kusema unapounda.majimbo unataka.kuwasogegezea karibu Wananchi huduma lakini kuna huduma zilokaribu na Wananchi kuliko Serikali za Mitaa?
Kumbuka tu kwamba hakuna kubwa.ambalo Seeikali ya Majimbo.itafanya dhidi ya Serikali Kuu kuliko serikali za mitaa ambazo zina ukubwa mdogo na kata chache zaidi lakini ndiko Ubadhilifu mkubwa unatokea.
Now, imagine unaongeza wigo kuwa na Majimbo mathlan Shinyanga, Mwanza, Geifa, Mara na Bukoba! Halafu uunde serikali yake na Bunge lake! Patakuwa na wabunge wa jimbo hilo pia Wabunge wawakilishi Bunge la JMT. Fedha hizi za matumizi haya makubwa zitatoka wapi?
Ikiwa.mimi napingana na Seeikali 3, halafu unanambia acha 3 tuunde Majimbo ina maana unaunda Seeikaki Isopungua 6 zenye viongozi na Wabunge wake kisha bado wa Kitaifa!
Kwani Mikoa na Wilaya zina kasoro zipi? Bila shaka ni UTUMISHI yaani hakuna UWAJIBIKAJI. Kama haya yanakosekana na WATU ni walle wale tulonao huoni kwamba tatizo ni WATU sio UTAWALA?
Sisi watumishi ndio tatizo hata kama.tutagawa nyumba kwa nyumba shida zitabakia palepale. Tatizo ni TAASISI zeru haziwajibiki. La kufanya ni.kutafuta mbinu ziwajibike. Kila mmoja wetu aogope kuiibia serikali. Na ndivyo wenzetu waliweza kufanikiwa kwa sababu kila mtumishi ana wajibu na nishani ya kazi.
- Sisi ni Kanyaga Twende, tumechelewa mno..
Serikali za mitaa unazoongelea hapa ni institutions za kipuuzi sana hapa Tanzania. Hazina uwezo wowote na hazitofautiani na zile za wakati wa ukoloni. Kimsingi serikali ndo inataka iwe hivyo.. kazi yake ni unyampala dhidi ya wananchi.. hakuna aliyezichagua, zinawajibika kwa aliyeziteua na si vinginevyo. Tunataka mkuu wa mkoa awajibike kwa wananchi moja kwa moja na si kwa Rais aliyemteua.
Hii ndo maana halisi ya kuwa wenye nchi ni wananchi