Baadhi ya Malengo;
1 - ni kusogeza uwajibikaji wenye maana karibu zaidi kwa Wenye-nchi (Wananchi).
2 - kutenganisha majukumu, mipango ya maendeleo na utekelezaji wake, etc ya Kitaifa (yanayohusi Taifa zima) na ya kijimbo (Yanayohusu au Yaliyo na maana katika Jimbo)
3 - Kusaidia kupunguza mzigo mkubwa wa majukumu aliyonayo Raisi, kutoka majukumu ya sasa yanayohitaji Raisi mwenye uwezo wa "kiMungu" ili kutelekezeka ipasavyo, kwenda majukumu yanayoweza kutekelezeka na Bin-Adamu mwenye uwezo wa wastani na kuendelea.
4 - Kusaidia kupunguza madhala ya makosa yanayofanywa na viongozi wa Kitaifa ( na hata yatakayokua yanafanywa na viiongozi wa Kimajimbo.
5 - Kuipa Serikali ya Kitaifa/Kuu (Kwa kushirikiana na Serikali za Majimbo) wajibu na nafasi ya kutunga, kusimamia na kurekebisha Miongozo mbalimbali, ambayo itatumika kama Mahitaji ya kima cha chini katika upangaji na utekeleza wa shughuli za maendeleo nchi nzima.
6. N.K
- Kuwe na mambo ya Kitaifa na mambo ya Kimajimbo. Watumishi watawajibika kwa wasimamizi wao. Ajira zao, Mishahara yao itatoka sehemu waliyo ajiliwa. Mfano mwalimu wa shule ya msingi A katika Jimbo A, atawajibika kwa Mwalimu mkuu wa shule hiyo, na kulipwa na Jimbo A. Mhasibu wa TCRA tawi la Jimbo A, atawajibika kwa Mhasibu-mkuu, makao makuu ya TCRA, na atalipwa mshahara kutoka serikali kuu.
- Mapato katika Majimbo yagawanywe, ili kiasi kibaki katika Jimbo na Kiasi kiende Serikali kuu.
Leo liwe kutotegemea misaada, huku tukiwa na nchi Tajiri kabisa. Hata hivyo, misaada huja kwa lengo fulani.
Misaada itumike kutegemea malengo ya misaada hiyo.
Itengenezwe miongozo ya kifedha itakayo hakikisha ubadhilifu unazuiwa kabla haujatokea, na Ukitokea miongozo irekebishwa kuhakikisha hautatokea tena.
- Naamini, mfumo wa Majimbo hautakosa changamoto. Lakini faida zake zinahalisha, uthubutu wa kujikita katika kutatua changamoto hizo.
- Tanganyika ina historia yake. Mfumo wetu wa Majimbo, utakone na hali, historia na mahitaji yetu.