Sorry, hiyo ni muundo wa Serikali ya Tanganyika siyo Zanzibar...kwa Zanzibar Sina cha kupendekeza kwenye katiba make nataka serikali tatu.Unisamehe nitakuwa nauliza.maswali kama nilivyojeleza toka mwanzo. Usjje dhani napingana na wewe laa hasha.
1. Umeseme Waziri Mkuu atakuchukua nafasi ya rais lakini huyu ni mbunge alochaguliwa na jimbo lake na kupitishwa na Bunge. Hii itazaa hoja nyingine kuwa Waziri Mkuu huyu wa Tanganyika atakuwa katika Katiba ya Tanganyika sio Katiba ya Muungano wakati Makamu wa rais ni hoja ya Katiba ya JMT. Unapomuondoa Makamu ya rais inatakiwa Waziri Mkuu pia alokubalika pande zote mbili za Muungano.
2. Utawezsje waondoa Wabunge wa Majimbo 214 ili kuunda Bunge kulingana na mikoa ikiwa leo kuna majimbo yanatakiwa kuongezwa kwa madai ya UKUBWA wake? Hili sidhani kama litaungwa mkono.
Rais wa nchu lazima awe na Mamlakannchi nzima.na nsjo sababu ya kuwepo Wakuu wa Mikoa na Wilaya kama representantive wa dola. Kama haitakuwa hivyo, rais atakosa mamlaka ya mikoa na kuna hatari ya baadhi mikoa kujiamlia mambo yao wenyewe. Waziri Mkuu ni msimamizi wanutekelezaji wa Serikali ambayo haina mwakilishi Mikoani. Serikali inaundwa na rais..
Suala la kugawa majimbo yaliyopo ni tamaa za viongozi ndiyo maana napendekeza yarudi kuwa mkoa mmoja mbunge mmoja...tukiruhusu kugawa majimbo...mwisho wa siku Tarafa itakuwa jimbo na kuwa na mwakilishi kwenye jimbo.
Nisome vizuri tena uwingi wa watu kuna uongozi kuanzia serikali ya mtaa..pia ofiai ya mbunge iboreshwe kwa kuongezewa watumishi wanaofanya kazi ya kukusanya maoni na kero za wananchi ili ziwasilishwe bungeni kwa ajili ya majadiliano...siyo ujinga inayofanyika hivi sasa, yaani mbunge anakaa miaka 2 hajarudi bungeni lakini kutwa anatoa maoni yake mbungeni bila kutembelea jimboni.