Rasimu ni maoni sio Katiba

Rasimu ni maoni sio Katiba

Unisamehe nitakuwa nauliza.maswali kama nilivyojeleza toka mwanzo. Usjje dhani napingana na wewe laa hasha.
1. Umeseme Waziri Mkuu atakuchukua nafasi ya rais lakini huyu ni mbunge alochaguliwa na jimbo lake na kupitishwa na Bunge. Hii itazaa hoja nyingine kuwa Waziri Mkuu huyu wa Tanganyika atakuwa katika Katiba ya Tanganyika sio Katiba ya Muungano wakati Makamu wa rais ni hoja ya Katiba ya JMT. Unapomuondoa Makamu ya rais inatakiwa Waziri Mkuu pia alokubalika pande zote mbili za Muungano.
2. Utawezsje waondoa Wabunge wa Majimbo 214 ili kuunda Bunge kulingana na mikoa ikiwa leo kuna majimbo yanatakiwa kuongezwa kwa madai ya UKUBWA wake? Hili sidhani kama litaungwa mkono.

Rais wa nchu lazima awe na Mamlakannchi nzima.na nsjo sababu ya kuwepo Wakuu wa Mikoa na Wilaya kama representantive wa dola. Kama haitakuwa hivyo, rais atakosa mamlaka ya mikoa na kuna hatari ya baadhi mikoa kujiamlia mambo yao wenyewe. Waziri Mkuu ni msimamizi wanutekelezaji wa Serikali ambayo haina mwakilishi Mikoani. Serikali inaundwa na rais..
Sorry, hiyo ni muundo wa Serikali ya Tanganyika siyo Zanzibar...kwa Zanzibar Sina cha kupendekeza kwenye katiba make nataka serikali tatu.
Suala la kugawa majimbo yaliyopo ni tamaa za viongozi ndiyo maana napendekeza yarudi kuwa mkoa mmoja mbunge mmoja...tukiruhusu kugawa majimbo...mwisho wa siku Tarafa itakuwa jimbo na kuwa na mwakilishi kwenye jimbo.

Nisome vizuri tena uwingi wa watu kuna uongozi kuanzia serikali ya mtaa..pia ofiai ya mbunge iboreshwe kwa kuongezewa watumishi wanaofanya kazi ya kukusanya maoni na kero za wananchi ili ziwasilishwe bungeni kwa ajili ya majadiliano...siyo ujinga inayofanyika hivi sasa, yaani mbunge anakaa miaka 2 hajarudi bungeni lakini kutwa anatoa maoni yake mbungeni bila kutembelea jimboni.
 
Tuongee kizalendo kabisa, kikwazo kikuu cha Tanzania kutosonga mbele kwa kasi ni rais kutokana na chama cha siasa. Kwa sababu serikali anayounda rais itaitwa "serikali ya chama xxxx" -mwanzo wa anguko la nchi kwa sababu wabunge wanaotokana na chama cha rais (katika hali ya kawaida watakuwa wengi) automatically wanakosa uwezo wa kuisimamia serikali na kubaki watetezi wa serikali ya chama chao; na mbaya zaidi rais anakuwa ndiye mwenyekiti wa chao na ndiye anaamua hatima yao ya kuendelea kuwa wabunge. SUMU KALI.
Rais ambaye hatokani na chama katiba imruhusu kuunda baraza lake la mawaziri apendavyo ila wasitokane na wabunge. Ajichagulie mwenyewe wanataaluma nguli kuwa mawaziri wake.
Hapo wabunge wanaotokana na vyama kazi yao inakuwa kusimamia utendaji wa rais na baraza lake la mawaziri. Hapo credit kwa chama cha siasa itatokana na jinsi wanavyomsimamia rais na baraza lake. Nakuambia, utaliona bunge la ukweli. Vyama vitashindania uspika bungeni. Ikipendeza hata spika awe netral.
Narudia kusema hiki ndicho kikwazo chetu kikuu. Mwenyekiti Mao alisema, tatua kikwazo kikuu, vikwazo vidogovidogo vitatoweka bila shida. Kama kweli tunaipenda TANZANIA hii ndiyo DAWA. Lakini kama tunapenda VYAMA vyetu tubaki hivi tulivyo ila MAENDELEO YA KASI tusahau kabisa, tubaki na MAIGIZO kizazi hadi kizazi.
Chama XXX ni jina tu la Utambulisho tu wa Itikadi. Makksa tuyaofanya sisi Waafrika ni dhana ya kwamba CCM ni chama tawala lazima kipate mpinzani wa kukitoa madarakani. Ukiuliza kwa nini? Wanasema wametawala toka tupate Uhuru lkn hakuna la maana walichokifanya!

Sasa tuna uhakika gani wakija wengine watafanya tofauti? Nini haswa tunataka Chama au vyama vya siasa vifanye na kwa nini tunafanya Uchaguzi? Majibu yake yatakuumiza kichwa.

Tumechukua Demokraiaa ya Vyama vingi kama box la Pandora hayujui tunachagua Chama kwa sababu zipi zaidi ya Unazi, ukabila na Ukanda.

Ndio maana binafsi napendekeza kuundwa upya Vyana vya siasa kwa kushibdanisha IDEA ambazo zina malengo ya kumkomboa Mtanzania tokana na mambo haya matatu - Umaskini, Ujinga na Maradhi. Chama chenye sera bora zaidi ndicho kitachaguliwa na utekelezaji wa ILANI yake ndio pekee itakiweka madarakani.
 
Basi utakuwa umetoka nje kidogo maana tunazungumzia KATIBA MPYA ya JMT. Ikiwezekana kupata serikali 3 ndio Tanganyika nayo itaunda Katiba yake lakini ningependa utueleze faida ya kuwa na Serikali 3!

Pia elewa nimekueleza ongezeko la Wabunge kama ilivyo Zanzibar leo nchi ndogo kabisa kama ile wana Wabunge 100. Tanganyika watakuwa na Wabunge 428 nakuhakikishia hatuwezi kuyapunguza kwa kufuata idadi ya Mikoa ama Wilaya ikiwa wao ndio wagawaji.

Wabunge waliopo wanalalamikia ukubwa wa Majimbo tutawezaje kuyafuta wakato kila Mbunge ni mjumbe wa Halmashauri ya Serikali za Mitaa.

Je Serikali za Mitaa nazo Inapunguzwa? Utaundaje ushirikiano baina ya Mbunge na Serikali za mitaa zilizopo? Rais atakuwa na mamlaka gani kwenye utawala wa RAS?

I nfact, Wanasiasa wanataka kuigawa nchi zaidi ya Kuiunganisha na sidhani kama hili ni jambo jema kwa maslahi mapana ya nchi yetu maskini Je, ni zipi faida za mageuzi haya tofauti na hali iliyopo sasa hivi?
 
Mimi napendekeza raisi asiwe na chama au ajiuzulu chama kabla ya kugombea uraisi awe entreprenua mwenye senti ndefu asiyekuwa na njaa au mtu mwenye uzoefu mpana katika sheria na au waziri ila ajiulizun wanachama ili awe fair kama katiba ya Singapore ya sasa
 
Basi utakuwa umetoka nje kidogo maana tunazungumzia KATIBA MPYA ya JMT. Ikiwezekana kupata serikali 3 ndio Tanganyika nayo itaunda Katiba yake lakini ningependa utueleze faida ya kuwa na Serikali 3!

Pia elewa nimekueleza ongezeko la Wabunge kama ilivyo Zanzibar leo nchi ndogo kabisa kama ile wana Wabunge 100. Tanganyika watakuwa na Wabunge 428 nakuhakikishia hatuwezi kuyapunguza kwa kufuata idadi ya Mikoa ama Wilaya ikiwa wao ndio wagawaji.

Wabunge waliopo wanalalamikia ukubwa wa Majimbo tutawezaje kuyafuta wakato kila Mbunge ni mjumbe wa Halmashauri ya Serikali za Mitaa.

Je Serikali za Mitaa nazo Inapunguzwa? Utaundaje ushirikiano baina ya Mbunge na Serikali za mitaa zilizopo? Rais atakuwa na mamlaka gani kwenye utawala wa RAS?

I nfact, Wanasiasa wanataka kuigawa nchi zaidi ya Kuiunganisha na sidhani kama hili ni jambo jema kwa maslahi mapana ya nchi yetu maskini Je, ni zipi faida za mageuzi haya tofauti na hali iliyopo sasa hivi?
Poa independent commision ya kugawa majimbo ya uchaguzi na mipaka ya mikoa na sii Pinda kwa vile waziri mkuu anatoka Katavi anagawA mkowa wa Rukwa wakati kwa sasa Katavi wanachangia 7 bilioni kodi TRA na mkoa Arusha unachangia bilioni 450 kwa mwaka
 
Chama XXX ni jina tu la Utambulisho tu wa Itikadi. Makksa tuyaofanya sisi Waafrika ni dhana ya kwamba CCM ni chama tawala lazima kipate mpinzani wa kukitoa madarakani. Ukiuliza kwa nini? Wanasema wametawala toka tupate Uhuru lkn hakuna la maana walichokifanya!

Sasa tuna uhakika gani wakija wengine watafanya tofauti? Nini haswa tunataka Chama au vyama vya siasa vifanye na kwa nini tunafanya Uchaguzi? Majibu yake yatakuumiza kichwa.

Tumechukua Demokraiaa ya Vyama vingi kama box la Pandora hayujui tunachagua Chama kwa sababu zipi zaidi ya Unazi, ukabila na Ukanda.

Ndio maana binafsi napendekeza kuundwa upya Vyana vya siasa kwa kushibdanisha IDEA ambazo zina malengo ya kumkomboa Mtanzania tokana na mambo haya matatu - Umaskini, Ujinga na Maradhi. Chama chenye sera bora zaidi ndicho kitachaguliwa na utekelezaji wa ILANI yake ndio pekee itakiweka madarakani.
Mkandara, mimi siamini katika kitu kinachoitwa itikadi ya chama na ilani ya uchaguzi ya chama. Havina msaada wowote kwa taifa. Tunapaswa kuwa na dira ya taifa ambayo wagombea urais (wasiokuwa na chama) watatueleza wataitekeleza namna gani. Narudia, kwenye uchaguzi wa rais kusiwe na habari ya chama hapo. Wagombea wa vyama wawe kwenye ubunge. Hapo vyama na wagombea ubunge watueleze mikakati yao ya namna watakavyomsimamia rais na baraza lake anapotekeleza dira ya taifa.
 
Poa independent commision ya kugawa majimbo ya uchaguzi na mipaka ya mikoa na sii Pinda kwa vile waziri mkuu anatoka Katavi anagawA mkowa wa Rukwa wakati kwa sasa Katavi wanachangia 7 bilioni kodi TRA na mkoa Arusha unachangia bilioni 450 kwa mwaka
Sasa huo Ukabila ila sema unetumua neno Mkoa badala ya Makabila. Kumbuka Katavi ina Wa Arusha vile vile na pengine hiyo Arusha wachangia kodi sii Wananchi wa hapo. Nyuma ya pazia hili kuna UKANDA na nikuhakikishie Ukanda ulikuwepo kabla ya Uhuru.

Na ndio sababu kubwa uandishi wa Katiba ya mwaka 1977 ili kutuunganisha sii Bara na Zanzibar tu bali hata Bara lengo likiwa kuondoa Ukabila na Udini.

Kwa hiyo kama tunaandika Katiba Mpya ina maana hatutaki kurudi kule tulikotoka. Tunatazama mazingira ya leo na kesho na sii Kurudi nyuma. Tanzania ya leo inatakiwa haina mipaka kwa watu wake kama tunavyoitaka Afrika isokuwa na Mipaka.

Mipaka ihusiane tu na mamlaka ya Kimkakati katika ujenzi wa nchi kwa kugawanisha (decentralisation) shughuli za serikali kwa manufaa ya Watu wote
 
Ndio tuyajue basi maana ile rasimu ilikuwa na mapendekezo ya watu wachache sana ukizingatia ripoti ile. Na ndio sababu ilompa ujasiri JK kuipiga vita..
Ilikuwa na mapendekezo ya watu wachache wakina nani ? Na wakati waliotoa maoni ni wananchi wa pande zote mbili.
 
Mkuu sibishani na wewe. Rasimu ya Warioba ninayo na imejadiliwa sana wakati wa Bunge la Katiba. Kuchangia hapa ni mawazo tofauti na yalokuwepo huko. Nisome toka mwanzo wa mada hii upate wewe kunielewa.

Rasimu ya Warioba inapendekeza serikali 3 na ndio kisa cha bunge kuvunjika. Hata mimi sikubaliani nayo! Sasa unataka mpaka niiweke rasimu hapa ndio utaweza kuchangia ?
Tuseme mkuu mkandara kitendo Cha rasimu ya Jaji Warioba kupendekeza serikali 3 ndo kinakupa hoja ya msingi ya kuikata rasimu hiyo ?

Mapendekezo ya serikali 3 ni maoni ya umma wa pande zote mbili sio matakwa ya tume ya Jaji Warioba.
 
Mkandara, mimi siamini katika kitu kinachoitwa itikadi ya chama na ilani ya uchaguzi ya chama. Havina msaada wowote kwa taifa. Tunapaswa kuwa na dira ya taifa ambayo wagombea urais (wasiokuwa na chama) watatueleza wataitekeleza namna gani. Narudia, kwenye uchaguzi wa rais kusiwe na habari ya chama hapo. Wagombea wa vyama wawe kwenye ubunge. Hapo vyama na wagombea ubunge watueleze mikakati yao ya namna watakavyomsimamia rais na baraza lake anapotekeleza dira ya taifa.
Unaposema DIRA YA TAIFA una maana gani? Nijuavyo dira ni kielekezi cha NJIA yawapi mnapotaka kwenda kama vile GPS lakini haielezi mtafikaje!

Itikadi ndio chombo kinatueleza tunakotaka kwenda tutatumia usafiri gani na nahodha atakuwa nani? Saaa ni jukumu lako mwananchi kuamua utasafiri na chomvo gani, unapima risk zake na faida zake kama kweli Itikadi hii inaweza kufuta Umaskini, Ujinga na Maradhi.

Nini maana ya Itikadi? Ni imani kama waumini wa Dini zetu. Dira ni kufika mbinguni au njseme peponi lakini kila dini na kila dhehebu linakuonyesha ibada, njia ya kupata uzina wa milele au sio. Sasa ni jukumu lako kuchagua unaikubali dini gani.

Katiba inakupa wewe Uhuru wa kuamini itikadi yoyote ya Kisiasa lakini dira yetu toka zamani mwisho wa safari hii ni kufuta Umaskini, Ujinga na Maradhi. haya ndio tuloyaona kuwa maendeleo ya WATU sio VITU.

Sasa kama kuna Chama kinaamini katika maendeleo ya VITU, ndio nikasema Upinzani ujengwe kwa nadharia hiyo halafu Wananchi wachague Je, ni maendeleo ya WATU au VITU yataweza kuondoa maadui hao watatu.
 
Tuseme mkuu mkandara kitendo Cha rasimu ya Jaji Warioba kupendekeza serikali 3 ndo kinakupa hoja ya msingi ya kuikata rasimu hiyo ?

Mapendekezo ya serikali 3 ni maoni ya umma wa pande zote mbili sio matakwa ya tume ya Jaji Warioba.
Hayo ni mawazo yangu miye ndio maana nikasema rasimu ni Maoni sio Katiba. Serikali 3 sizikubali mimi kwa sababu nimeishi nchi yenye serikali 3 na ninazijua gharama zake. Na nimeeleza kwa nini siafiki..

Hakuna Ubaya kuwa na Serikali 3 lakini gharama zake ni kubwa sana kwa nchi maskini ambayo inataka kufuta umaskini. Pili, inaongeza ukubwa wa serikali watu wengi hawajui hilo.

Watu wengi wanadhani ukiwa na serikali 3 sijui kuna mambo ga Muungano ya yasokuwa ya Muungano itaongeza ufanisi sio kweli kabisa ila italeta Urasinu zaidi. Mtanganyika kuwekeza Zanzibar itakuwa shida na Mzanzibar vile vile tutataka kujua pato lako linafaidisha upandw gani. Nduo mwanzo tutagawanyika zaidi ya hizi serikali 2.

Warioba mwenyewe alikuwa mawazo ya Wananchi tu lakini hata yeye haikubaliani na serikali 3 isipokuwa Wananchi wametaka hivyo. Ana wajibu wa kuwakilisha maoni ya Wananchi kama alivyopewa.

Unakumbuka hata Vyama vingi vya Siasa ilipigwa chini na maoni ya Wananchi kwa asilimia 80? Je, unadhani ilikuwa sawa kama tungebakia na chama kimoja?
 
Unaposema DIRA YA TAIFA una maana gani? Nijuavyo dira ni kielekezi cha NJIA yawapi mnapotaka kwenda kama vile GPS lakini haielezi mtafikaje!

Itikadi ndio chombo kinatueleza tunakotaka kwenda tutatumia usafiri gani na nahodha atakuwa nani? Saaa ni jukumu lako mwananchi kuamua utasafiri na chomvo gani, unapima risk zake na faida zake kama kweli Itikadi hii inaweza kufuta Umaskini, Ujinga na Maradhi.

Nini maana ya Itikadi? Ni imani kama waumini wa Dini zetu. Dira ni kufika mbinguni au njseme peponi lakini kila dini na kila dhehebu linakuonyesha ibada, njia ya kupata uzina wa milele au sio. Sasa ni jukumu lako kuchagua unaikubali dini gani.

Katiba inakupa wewe Uhuru wa kuamini itikadi yoyote ya Kisiasa lakini dira yetu toka zamani mwisho wa safari hii ni kufuta Umaskini, Ujinga na Maradhi. haya ndio tuloyaona kuwa maendeleo ya WATU sio VITU.

Sasa kama kuna Chama kinaamini katika maendeleo ya VITU, ndio nikasema Upinzani ujengwe kwa nadharia hiyo halafu Wananchi wachague Je, ni maendeleo ya WATU au VITU yataweza kuondoa maadui hao watatu.
Mkuu, para yako ya kwanza ndiyo msingi wa hoja yangu; kwa maana kuwa dira ya taifa inaprescibe "what" and "when". Sasa kila mgombea (asiyetokana na chama) aje na "how", nasi wapigakura tuchague mwenye realistic "how".
Itikadi yakisiasa ni mbwembwe tu. Kuna wanaoshikilia itikadi ya ujamaa lakini vitendo si vya kijamaa. Kwanini nisumbuke na itaikadi? Kwangu dira ya taifa ndiyo kila kitu - permanent national interest.
 
Hayo ni mawazo yangu miye ndio maana nikasema rasimu ni Maoni sio Katiba. Serikali 3 sizikubali mimi kwa sababu nimeishi nchi yenye serikali 3 na ninazijua gharama zake. Na nimeeleza kwa nini siafiki..

Hakuna Ubaya kuwa na Serikali 3 lakini gharama zake ni kubwa sana kwa nchi maskini ambayo inataka kufuta umaskini. Pili, inaongeza ukubwa wa serikali watu wengi hawajui hilo.

Watu wengi wanadhani ukiwa na serikali 3 sijui kuna mambo ga Muungano ya yasokuwa ya Muungano itaongeza ufanisi sio kweli kabisa ila italeta Urasinu zaidi. Mtanganyika kuwekeza Zanzibar itakuwa shida na Mzanzibar vile vile tutataka kujua pato lako linafaidisha upandw gani. Nduo mwanzo tutagawanyika zaidi ya hizi serikali 2.

Warioba mwenyewe alikuwa mawazo ya Wananchi tu lakini hata yeye haikubaliani na serikali 3 isipokuwa Wananchi wametaka hivyo. Ana wajibu wa kuwakilisha maoni ya Wananchi kama alivyopewa.

Unakumbuka hata Vyama vingi vya Siasa ilipigwa chini na maoni ya Wananchi kwa asilimia 80? Je, unadhani ilikuwa sawa kama tungebakia na chama kimoja?
Mkuu mkandara Mimi napo shindwa kukubaliana na wewe ni kitendo Cha kuikata rasimu yote sababu ya muundo wa serikali 3 hapa hautendi haki kwa maoni ya umma.

Kama watu wenye utashi kamili tukipuuza maoni ya umma je,tunapaswa kujiita nchi ya kidemokrasia ?

Katika uthibiti wa matumizi ya umma bado tuna safari ndefu sana maana serikali inafanya matumizi mengi yasiyo ya lazima uku umma ukiwa na hali mbaya sana katika huduma za kijamii sijaona ukitupia umakini katika hili lakini naona unatupia jicho katika uendeshaji wa serikali 3 jinsi utakavyo kuwa na gharama kubwa tu na kupuuza gharama tulizo nazo sasa.

Je,unaweza kusema kwamba kipindi umma unatoa maoni juu ya serikali 3 ulikuwa haujui kwamba kutakuwa na gharama za uendeshaji wake ?

Nchi yetu kabla ya kupata uhuru ilikuwa chini ya mfumo wa vyama vingi kabla ya Nyerere na TANU kufuta mfumo wa vyama vingi na kuleta mfumo wa chama kimoja ambapo mimi binafsi huwa natafsiri hatua hii kama jadi na desturi ya viongozi wengi wa Afrika katika hali na hulka ya tamaa ya madaraka,kupuuziwa kwa maoni ya umma juu ya kurejesha mfumo wa vyama vingi ni tabia ile ile ya viongozi wetu kuona kwamba wao ndio wenya akili kuliko watu wanao waongoza na hii tabia imedumu mpaka sasa maoni ya umma hayaheshimiwe bali ya viongozi kwa utashi wao binafsi.
 
Nimefungua mjadala huu ili sote tupate kujua yapi mapendekezo ya Wana JF katika kudai KATIBA MPYA. Kesho msianze kudai sijui Muungano hatuutaki, tunaitaka Tanganyika, sijui rais ana madaraka makubwa sana! Njooni tujadili sote hapa!

Isije tokea siku ya mchakato ndio mkaanza kuwa nyuma ya mashinikizo ya Ukanda, Vyama, na Wanasiasa.

Hoja yako inaweza toka eneo lolote kati ya hayo tisa tukaanza kuijadili.
Mimi kazi yangu itakuwa kutazama upande wa pili wa sarufi.

Kama tunaitakia mema Tanzania, tujenge nchi ya serikali moja. Muungano wetu umetusitiri na mengi. Kuwa na serikali tatu, kutachangia wajanja kuuvunja muungano kwa malengo yao wenyewe.
Ingawaje, katika muundo tunaweza kufikiria namna ya tanzania bara na Zanzibar zitakavyoweza kuwa na mamlaka zisizo kinzana, wala kuufanya muundo wa serikali kuwa mkubwa na mzigo kwa walipa kodi
 
Mawaziri wanapoteuliwa, pamoja na viongozi wengine wote wa vyeo vya juu vya umma, ikiwemo vyombo vya usalama, uteuzi wao uwe unaidhinishwa na bunge. Katiba iwape uhuru wa kufanya kazi zao bila kuingiliwa kisiasa na mamlaka nyingine
 
Mkuu, para yako ya kwanza ndiyo msingi wa hoja yangu; kwa maana kuwa dira ya taifa inaprescibe "what" and "when". Sasa kila mgombea (asiyetokana na chama) aje na "how", nasi wapigakura tuchague mwenye realistic "how".
Itikadi yakisiasa ni mbwembwe tu. Kuna wanaoshikilia itikadi ya ujamaa lakini vitendo si vya kijamaa. Kwanini nisumbuke na itaikadi? Kwangu dira ya taifa ndiyo kila kitu - permanent national interest.
Tatizo lake watakuwa watu 100 wagombea. Chama kinarahisisha kuwachuja hadi unapata mmoja na kile kinacholetwa kina timu nyuma yake yani watu watakao unda serikali yake.

Wee chukulia hivi, toka 1977 tulidhamilia kufuta Umaskini, Ujinga na Maradhi lakini tumeshindwa wakati serikali ina wataalam na wasomi wenye mweleko mmoja, sasa itawezekanaje aje mtu ambaye hana timu atuambie yeye ataweza kuondoa Umaskini? Wakati hana chombo cha Usafiri?
Okay katudadisi zote tumekubali tukafanya booking tukamchagua yeye kumbe tapeli hapo inakuwaje? Kumbuka kama mgombea anaweza kuwashawishi wachache kama alivyofanya Lowassa 2015 inaweEkana pia yeyote anayejiona ana sifa na vision akai present kwenye chama chake kupunguza utitiri wa wagombea ili sifa na vision yake ifanyiwe vetting huko kabla hajawafikia Wananchi.

Pengine, tungeanza na Ubunge tuone kama italeta mabadiliko. Isipokuwa iwe kama kwa rais ambaye hawezi kuchaguliwa mgombea asiye ishi Tanzania basi kwa udogo wake mbunge pia lazima awe anaishi (mkazi) katika jimbo analogombea maana wananchi watakuwa wanamjua vema kuliko kumsikia.

Ni vigumu sana wagombea wa jimbo moja kutumia fedha kununua Ubunge lazima mshindani wake atajua kwa sababu pale ni kwao wote.
 
Mawaziri wanapoteuliwa, pamoja na viongozi wengine wote wa vyeo vya juu vya umma, ikiwemo vyombo vya usalama, uteuzi wao uwe unaidhinishwa na bunge. Katiba iwape uhuru wa kufanya kazi zao bila kuingiliwa kisiasa na mamlaka nyingine
Mimi hapa nipendekeza kitu kimoja zaidi. Kuundwa kwa Baraza la Wazee ambalo tutaliita Senate. Mteule yeyote wa rais lazima apitishwe na mabaraza haya mawili.

Baraza la Senate dogo ambalo litaundwa na Wazee wa Wilaya zetu zote Walochaguliwa na Wananchi kwa Busara na hekima zao. Wajumbe hawa sii lazima wawe Wanachama wa Chama cha Siasa, lengo ni kupata ridhaa wa watu wanatumia hekima na busara zaidi ya Uchama kulingana na historia ya mteule katika uwajibikaji wake.
 
Hilo Baraza la wazee ambalo umeliita Senate mbona lita ongeza gharama kwa umma hasa kwenye matumizi ya kodi kulipa mishahara, posho nk mbona unataka kumpa mwananchi mzigo wa Kodi na wakati huo huo ukisema uendeshaji wa serikali 3 utakuwa na gharama ?

Yapi yatakuwa manufaa ya Baraza hilo katika taifa ukizingatia tuna Bunge na Baraza la mawaziri ?
 
Mkuu mkandara Mimi napo shindwa kukubaliana na wewe ni kitendo Cha kuikata rasimu yote sababu ya muundo wa serikali 3 hapa hautendi haki kwa maoni ya umma.

Kama watu wenye utashi kamili tukipuuza maoni ya umma je,tunapaswa kujiita nchi ya kidemokrasia ?

Katika uthibiti wa matumizi ya umma bado tuna safari ndefu sana maana serikali inafanya matumizi mengi yasiyo ya lazima uku umma ukiwa na hali mbaya sana katika huduma za kijamii sijaona ukitupia umakini katika hili lakini naona unatupia jicho katika uendeshaji wa serikali 3 jinsi utakavyo kuwa na gharama kubwa tu na kupuuza gharama tulizo nazo sasa.

Je,unaweza kusema kwamba kipindi umma unatoa maoni juu ya serikali 3 ulikuwa haujui kwamba kutakuwa na gharama za uendeshaji wake ?

Nchi yetu kabla ya kupata uhuru ilikuwa chini ya mfumo wa vyama vingi kabla ya Nyerere na TANU kufuta mfumo wa vyama vingi na kuleta mfumo wa chama kimoja ambapo mimi binafsi huwa natafsiri hatua hii kama jadi na desturi ya viongozi wengi wa Afrika katika hali na hulka ya tamaa ya madaraka,kupuuziwa kwa maoni ya umma juu ya kurejesha mfumo wa vyama vingi ni tabia ile ile ya viongozi wetu kuona kwamba wao ndio wenya akili kuliko watu wanao waongoza na hii tabia imedumu mpaka sasa maoni ya umma hayaheshimiwe bali ya viongozi kwa utashi wao binafsi.
Hapo.mkuu umeweka.maneno mdomoni kwangu, aijasema.hivyo isipokuwa najaribu kuwa tofauti na maoni yako ama ya rasimu kwa.kuzingatia wapo watu.mawazo yao hayakukusanywa na wengine yaliachwa. Istoshe kila sarufi una pande mbili. Nahoji na kuweka sababu wa upande usokubaliana..

Nimesemaa - Rasimu ya Katiba ni Maoni sio Katiba yenyewe, mimi nina yangu na wewe changia yako nje ya rasimuama owneekezwa pale unapoona palihitaji mjadala zaidi maana kumbuka mchakato unaanza karibuni kwa kodi yako.

Sasa usije shangaa na matokeo wakati hujapata wasaa kuchangia mawazo yako wewe bali yamechukuliwa ya wateule.
 
Back
Top Bottom