Rasimu ni maoni sio Katiba

Rasimu ni maoni sio Katiba

Hapo.mkuu umeweka.maneno mdomoni kwangu, aijasema.hivyo isipokuwa najaribu kuwa tofauti na maoni yako ama ya rasimu kwa.kuzingatia wapo watu.mawazo yao hayakukusanywa na wengine yaliachwa. Istoshe kila sarufi una pande mbili. Nahoji na kuweka sababu wa upande usokubaliana..

Nimesemaa - Rasimu ya Katiba ni Maoni sio Katiba yenyewe, mimi nina yangu na wewe changia yako nje ya rasimuama owneekezwa pale unapoona palihitaji mjadala zaidi maana kumbuka mchakato unaanza karibuni kwa kodi yako.

Sasa usije shangaa na matokeo wakati hujapata wasaa kuchangia mawazo yako wewe bali yamechukuliwa ya wateule.
Mkuu mkandara kwanza niunge mkono hoja yako kuwa sio wananchi wote walio toa maoni juu ya katiba mpya kupitia tume ya Jaji Warioba.

Lakini sioni haja ya kuzunguka Tanzania nzima kuchukua maoni upya na wakati mchakato tayali usha fanywa tukifanya tena hii itakuwa matumizi mabaya ya rasilimali fedha za umma na muda.

Wewe unadhani maoni yakianza kukusanywa upya kila mwananchi atapata fursa ya kuchagia maoni yake ? Kama jibu ni ndio toa ufafanuzi inawezekanaje wananchi wote kushiriki ?

Nitarudi
 
Hilo Baraza la wazee ambalo umeliita Senate mbona lita ongeza gharama kwa umma hasa kwenye matumizi ya kodi kulipa mishahara, posho nk mbona unataka kumpa mwananchi mzigo wa Kodi na wakati huo huo ukisema uendeshaji wa serikali 3 utakuwa na gharama ?

Kwanini Baraza hilo lisichaguliwe na wananchi badala ya kumpa rais madaraka ya kufanya teuzi katika kila nyanja ?

Yapi yatakuwa manufaa ya Baraza hilo katika taifa ukizingatia tuna Bunge na Baraza la mawaziri ?
Hili baraza la Wazee litaingeza kweli gharama lakini ufanisi wa viongozi utaongezeka, uzembe, usaliti, unafiki utapungua kwa sababu Baraza la Senate lina mamlaka ya kumuita hata rais ajieleze ikitokea katumia vibaya madaraka.

Baraza litakuwa na mamlaka ya kumuita kiiongozi yeyote ajibu tuhuma au mashtaka ambao aidha hayawezi kufikishwa mahakamani.

Lengo la kuwa na Baraza hili ni kuondoa mchezo wa Wateule wa rais kutoka chama kimoja kucheza mchezo mchafu maana hata Bunge likiwa na akidi ya kutosha linaweza kumtetea mhalifu akabakia madarakani.

Kazi ya kutumbua iwe ni kazi ya Baraza hili ili ikiwezekana tutaweza kujua kundi zima la wahusika badala ya kumnasa Bangusilo mmoja. Mengi yamepita yakatupwa uvunguni kwa sababu tunategemea sana maamuzi ya rais au Mahakama.

Watazame Marekani wanavyoendesha baraza lao utajua wazi kwamba Kiongozi yeyote Marekani toka anaogopa kabisa kuitwa na baraza hili.

Vitu kama Kosa la Uzembe, Udikteta, matumizi mabaya ya madaraka, kusababishia serikali hasara hayawezi hukumiwa mahakamani kama sababu mambo haya mengi hutokea sii lazima Ufisadi bali ukosefu wa Uzalendi n ukiukaji miiko na maadili.
 
Kuliko kuchagua hao wazee kutoka kila wilaya kwanini tusiwe na mfumo wa majimbo ?
 
Mkuu mkandara kwanza niunge mkono hoja yako kuwa sio wananchi wote walio toa maoni juu ya katiba mpya kupitia tume ya Jaji Warioba.

Lakini sioni haja ya kuzunguka Tanzania nzima kuchukua maoni upya na wakati mchakato tayali usha fanywa tukifanya tena hii itakuwa matumizi mabaya ya rasilimali fedha za umma na muda.

Wewe unadhani maoni yakianza kukusanywa upya kila mwananchi atapata fursa ya kuchagia maoni yake ? Kama jibu ni ndio toa ufafanuzi inawezekanaje wananchi wote kushiriki ?

Nitarudi
Hakuna mtu alosema wazunguke tena bali wewe mwenyewe kama hukuoata nasi ile basi una unawajibu wa kuchagia mawazo yako juu ya Katiba Mpya.

Na haina maana Rasimu ndio pendwa au hiyo pendekezwa maana huko kote wewe na mimi hatumo. Na isitoshe basi niseme kuwa tunahitaji AZIMIO JIPYA maana huwezi kuandika katiba moya pasipo kuwa na Azimio. Tunataka kujenga nini na Katiba imekuwa kigingi cha mafanikio hayo?

Je, ni Demokrasia! Kama ndio je mapungufu ni yapi? Je, Haiwezekani kufanyiwa marekebisho tu mpaka imetulazimu kuandika mpya?

Ile ya 1977 ilidumu kwa sababu tuliweka Azimio la Arusha na imepitwa na wakati kwa sababu Azimio lile halipo tena. Na hata la Zanzibar lilifanyiwa marekebisho tu kuwavisha viongozi kofia mbili

Mimi na wewe tutafaidikaje na Katiba hii Mpya ikiwa hakuna Azimio la Kitaifa?, niseme wazi, kama hivyo ndivyo basi katiba Mpya haiwezi kuwa muarobaini, haiwezi kuondoa mapungufu yetu ila ya Kisiasa, itakuwa sawa kabisa na ile ya South Afrika, Kenya, Uganda n.k
 
Kuliko kuchagua hao wazee kutoka kila wilaya kwanini tusiwe na mfumo wa majimbo ?
Majimbo ni Utawala ambao unaligawa taifa. baraza la Wazee ni watu wasiozidi 50 ambao watakuwa na kazi ya kusimamia serikali ioaswavyo kama ya mabaraza ya Bunge kwenye nidhamu, mikataba, hesabu za serikali (report ya CAG)n.k. Nia ni kudhibiti miaya ya viongozi kushindwa kulitumikia taifa (Wananchi) badala yake wanakitumikia Chama ama rais.
 
----

1b) kutakuwepo dira ya taifa na Sera ya taifa ya maendeleo kwa muda WA kipindi cha kinacholingana na kipindi cha urais ktk miaka 5 au 10. Na kitengo maalum cha kusimamia dira na Sera ya maendeleo kitakachofanya kazi kizalendo na kupenda maendeleo ya nchi. Kabla ya kupanga kitapokea mapendekezo kutoka kwa wananchi mojakwamoja au kupitia wawakilishi. Wakati WA kapeni mgombea urais na ubunge na udiwani hakutakuwa Sera zao au za vyama bali wataeleza kwa wananchi namna wayakavyotekeleza na kusimamia na kuwezesha utekelezaji WA dira na Sera ya taifa itakavyokuwa ili kupigiwa kura. Hii itaondoa uholela WA rais kupanga na kutenda aonavyo tu au kwa kutumia tu Sera ya chama chake tu isiyoendana maranyingi na dira na Sera ya kitaifa kama ilivyo sasa.

-----

3. Rais hatahusika na uteuzi WA wakuu WA mihimili mingine. Mihimili itajichagulia wakuu wake bila rais kuhusika ili kuwezesha Uhuru WA maamuzi kiweredi sio kama rais apendavyo. Hii imeoneshwa na jaji mmoja aliyelalamika kuwa kuna kiongozi WA serikali alichana hukumu yake ambayo haikumpendeza. Na kuondoa dhana ya mhimili WA serikali kujichimbia zaidi kama magufuri alivyosema.
Naunga mkono 1b na 3.
Kwa kuongezea tu katika 1b, Dira/Sera/Mipango ya Maendeleo kitaifa iwe ya Muda mrefu ihitajikavyo, lakini utekelezaji wake ugawanywe kwa vipindi vya Uraisi.
 
Labda nikuulze hivi. Mambo ya Tanganyika ni yapi hayatekelezwi leo? na Je, kuwepo Serikali 2 kinachopungua hapo ni kipi kama sii jina la Tanganyika maana kama ni utawala wa Mawaziri tunao mpaka manaibu na manispaa.
Kwakuwa mimi pia ninaunga mkono hoja ya Muungano wa Serikali tatu (3). Naomba nijaribu kujibu.
- Si swala la utekelazaji peke yake, lakini pia ni NANI anatekeleza, NANI anasimamia utekelezaji huo.
Mfano. Muungano upo kwenye baadhi ya Mambo tu. Kwa mambo yasiyo ya Muungano ya Tanganyika, inakuaje yatekelezwe/kusimamiwa na Mzanzibari?

Labda nikupe fununu kidogo, tu. Nchi zilogawana majimbo zjna Serikali kubwa sana kwa maana ya Watumishi wake. Mfano, tukiwa na Serikali 3 hiyo Tanganyika italazimika kuwa na Wabunge 428 badala ya 214 ili.kuwakilisha majimbo yao kwenye Bunge la JMT na Bunge la Tanganyika. Tutalazimika kugharamia viongozi wote ngazi ya Tanganyika na ngazi ya Kitaifa.

Kwa nchi maskini kama yetu kesho tutadai Majimbo maana mikoa ya Kanda ya ziwa au kusini watapata hoja kwa sababu 2. Kwaza utajiri wao wa dhahabu au gas! Na pili Kujitawala! Hili neno kujitawala hubeba ubaguzi ulonakshiwa. Je, tuko tayari kupambana na hali hiyo ikitokea?

Kama nilivyosema. Lengo la kuunganisha NCHI hizi mbili ni WATU kama vile wazazi wawili wanapofunga ndoa basi kizazi chao huwa na Ubin mmoja. Tukianza kusema kuna Qatanzania na Wazanzibar, Itakuja Wasukuma na Wazaramo maana unarudisha kuitazama zaidi mipaka badala ya Watu..
- Nafikiri, tunawajibu wa kutengeza mfumo wa uendeshaji wa serikali 3 utakao endana na hali na mahitaji yetu. Hatuwajibiki kunakiri kutoka nchi nyingine. Na hili hatutashindwa.

N.B Tanganyika sio nchi MASIKINI. Ni nchi yenye wananchi wengi masikini - masikini wa mali na akili.
 
Majimbo ni Utawala ambao unaligawa taifa. baraza la Wazee ni watu wasiozidi 50 ambao watakuwa na kazi ya kusimamia serikali ioaswavyo kama ya mabaraza ya Bunge kwenye nidhamu, mikataba, hesabu za serikali (report ya CAG)n.k. Nia ni kudhibiti miaya ya viongozi kushindwa kulitumikia taifa (Wananchi) badala yake wanakitumikia Chama ama rais.
Kuhusu mfumo wa Majimbo kuligawa Taifa, nafikiri itategemea umeundwa vipi.
 
Kuhusu umiliki wa Ardhi. Ningependekeza kuwa;

1 - Mtanganyika (mwenye Wazazi angalau kwa vizazi viwili) aweze kumiliki, na sio kupangishiwa Ardhi na Serikali kwa miaka 33, ambako anawajibika kulipa kodi ya Ardhi.
Yaani, Iwe kwamba, Mtanganyika huyu akisha nunua Ardhi, basi iwe ni mali yake binafsi (siyo ya serikali), mpaka pale atakapoamua kuiuza au kuitelekeza (kwa kufuata vigezo).

2 - Wasio timiza kigezo cha Utanganyika (no. 1) hao ndio wakodishiwe/wapangishiwe ardhi na Serikali.
 
Kuhusu mfumo wa Majimbo kuligawa Taifa, nafikiri itategemea umeundwa vipimoja tu kola.jimbo.lijitegemee

Kuhusu mfumo wa Majimbo kuligawa Taifa, nafikiri itategemea umeundwa vipi.
Nikuulize, Unapotaka kuunda Majimbo nini haswa malengo yake? Tutafadikaje na majimbo hayo na zipi hasara zake!

Kama ikiwa nia ni Majimbo yajitegemee kiuchumi ina maana watumishi watakuwa answerable kwa kiongozi wao. Share ya mapato ya kodi itafanyikaje? Misaada ya maendeleo itafantikaje?

Pia kama lengo lake ni kugawana madaraka, fikiria ikiwa leo Serikali za mitaa zinaongoza kwa ubadhilifu wa fedha za miradi, itakuwaje tukiwa na Majimbo ambayo rais hana mamlaka nayo?

Kama zamani miaka ya 70 tulishindwa Madaraka mikoani ikawa shida mkulima kusafirisha mazao toka mkoa mmoja kwenda mwingine. Tukavunja mfumo ule, tumeleta Serikali za mitaa, nazo tumeshuhudia urasimu mkubwa, wananchi wakilalamikia tozo na ushuru. kwa nini turudie makosa? Kwa nini tusiandike Katiba inayo wajali Wananchi kuondoa makosa ya awali na urasimu huo?

Binafsi yangu naamini serikali ya Majimbo yanaweza tutokea kama Nigeria. Mifano ipo mingi kwa nchi za Kiafrika kugawanyika kutokana na Majimbo. Kuanzia Ethiopia, Sudan, Somalia kote huko majimbo yameandamana na Ukabila. Kenya ni swala la muda tu.

Sisi tumeweza kufuta Ukabila na Udini karika.Umoja huu, kwa nini unataka mfumo ambao unaweza kurudisha hali ya hatari kwa usalama wa raia? Kama ya Zanzibar yanatushinda tunataka serikali 3 ili kila mtu awe na chake tutawezaje Majimbo?
 
Kuhusu umiliki wa Ardhi. Ningependekeza kuwa;

1 - Mtanganyika (mwenye Wazazi angalau kwa vizazi viwili) aweze kumiliki, na sio kupangishiwa Ardhi na Serikali kwa miaka 33, ambako anawajibika kulipa kodi ya Ardhi.
Yaani, Iwe kwamba, Mtanganyika huyu akisha nunua Ardhi, basi iwe ni mali yake binafsi (siyo ya serikali), mpaka pale atakapoamua kuiuza au kuitelekeza (kwa kufuata vigezo).

2 - Wasio timiza kigezo cha Utanganyika (no. 1) hao ndio wakodishiwe/wapangishiwe ardhi na Serikali.
Hili nalo ni swala zito sana maana leo hii tupo mil 60 utamilikishaje ardhi ambayo tuseme kuna watu wana eka mil moja ya shamba wakati mwingine hana hata nusu eka? Je unahitaji ardhi kwa sababu gani? Kama nyumba unaweza kununua ya ghorofani sio lazima iwe ardhi yako!

Kama kilimo huoni hatari ya wataondoshwa wakulima wadogo wadogo katika maeneo yao na kuzaa Wakulima matajiri ambao watauziwa ardhi hizo kutokana na tamaa ya kutokana na Umaskini wa wakulima mfano wa Kariakoo ilivyouzwa kwa matajiri?

Je, wafugaji wenye mifugo utawapa eka ngapi. Transpassing utazizuia vipi mtu akikatiaha shambani kwako? Najaribu kujenga hoja hapa kusikia majibu yako..
 
Kwakuwa mimi pia ninaunga mkono hoja ya Muungano wa Serikali tatu (3). Naomba nijaribu kujibu.
- Si swala la utekelazaji peke yake, lakini pia ni NANI anatekeleza, NANI anasimamia utekelezaji huo.
Mfano. Muungano upo kwenye baadhi ya Mambo tu. Kwa mambo yasiyo ya Muungano ya Tanganyika, inakuaje yatekelezwe/kusimamiwa na Mzanzibari?

- Nafikiri, tunawajibu wa kutengeza mfumo wa uendeshaji wa serikali 3 utakao endana na hali na mahitaji yetu. Hatuwajibiki kunakiri kutoka nchi nyingine. Na hili hatutashindwa.

N.B Tanganyika sio nchi MASIKINI. Ni nchi yenye wananchi wengi masikini - masikini wa mali na akili.
Muungano wa Serikali 3 utawatenganisha WATU wa Tanganyika na Zanzibar. Hilo.nakuhakkkishia hata kabla halijapitishwa.

Kumbuka lengo halisi la Muungano wa nchi zetu ilikuwa Kuunganisha WATU wake. Kama tutaunda Serikali 3 ina maana tumekubali kila nchi ibebe msalaba wake. Hapo ndio utawasikia Watanganyika nao wakidai Wazanzibar warudi kwao! Hawa Wazazibar wanafuata nini, nao kule Wabara rudini makwenu. Trust me itatokea wala sii swala la kupigia ramli..

Wenzetu Ulaya, wameweza kabisa kuondoa Ukabila na Ukanda. Mwananchi mkazi wa NewYork au Texas regardless ya race au uzawa wote ni WAMAREKANI na kujitambulisha kama Wamarekani. (Am American) muulize unatoka wapi atasema USA.

Angalia UK kinachiwakeka pamoja ni nguvu ya dola tu lakini Wana ubaguzi ndani ya nchi zao na kuna under ground movements kudai kujigawa.

Na Sisi itakuwa hivyo hivyo, mimi Mtanganyika, mimi Mzanzibar maana tayari dalili zipo wazi machoni mwetu lakini hatutaki kuamini. Nakuhakikishia jina la Tanzania litapotea kabisa kama Tanganyika.

Nia na dhumuni la Katiba hii iwe kuutujenga katika UTANZANIA tuwe proud na nchi yetu badala ta kuchukia kuwa kuitwa Mtanzania.
 
Hili nalo ni swala zito sana maana leo hii tupo mil 60 utamilikishaje ardhi ambayo tuseme kuna watu wana eka mil moja ya shamba wakati mwingine hana hata nusu eka? Je unahitaji ardhi kwa sababu gani? Kama nyumba unaweza kununua ya ghorofani sio lazima iwe ardhi yako!

Kama kilimo huoni hatari ya utawaondoshwa wakulima wadogo wadogo katika maeneo yao na kuzaa Wakulima matajiri ambao watauziwa ardhi hizo kutokana na jmaskini wa wakulima mfano wa Kariakoo ilivyouzwa
Je, wafugaji wenye mifugo utawapa eka ngapi. Transpassing utazizuia vipi mtu akikatiaha shambani kwako? Najaribu kujenga hoja hapa kusikia majibu yako..
Kuhusu Ardhi utaratibu wa sasa wa kuuza Mamilioni ya Ardhi kwa wazungu/ waarabu kwenye game reserves uangaliwe upya kwani kumuachia RAIS peke yake awe ndio pekee anaamua jinsi na nani amuuzie Ardhi ya Game reserves bila ya ridhaa ya wenye mali/ wananchi ina endeleza rushwa kwa Viongozi!
 
Ndio maana nikapendekeza kuwepo Baraza la Wazee (Senate) kwa sababu hao wengine wote mawaziri ni wateule wa rais Wabunge ni wateule wa rais (kamati kuu ndio huwapitisha kugombea Ubunge) kwa hiyo Wabunge ni wateule wa rais ambaye ndiye kiongozi wa chama. Akileta za kuleta anafutiwa Uanachama na hivyo kupoteza Ubunge.

Baraza la Senate linakuwa kama mhimili wa nne unaojitegemea hauwajibiki kwa chama wala mtu yeyote isipokuwa Wananchi

Hoja ya kuondoa vyama vya Siasa ni nzuri lakini tatizo lake Rais atawezaje kuunda Serikali na Mawaziri ambao pengine hawakubaliani naye ktk vision au hata sera zake?
 
Baraza la Senate linakuwa kama mhimili wa nne unaojitegemea hauwajibiki kwa chama wala mtu yeyote isipokuwa Wananch

Utaratibu gani utakaotumika kuwapata hao Senators bila kuingiliwa na " WANAMTANDAO" meaning utawapataje hao Senators ambao ni so patriotic such that their only allegiance is to the country and not "MSOGA"?
 
Wananchi katika mikoa, wilaya na Majimbo yao wanawajua wazee wao wenye Uzalendo, Hekima na Busara iwe hata Machief au Wazee ambao Wananchi huwafuata kwa ushauri kupata busara zao. Hata kama wana vyama kama kina mzee Warioba, Prof. Shivji na kadhalika.

Uchaguzi wao unakuwa kama inavyo pendekezwa kuchaguliwa Wakuu wa Mikoa na sio wateuliwe wa rais.

Muhimu wanajua hata eais hana mamlaka ya kuwaondoa ama hata kuwakemea wakitaka kumhoji kiongozi yeyote. Katiba imewapa mamlaka hayo juu ya viongozi wote. Hii ni kulinda Miiko na Maadili ya uongozi.

Mimi naamini hata hapa JF kuna watu wanauliza maswali magumu bila kujali itkadi za chama. Kama wapo humu bila shaka hata huko mikoani hawakosekani..
 
Uchaguzi wao unakuwa kama inavyo pendekezwa kuchaguliwa Wakuu wa Mikoa na sio wateuliwe wa rais.

Wakuu wa mikoa watachaguliwa utokana na affiliation yao ya vyama ; je kwanini katika kuchagua hao RC na Senators wasitoke kwa wananchi wanaowapenda lakini hawana affiliation ya political party!! That begs the issue of independent candidates sijui kama kwenye tume yenu mmelifikiria hilo!
 
Nadhani hukunielewa vizuri, Sasa hivi Wakuu wa.Mkoa wanatokanana vyama vya Siasa well, wateule wa rais lkn watu wameoendekeza Wakuu qa Mikoa wachaguliwe na Wananchi. Maoendekezo haya ndio nimeyatolea mfano lkn bado sikubaliani na Wakuu wa Mikoa au Wilaya kutomwakilisha rais katika maeneo hayo.

Kwa sababu ipo miradi ya Serikali kuu na ipo ya Halmashauri.

Ile ya Serikali kuu Mkuu wa Mkoa ndiye mwakilishi wa rais na timu yake katika utekelezaji wa.miradi ya Maendeleo usimamizi wa Usalama.

Serikali za mitaa tuna Meya huyu pengine ndiye tunaweza sema asitokane na chama cha Siasa kwa sababu tayari kuna Madiwani kutoka vyama vya Siasa, kuna Mkurigenzi mteule wa rais na Mbunge kama mjumbe.

Baraza la Senate mimi nalitasama kama kioo na tumaini la Wananchi kwa sababu tumeliwa sana, na nidhamu ya kazi hakuna kabisa. Viongozi wanajiona Waheshimiwa kweli kutwa Waziri Mkuu au rais wanalazimika kulambana nao.

Mama Samia kisha badilisha Wateule kama 200 ambao huletewa majina na timu yake ya washauri lakinu kwa sababu hawafanyiwi evaluation matokeo yake ndio haya. Kwa mtazamo wangu tunahitaji sana Baraza hili kuliko kila kitu kwa sababu ya uzembe, mikataba, urasimu, kuuza ardhi na mbuga, Usimamizi wa mashirika ya Umma hata kama ni Corporates yanatakiwa uwajibikaji wa CEO badala ya kuwa na kiongozi kama Magufuli apambane nao mpaka anaanza kuchafua kila kitu maana fitna kwetu ni mila 😂😂😂
 
Nadhani hukunielewa vizuri, Sasa hivi Wakuu wa.Mkoa wanatokanana vyama vya Siasa well, wateule wa rais lkn watu wameoendekeza Wakuu qa Mikoa wachaguliwe na Wananchi. Maoendekezo haya ndio nimeyatolea mfano lkn bado sikubaliani na Wakuu wa Mikoa au Wilaya kutomwakilisha rais katika maeneo hayo.

Kwa sababu ipo miradi ya Serikali kuu na ipo ya Halmashauri.

Ile ya Serikali kuu Mkuu wa Mkoa ndiye mwakilishi wa rais na timu yake katika utekelezaji wa.miradi ya Maendeleo usimamizi wa Usalama.

Serikali za mitaa tuna Meya huyu pengine ndiye tunaweza sema asitokane na chama cha Siasa kwa sababu tayari kuna Madiwani kutoka vyama vya Siasa, kuna Mkurigenzi mteule wa rais na Mbunge kama mjumbe.

Baraza la Senate mimi nalitasama kama kioo na tumaini la Wananchi kwa sababu tumeliwa sana, na nidhamu ya kazi hakuna kabisa. Viongozi wanajiona Waheshimiwa kweli kutwa Waziri Mkuu au rais wanalazimika kulambana nao.

Mama Samia kisha badilisha Wateule kama 200 ambao huletewa majina na timu yake ya washauri lakinu kwa sababu hawafanyiwi evaluation matokeo yake ndio haya. Kwa mtazamo wangu tunahitaji sana Baraza hili kuliko kila kitu kwa sababu ya uzembe, mikataba, urasimu, kuuza ardhi na mbuga, Usimamizi wa mashirika ya Umma hata kama ni Corporates yanatakiwa uwajibikaji wa CEO badala ya kuwa na kiongozi kama Magufuli apapmbane nao mpaka anaqnza kuchafua kila kitu maana fitna kwetu ni mila 😂😂😂

Miradi ya maendeleo katika mkoa kuwepo sio sababu ya wakuu wa mikoa waliochaguliwa na wananchi wasiisimamie simply because hawakuchaguliwa na Rais!! Aferall usimamizi wa miradi ya maendeleo ni kazi ya watendaji, unfortunately our civil servants who are supposed to be apolitical serving any party in power have been politicized by ccm; kiasi kwamba watendaji hao ni wanachama wa vyama vya siasa! Watendaji wote wa civil service wizarani na mikoani WOTE wawe apolitical.

Kwanini Mkurugenzi awe mteule wa Rais badala ya kuwa part of the civil service; yote hii ilikuwa ni kuhodhi madaraka kwa mtu mmoja and in the process tunazalisha CHAWA ambao hawaleti maendeleo bali wizi!! Miradi ya Serikali kuu na miradi ya Halmashsuri yote inatumia fedha za wananchi sioni sababu kwani usimamizi wake uwe tofauti ; hii yote ni kuongeza gharama za usimamizi na kuongeza nafasi za matumizi mabaya ya fedha!

Baraza la Senate linaweza kua na ufanisi tu pale upatikanaji wa hao Senators utakuwa kwa utashi wa wananchi kwa kuwachagua bila mizengwe ya vyama vya siasa.

Katiba ilenge kupunguza madaraka ya Rais ambae hivi sasa ni omnipotent; moja sapo ni hilo la kuteua Regional na District commissioners!! Msiwe kwenye hiyo kamati kutetea status quo!!! Nchi hii imaeharibiwa sana na current arrangements.
 
Back
Top Bottom