Rasimu ni maoni sio Katiba

Rasimu ni maoni sio Katiba

Ahsante Mkandala hebu fikiria mkoa wa Arusha ulikussanya kodi TRA bilioni 450 bilioni na bila kujumuisha utalii na 2022 na Zanzibar bilioni 250 yet Zanzibar wana wabumge 80 bungeni NA MKOA WA arusha una wabunge 10 !! Dodoma ni mtu gani wa Arusha atakubali hali hii? KAMA WANA CHA KUCHANGIA MUUNGANO HUU BASI NI WAJIBU SII KUGAWIWA TU WEMGI WA BARA HAWATAKI HALI HII
Lakini hii imekula kwao Zanzibar sio Arusha kwa sababu Serikali ya Zanzibar ina wabunge 51 Bunge la Jamhuri na wengine 51 Baraza la Wawakilishi. Bado mawaziri na Manaibu.

Kwa kutumia akili ndogo, utaona Arusha yenye mapato makubwa inagharimia Wabunge 10 wakati Zanzibar nchi ndogo kabisa ina wabunge 100 pengine kila Mbunge kwa watu chini ya laki moja!

Kwa nini unaitaka Bara nayo iingie katika shimo hilo?
 
Rasimu ya Warioba ipo, wewe kama mwananchi una mawqzo gani tofauti katika mapwndekezo ya sura ibara zike. Kumbuka sisi wote tuna mitazamo tofauti na hatukubaliani kwa mengi na ndio maana rasimu ile ilisukumwa uvunguni. Je, leo hii tutawezaje kupata suluhu katika Mambo yale yale yalokwama mwanzoni pasipo hata kuwafikia Wananchi.
Wananchi tuliotoa maoni kikundi Cha CCM kikakataa.

Halipo Cha kupunguza labda maboresho tu na Kutoa Elimu Kwa ambao hawakushiriki.

CCM Haina jatimiliki ya nchi hii, CCM ni sawa tu na chama Cha Rungwe tofauti ni idadi kidogo ya Wanachama.

Hatuanzi UPYA, tunataka Rasimu iwekwe mezani ndo tuanzie hapo.

Bring back our WARIOBA 💪💪💪
 
Kwa mara ya kwanza kabisa nitashiriki katika kongamano la KATIBA MPYA hapa kwa dhumuni maalum lenye kutoa fursa ya mawazo mbadala nje ya rasimu ama ile ilopendekezwa ambayo muda sii mrefu mchakato wake utaanza.

Ni matumaini yangu kuwa sii Wananchi wote walopata fursa ya kuchangia mawazo ama maoni yao katika dai la Katiba Mpya. Aidha wapo pia ambao maoni yao hayakupewa umuhimu kwa sababu hayakupata kuungwa mkono na watu wengi japo yalikuwa na umuhimu mkubwa wa kuzingatiwa na ndio ikawa sababu kubwa ya kuahirishwa upatikanaji wa Katiba Mpya.

Katiba ni Sheria mama, haihitaji matakwa ya Vyama vya siasa, Utashi wa Viongozi ama matamanio ya Wananchi isipokuwa huzingatia HAKI, UHURU, FURSA, MIIKO na MAADILI ili kulinda UTU wa Mtanzania kwa Maslahi mapana ya Taifa letu.

Binafsi, nitaorodhesha baadhi ya sehemu ambazo naziona zina utata lakini muhimu sana na zinahitajika kuangaliwa kwa makini sana ili tupate suluhisho la Katiba yenye kukidhi Mahitaji ya Jamhuri.

Maeneo hayo ni kama ifuatavyo:-

1. MUUNGANO
2. MUUNDO WA SERIKALI
3. MADARAKA YA RAIS
4. UKOMO WA VIONGOZI
5. VYOMBO VYA USALAMA
6. DEMOKRASIA
7. MIIKO NA MAADILI
8. UHURU NA HAKI ZA WANANCHI
9. MASLAHI YA TAIFA

Najaribu kukusanya mawazo yetu nikiwa na lengo la kutazama ni jinsi gani hata sisi tunaweza kufikia muafaka katika maono yetu kwa kuzingatia Utu na Maslahi mapana ya Taifa. Nitajikita zaidi upande wa pili kwa hiyo jiandaeni malumbano - HOJA hujibiwa kwa HOJA..

Karibuni - Tuanze na hoja ya kwanza.
Swali lako lingekuwa rahisi sana kujibiwa kama tungekuwa enzi za Mwalimu Nyerere na Sheikh Abedi Karume: tungesoma Hati ya Muungano inayotaka Serkali 2 kama ilivyo.

Thank God sasa tuna Vyama vingi: CCM wanataka Serkali 2, Waarabu na CHADEMA wanataka Serkali 3 ili Waarabu wachukue Zanzibar na huku tuwe na serkali ya Majimbo yaani kila Kabila na Rais wake. Hawa wote ni Watanzania wana haki ya kutoa maoni yao.

Kwa kwa vile TAYARI tuna Katiba, cha kufanya ni kila Chama chenye usajili kiwe huru kutoa Ilani yake tusubiri Uchaguzi 2025. I assume CCM wataahidi Serkali 2 huku CHADEMA na CUF wakiahidi Serkali 3.

Pamoja na uhuru huo, tuzingatie masharti makuu: (1) UWEPO WA MUUNGANO (2) UDINI NA UKABILA, WALA UPENDE MMOJA TU WA MUUNGANO marufuku.

Haya mawili kama yakizingatiwa kwa nguvu zote za Serkali iliyopo, tukaeni mkao wa kula tusubiri 2025.

Tumesikia wakisema bila Katiba Mpya 2025, wao hawatoshiriki uchaguzi. Hiyo nayo ni hiari yao Kikatiba. Iheshimiwe. Wengine hawakuishia hapo, wamesema bila Katiba mpya watafanya fujo ili Uchaguzi usiwepo kabisa. Hiyo haki ya fujo hawana Kikatiba.

Kwa hiyo watakafanya fujo wajiandae kufa au kupona wakipambana na Polisi au TPDF ikibidi: vyombo hivi vinalipiwa kwa gharama kubwa, viliwekwa kwa kazi hiyo kila vinapohitajika.
 
Maboresho yapi unayoyataka wewe Mwananchi?
 
Mimi nitatoa mapendekezo yangu Rasimu alosimamia Judge WARIOBA itaporudishwa mezani sababu nilishiriki Kutoa maoni mbele ya Tume na Kodi yangu ilitumika.

Siezi toa maoni UPYA wakati nilotoa hayajafanyiwa KAZI. Huo ni ufujaji pesa za Umma.

Bring back our WARIOBA 💪💪💪💪
 
Nisingependa kusubiri hadi 2025 bila kusikia wewe Maananchi unataka mbadiliko gani ndani ya Katiba. Yaweke, tuyajadili ikiwa ni pamoja na maswala 9 muhimu niloyaweka hapo.

Tukitegemea vyama vya Siasa, utalishwa matango pori matokeo yake ni kuharisha siku nzima! 😂😂😂
 
Ndio tuyajue basi maana ile rasimu ilikuwa na mapendekezo ya watu wachache sana ukizingatia ripoti ile. Na ndio sababu ilompa ujasiri JK kuipiga vita..
 
Nenda jukwaa la Katiba, download RASIMU ya kwanza ya Warioba,ilete hapa Kwa Uzi huu, usome Kwanza kabla ya kuanza Kutoa maoni Yako isijekuwa unarudia.
 
Nisingependa kusubiri hadi 2025 bila kusikia wewe Maananchi unataka mbadiliko gani ndani ya Katiba. Yaweke, tuyajadili ikiwa ni pamoja na maswala 9 muhimu niloyaweka hapo.

Tukitegemea vyama vya Siasa, utalishwa matango pori matokeo yake ni kuharisha siku nzima! 😂😂😂
Rasimu ya Warioba haikuwa ya wanasiasa, ni matakwa ya wananchi wote, wanasiasa wakiwemo.

Bring back our Rasimu ya WARIOBA 💪💪💪💪
 
Rasimu ya Warioba haikuwa ya wanasiasa, ni matakwa ya wananchi wote, wanasiasa wakiwemo.

Bring back our WARIOBA 💪💪💪💪
Basi nadhani hapa hapakufai maana lengo ni kutaka Wananchi ambao hawakushiriki ama mawazo yao hayakuchukuliwa ndio tujadili rasimu ile na pendekezwa.

Mimi sikushirikishwa na wala simfahamu ndugu, jamaa au rafiki aloshiriki. Na niseme hivi karibu sehemu zote nimekutana na mapingamizi na mitazamo tofauti inayo kinzana na rasimu. Sehemu hizi zimejaribu kuziorodhesha.

Mathlan, mimi binafsi ningependa kuona vyama vya Siasa vilivyopo vyote vifutwe, tuanzishe vyama vipya VIKUU vitatu (3) tu. Chama kimoja kiwe Cha Kihafidhina kinacholenga kulinda na kusimamia UJAMAA na KUJITEGEMEA (Azimio la Arusha) kama lilivyo asisiwa na wazee wetu halafu Chama pinzani kiwe Liberali kinachotaka mabadiliko katika falsafa ya Kijamaa. Chama cha tatu kichukue baadhi ya Uhafidhina na baadhi Uliberali. Hapo watangana kwa sera na Wananchi watajua chama hiki kinasimamia mambo yapi kwa ajili ya nini na sii Nani ni nani..

Kuwa na vyama vya Siasa 20 ambavyo havina tofauti ya Kiitikadi ndio chimbuko la matatizo yote ya kupingana WATU badala ya SERA na tunapoteza hela nyingi sana kwenye ruzuku za vyama vya Siasa ambavyo havileti mabadiliko ya fikra..
 
Basi nadhani hapa.hakakufai maana lengo ni kutaka Wananchi ambao hawakushiriki ama mawazo yao hayakuchukuliwa ndio tujadili rasimu ile na pendekezwa.

Mimi sikushirikishwa na wala simfahamu ndugu jamaa au rafiki aloshiriki. Na niseme hivi karibu sehemu zote nimekutana na.mapungamizi na mitazamo tofauti inakinzana na rasimu. Sehemu hizi zimejaribu zizuorodhesha.

Mathlan, mimi binafsi ningeoenda vYama vya Siasa viluvyopo vyote vifutwe, tuanzishe vyama vipya vitatu (3) tu. Chama kimoja kiwe Cha Kihafidhina kinacholenga kulinda na kusimamia UJAMAA na Azimio la Arusha kama lilivyoa asisiwa na Chama punzani kiwe Leberali kinachitaka mabadiliko katika faslafa ya Kijamaa. Chama cha tatu kichukue baadhi ya Uhafidhina na baadhi Uliberali.

Kuwa na vyama vya Siasa 20 ambavyo havina tofauti ya Kiitikadi ndio chimbuko la matatizo yote ya kupingana WATU badala ya SERA na tunapoteza hela nyingi sana kwenye ruzuku za vyama vya Siasa ambavyo ni havileti mabadiliko ya fikra..
Hakuna haja ya kubishana,

Nimekwambia kabla ya mjadala tupate kwanza pa kuanzia kama Reference.

Huwezi kuwa na akili kuliko waliokuzaa, ilete Rasimu ya Warioba kabla haijapelekwa bungeni mjadala uanzie hapo.

Hatutakubali kamwe kuanza UPYA wakati tuna pa kuanzia.

Bring back our Rasimu ya WARIOBA 💪💪💪💪
 
Hakuna haja ya kubishana,

Nimekwambia kabla ya mjadala tupate kwanza pa kuanzia kama Reference.

Huwezi kuwa na akili kuliko waliokuzaa, ilete Rasimu ya Warioba kabla haijapelekwa bungeni mjadala uanzie hapo.

Hatutakubali kamwe kuanza UPYA wakati tuna pa kuanzia.

Bring back our Rasimu ya WARIOBA 💪💪💪💪
Mkuu sibishani na wewe. Rasimu ya Warioba ninayo na imejadiliwa sana wakati wa Bunge la Katiba. Kuchangia hapa ni mawazo tofauti na yalokuwepo huko. Nisome toka mwanzo wa mada hii upate wewe kunielewa.

Rasimu ya Warioba inapendekeza serikali 3 na ndio kisa cha bunge kuvunjika. Hata mimi sikubaliani nayo! Sasa unataka mpaka niiweke rasimu hapa ndio utaweza kuchangia ?
 
Kwa mara ya kwanza kabisa nitashiriki katika kongamano la KATIBA MPYA hapa kwa dhumuni maalum lenye kutoa fursa ya mawazo mbadala nje ya rasimu ama ile ilopendekezwa ambayo muda sii mrefu mchakato wake utaanza.

Ni matumaini yangu kuwa sii Wananchi wote walopata fursa ya kuchangia mawazo ama maoni yao katika dai la Katiba Mpya. Aidha wapo pia ambao maoni yao hayakupewa umuhimu kwa sababu hayakupata kuungwa mkono na watu wengi japo yalikuwa na umuhimu mkubwa wa kuzingatiwa na ndio ikawa sababu kubwa ya kuahirishwa upatikanaji wa Katiba Mpya.

Katiba ni Sheria mama, haihitaji matakwa ya Vyama vya siasa, Utashi wa Viongozi ama matamanio ya Wananchi isipokuwa huzingatia HAKI, UHURU, FURSA, MIIKO na MAADILI ili kulinda UTU wa Mtanzania kwa Maslahi mapana ya Taifa letu.

Binafsi, nitaorodhesha baadhi ya sehemu ambazo naziona zina utata lakini muhimu sana na zinahitajika kuangaliwa kwa makini sana ili tupate suluhisho la Katiba yenye kukidhi Mahitaji ya Jamhuri.

Maeneo hayo ni kama ifuatavyo:-

1. MUUNGANO
2. MUUNDO WA SERIKALI
3. MADARAKA YA RAIS
4. UKOMO WA VIONGOZI
5. VYOMBO VYA USALAMA
6. DEMOKRASIA
7. MIIKO NA MAADILI
8. UHURU NA HAKI ZA WANANCHI
9. MASLAHI YA TAIFA

Najaribu kukusanya mawazo yetu nikiwa na lengo la kutazama ni jinsi gani hata sisi tunaweza kufikia muafaka katika maono yetu kwa kuzingatia Utu na Maslahi mapana ya Taifa. Nitajikita zaidi upande wa pili kwa hiyo jiandaeni malumbano - HOJA hujibiwa kwa HOJA..

Karibuni - Tuanze na hoja ya kwanza.
Bado nasisitiza kuwa sheria itungwe ili wote watakaoshiriki mchakato hadi kupitisha wasigombee nafasi yeyote kwa muda wa miaka 20 ili kuepuka kuingiza maslahi binafsi katika katiba mpya.
 
Maoni yangu.
Muungano:
Tuwe na muundo wa serikali 3, Zanzibar, Tanganyika na Muungano.
Kwenye serikali ya muungano tuungane kwenye nyanja tatu 1. Biashara. 2. Ulinzi 3. Elimu
Muundo wa Serikali.
Serikali ya Tanganyika. Serikali ya Tanganyika iwe na Rais anaechanguliwa na wanannchi kupitia mgombea huru au mgombea aliepitishwa na Chama cha siasa. Lakini pasiwepo na makamu wa Rais.
Waziri mkuu atatokana na kura ya wananchi kama mbunge ila atachaguliwa Bungeni kama spika anavyochaguliwa siyo Jina kupendekezwa na Rais.
Mikoa itakuwa chini ya RAS, hivyo RC watafutika, Wilaya zitakuwa chini ya DAS hivyo DC watafutika.
Wabunge, kila mkoa itawakilishwa na mbunge mmoja...ofisi ya mbunge itaboreshwa na kuwa watumishi wanaoshughulika na kazi zifutazo. 1. Utafiti na ukusanyaji wa maoni pamoja na kero za wananchi katika mkoa husika ili ziweze kuwasilishwa bungeni na mbunge wao. 2. Wanaohusika na kutoa taarifa kwa wananchi kuhusiana na kero na maoni waliyotoa ili ziwasilishwe bungeni.
Baraza la Mawaziri.
Waziri awe mtu asiye mbunge na nafasi hizo ziwe wazi kwa ajili ya wananchi wenye sifa kuziomba na kupigiwa kura mbungeni baada ya usahili kufanyika.

Mwakilishi kwenye serikali ya muungano.
Waziri mkuu atakuwa kiongozi wa jopo la wawakili wa Tanganyika kwenye serikali ya Muungano..wawakilishi wasizidi viongozi 10.
 
Mawazo mazuri ebu niruhusu kuuliza maswali kidogo.
1. Kama hatakuwepo Makamu wa rais, ikitokea rais kufariki nani atachukua madaraka hayo (kukaimu) ama ndio Uchaguzi mpya ufanyike?

2. Je, Watanganyika wapo tayari kugharamia Wabunge 428 na Mawaziri 21 na manaibu 21 (42) wapya ambao sii Wabunge? Hapapekee kutakuwa na ongezeko la Viongozi wengine 235 ambao hawapo sasa hivi. Hizo gharama zitalipwaje.

3. Kuondosha Wakuu wa Mikoa ili RAS awe kiongozi huoni kama mikoa itajiendesha bila ridhaa ya rais? Rais hatapoteza mamlaka yake mikoani?
4. Je, mkoa wakitokea kutaka kujitenga na Jamhuri kwa mapendekezo ya RAS na wananchi wake, hoja hii itashughulikiwa na nani?

Kumbuka pia kuwepo kwa mambo ya Muungano na yasokuwa ya Muungano haipunguzi Viongozi bali inaongeza.

Nimeuliza kwa.udadisi nipate kujua mfumo mzima utatusaidiaje badala ya kuleta migogoro.. (faida vs hasara)
 
1. Kutokuwepo makamu wa Rais, Waziri mkuu atachukuwa usukani kama Rais kwa kipindi cha mpito.
2. Wabunge watapungua kuendana na idadi ya mkoa hivyo gharama ya kuendesha bunge itakuwa kidogo sana. Pia hii itasababisha tupeleke wabunge wachache wenye kujadili jambo kwa upana wake na kufikia muafaka...siyo Yale yanayoendelea bilingeni sasa miaka mitatu mbunge hajachangia chochote bungeni.
3 na 4. RC ni mtu mmoja anateuliwa na kutenguliwa kila wakati pia RAS inaweza kuwekwa utaratibu mpya ya kuwajibika moja kwa moja ofisi ya waziri mkuu.
 
Watu wanaogombea urais wasiwe wanachama WA chama cha siasa. Kwa kuwa
Tuongee kizalendo kabisa, kikwazo kikuu cha Tanzania kutosonga mbele kwa kasi ni rais kutokana na chama cha siasa. Kwa sababu serikali anayounda rais itaitwa "serikali ya chama xxxx" -mwanzo wa anguko la nchi kwa sababu wabunge wanaotokana na chama cha rais (katika hali ya kawaida watakuwa wengi) automatically wanakosa uwezo wa kuisimamia serikali na kubaki watetezi wa serikali ya chama chao; na mbaya zaidi rais anakuwa ndiye mwenyekiti wa chao na ndiye anaamua hatima yao ya kuendelea kuwa wabunge. SUMU KALI.
Rais ambaye hatokani na chama katiba imruhusu kuunda baraza lake la mawaziri apendavyo ila wasitokane na wabunge. Ajichagulie mwenyewe wanataaluma nguli kuwa mawaziri wake.
Hapo wabunge wanaotokana na vyama kazi yao inakuwa kusimamia utendaji wa rais na baraza lake la mawaziri. Hapo credit kwa chama cha siasa itatokana na jinsi wanavyomsimamia rais na baraza lake. Nakuambia, utaliona bunge la ukweli. Vyama vitashindania uspika bungeni. Ikipendeza hata spika awe netral.
Narudia kusema hiki ndicho kikwazo chetu kikuu. Mwenyekiti Mao alisema, tatua kikwazo kikuu, vikwazo vidogovidogo vitatoweka bila shida. Kama kweli tunaipenda TANZANIA hii ndiyo DAWA. Lakini kama tunapenda VYAMA vyetu tubaki hivi tulivyo ila MAENDELEO YA KASI tusahau kabisa, tubaki na MAIGIZO kizazi hadi kizazi.
 
Ili hayo yawezekane, rais aondolewe mamlaka ya kuvunja bunge.
 
1. Kutokuwepo makamu wa Rais, Waziri mkuu atachukuwa usukani kama Rais kwa kipindi cha mpito.
2. Wabunge watapungua kuendana na idadi ya mkoa hivyo gharama ya kuendesha bunge itakuwa kidogo sana. Pia hii itasababisha tupeleke wabunge wachache wenye kujadili jambo kwa upana wake na kufikia muafaka...siyo Yale yanayoendelea bilingeni sasa miaka mitatu mbunge hajachangia chochote bungeni.
3 na 4. RC ni mtu mmoja anateuliwa na kutenguliwa kila wakati pia RAS inaweza kuwekwa utaratibu mpya ya kuwajibika moja kwa moja ofisi ya waziri mkuu.
Unisamehe nitakuwa nauliza maswali kama nilivyojieleza toka mwanzo. Usije dhani napingana na wewe laa hasha.

1. Umesema Waziri Mkuu atakuchukua nafasi ya rais lakini huyu ni mbunge alochaguliwa na jimbo lake na kupitishwa na Bunge hakuchaguliwa na Wananchi wote kama Makamu wa rais.

Hoja nyingine, Waziri Mkuu huyu wa Tanganyika atakuwa katika Katiba ya Tanganyika sio Katiba ya Muungano wakati Makamu wa rais ni hoja ya Katiba ya JMT.

Unapomuondoa Makamu ya rais inatakiwa Waziri Mkuu pia alokubalika pande zote mbili za Muungano.

2. Utawezsje waondoa Wabunge wa Majimbo 214 ili kuunda Bunge kulingana na mikoa ikiwa leo kuna majimbo yanatakiwa kuongezwa kwa madai ya UKUBWA wake? Hili sidhani kama litaungwa mkono.

Rais wa nchi lazima awe na Mamlaka nchi nzima na ndio sababu ya kuwepo Wakuu wa Mikoa na Wilaya kama representantive wa dola.

Kama haitakuwa hivyo, rais atakosa mamlaka mikoani na kuna hatari ya baadhi mikoa kujiamlia mambo yao wenyewe. Waziri Mkuu ni msimamizi wa utekelezaji wa Serikali ambayo haina mwakilishi Mikoani itawezekanaje.
NB:- Serikali inaundwa na rais..
 
Mkandara,

Upo sahihi kwa aina hii ya mjadala,Kimsingi tunaouhitaji wa katiba Mpya kulingana na nyakati hizi, Tukirejea kwenye hoja hapo juu ni dhahiri swala la muundo wa Muungano wetu limekuwa msingi mkuu wa aina ya katiba tunayoitamani.

Yaliyotokea katika Bunge Maalumu La Katiba ndio yanayotia makandokando ya upatikanaji was Katiba Mpya na Sioni namna zaidi kwanza Wananchi kwa namna ya kipekee na kwa katiba iliyopo kwanza kuamua aina ya Muungano wanoutaka.
 
Back
Top Bottom