Rasimu ya II ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Rasimu ya II ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Serikali 2 imeshidikana miaka mingapi sasa, kwanini watanzania tunaogopa mabadiliko ? Mfumo wa shirikisho wa serikali 3 ndio mwafaka.
 
Hali ni mbaya, serikali mbili ni tatizo, serikali tatu ni tishio. Nadhani ni wakati wa kukiri kuwa utaratibu ulikosewa kwa kutokutarajia haya yanayojiri. Tulipaswa tuanze na referandum juu ya muundo wa Muungano tukimaliza ndio tuongelee Katiba. Wanao hofia mabadiliko wana hoja ya msingi kwani wanajua kuibadili katiba ya Zanzibar ni muujiza na Muungano umekaa tenge ila tenge hii ni imara kuliko kubomoa na kujenga upya. Tenge hii ina nondo iliyopenya ndani ya Zanzibar na kuishikilia haiwezi kuchomoka (si jambo ambalo Zanzibar wangependa kulisikia). Kuweka serikali tatu nikirejea hoja ya Mh Membe ambayo kimsingi kwangu ndio inayobeba taswira halisi ya mambo, kunaichomoa nondo hii na uwezekano wa Zanzibar tunayoishikilia kuponyoka ni mkubwa. Hali ya usalama upande wa bahari na visiwa vyake si shwari hata kidogo na tukikosa nguvu ya kuingilia maswala ya Zanzibar basi tutakuwa na eneo tete bila shaka. Aidha Serikali tatu kwa sura nzuri inayoonekana ambayo inanishawishi hata mimi, inategemea nia ya dhati ya kuibadili katiba ya Zanzibar kwanza, ili kutambua vigezo muhimu vya muungano ambavyo walivitengua 2010, kwani Tanzania bara walishapoteza uwezo huo na wanajua hili. Waliobadili katiba ya Zanzibar ni hawa waliiko sasa ambao wameficha nia yao ya dhati na misimamo kwani wanajua Tanzania bara wamenasa.
Ni wakati wa kusimamisha mjadala huu maana tumesikia hoja zote tayari na tuweke swala hili tayari kwa kura maoni. Serikali1, 2 au 3. Hakuna ubishi swala hili limebeba muundo wa Katiba. Tuendelee kujadili Sura nyingine tukizingatia msingi huu mkuu wa Muundo wa Muungano.
 
Kinacho takiw hapo ni malidhiano ya pand mbil na kuvutan mar 3 mar 2 ss hapo wananch hawajui lip ambalo umeamua,watoe hoja za msing ktk katba hii mpya ya tanzania
 
Mara 2, Mara 3.. Mbona Hatusemi 1? au ndo 2metekwa kimawazo na ccm na ukawa.! hebu 2piganie serikali 1, hii ndo mwarobain Wa muungano.
 
Jamani mbona tunafika mbali naomba tukumbuke waasisi wa muungano walifikilia nini kuungana ile april 1964? baada ya hapo tukigundua chanzo tukae mezani tujadili nijinsi gani tutaendesha serikali yetu na budget ya taifa letu twawezaje kuibalance ilikukuza uchumi wa taifa letu la TANZANIA achilia mbali UZANZIBAR na UTANGANYIKA.
 
Kwanza tujue walioanzisha serikari moja lengo ilikuwa nini
naninyi munaoanzisha serikari tatu lengo
ni nini
 
Kwanza tujue walioanzisha serikari moja lengo ilikuwa nini
naninyi munaoanzisha serikari tatu lengo
ni nini



Ipo wazi tu kwamba Nyerere kama alivyo Karume walijua umhimu wa kuwa na nchi moja serikali moja. Lakini tujiulize kwamba ni kwa nini Nyerere alikataa wakati Karume alikubali ?

Tukifikiria kwa undani tutagundua kwamba Nyerere akigundua kuwa patakua na mgogoro wa madaraka kati yake na Karume; Je,Karume angekubali moja kwa moja kumwachia Nyerere urais wa hiyo serikali moja wakati Nyerere alitamani kuwa rais wa maisha wa ?Je,Nyerere angekubali kumwachia Karume Urais wakati alijua fika kwamba elimu yake ilika ndogo?

Na alipofikiria kuhusu serikali tatu aliona pia patakua na mgogori wa kimadaraka;
Je,awe rais wa Tanganyika ?Nani atakua bosi wake,yaani rais wa muungano,na je, atazipeleka wapi hizo nchi mbili ?
Je,aachie Tanganyika yake aliyoipigania mpaka ikapata Uhuru ili awe rais wa Muungano ? na je Muungano ukivunjika atakua mgeni wa nani wakati hana ardhi?
Aliwaza,Nani atawachagua marais wa Tanganyika na wa Zanzibar wakati hakuamini katika Demokrasia ya vyama vingi kwa wakati huo na uchanga wa nchi zote mbili?

Nyerere aliona serikali mbili zinafaa kwasababu alijua kwamba atatawala Tanganyika na Muungano . Ndio maana alijivika koti la Muungano. Pia alijua kwamba Muungano ukivunjika ataendelea kuwa rais wa Tanganyika.Ni ukweli kwamba muungano wa serikali mbili haukuzingatia suala la uchumi kabisa. Ndio maana Zanzibar wanachangia pato la Muungano wanapoamua tu na wala sio suala la kisheria,na kwamba wanaposhindwa kulipa inakuaje?
Mfano tu Zanzibar wana bili kubwa sana ya umeme na hawana mpango wa kulipa.Hakuna mtu yeyote anayeona kwamba huo ni mzigo kwa watu wa bara.
SMZ hailipi kwa sababu ya kutokua na mchanganuo kamili wa kiuchumi kwa sababu watendaji wamejikita zaidi kutafuta vyanzo vya fedha Tanzania Bara.Mafisadi wamejikita bara.

Tujiulize kama kweli Nyerere aliwaza juu ya Zanzibar kumezwa ni kwa nini Rais wa Zanzibar asiwe ndiye Rais wa Jamhuri ya Muugano?

Utagundua kua mfumo wa serikali mbili ni wa kiutawala zaidi sio kiuchumi kwa sababu Zanzibar isipolipa chochote hakuna hatua inayochukuliwa ,na imefanywa kama mwanamke kwenye nyumba. MUUNGANO WA SASA NI WA WATU KUPEANA MADARAKA TU,NDIO MAANA HAWAKO TAYARI KUSIKILIZA MAONI YA WANANCHI.
SUBIRINI KIFUNGU CHA KUPUNGUZA MADARAKA YA RAIS MTAJUA WATAWALA WANATAKA NINI.
 
Ndugu wana JF,
Hii Rasimu ya 2 imekaa poa sana tena sana tu.
Lakini kwa vile inapingana na maslahi na matakwa ya MAFISADI wa CCM wanaotaka kuendelea kutawala nchi hii milele ndiyo maana wanaipinga!!!

Kama isingelikuwa UBABE wa hiki chama Twawala tayari sasa hivi Watanzania tungelikuwa tunashangilia na kusherehekea KATIBA MPYA ya JMT. Watanganyika wangelikuwa nao wanasubiri Katiba yao ya Tanganyika na tungefanya Uchaguzi wa SM na Uchaguzi Mkuu mwaka 2015 chini ya Katiba mpya!

Kila Mtanzania anajua kabisa kuwa Rasimu ya 2 ya Katiba mpya ni MWIBA kwa CCM. Hawa MAFISADI wanajua kabisa kwamba ikipita na kuwa Katiba CCM watakuwa hawana chao. Fikiria tu kuhusu Ukomo wa Ubunge, Mawaziri kutotokana na Wabunge,Kuondolewa kwa Wabunge wa kuteuliwa Wabunge kuwajibishwa na Wananchi,Rais kushtakiwa anapomaliza muda wake kama alifanya fyongo lolote,kupunguza Mamlaka makubwa aliyonayo Rais, n.k.
 
watanzania tupiganie haki yetu. nchi ni tajiri kwa maliasili lakini maskini wa kutupwa. ona tanzanite, almas, coal, mafuta, gas, dhahabu, chokaa, mbuga za wanyama na nyingine nyingi zipo chini ya watu wa nje kisa ubinafsishaji ilhali kuna wachache wanafaidi kupitia rasilimali. uongozi sasa upo kikabila na mahusiano ya kifamilia au kujuana kwa kusoma pamoja au umaarufu wa baba au mama au mjomba japo mjomba nikwakiasi kidogo. jaribu kufuatilia uongozi tangu 1970 utakuta sir name (majina ya ukoo) yanajirudia. iv nchi twaipeleka wapi. tusimamishe katiba mpya na watanzania tusiwe wajinga kwani kodi zetu ndo hutumiwa na wachache kwa kunufaisha matumbo yao na familia zao huku wengine ata 2000 kwa wiki mtu haipati.
 
watanzania tupiganie haki yetu. nchi ni tajiri kwa maliasili lakini maskini wa kutupwa. ona tanzanite, almas, coal, mafuta, gas, dhahabu, chokaa, mbuga za wanyama na nyingine nyingi zipo chini ya watu wa nje kisa ubinafsishaji ilhali kuna wachache wanafaidi kupitia rasilimali. uongozi sasa upo kikabila na mahusiano ya kifamilia au kujuana kwa kusoma pamoja au umaarufu wa baba au mama au mjomba japo mjomba nikwakiasi kidogo. jaribu kufuatilia uongozi tangu 1970 utakuta sir name (majina ya ukoo) yanajirudia. iv nchi twaipeleka wapi. tusimamishe katiba mpya na watanzania tusiwe wajinga kwani kodi zetu ndo hutumiwa na wachache kwa kunufaisha matumbo yao na familia zao huku wengine ata 2000 kwa wiki mtu haipati.

Yan uko sawa kabisaaaaa.......ni vema kama tunatoa elimu kwa wenzetu wasiolielewa hili
 
Je sasa tuna sirikali ngapi?
1) Kuna mawziri wa sirikali ya Zanzibar.
2) Kuna mawaziri wa sirikali ya muungano.
3) Kuna mawaziri wasio muungano. Hawa ni mawaziri wa nchi gani. Ni wa Tanzania bara, ama ni wa Tanganyika.
Kwa vyovyote ni mawaziri wa sirikali ya tatu.
TUNAZO SIRIKALI TATU.

Tukiamua kuwa wa kweli tukubali hivyo... tupunguze idadi wizara nakupunguza gharama.
Suala la majina ya viongozi wa hizi sirikali sio tatizo.

SIRIKALI MBILI...MAWAZIRI 90.
SIRIKALI TATU ...MAWAZIRI 40.
Ipi ghali!!!!!!!!!!!!!!
 
Hivi wajumbe wa tume hawana soft copy ya randama wakaweka kwenye mitandao ya kijamii. Kama serikali imefunga tovuti waturushie maana nina uhakika wanayo soft copy
 
Mimi naona serikali ishinikizwe kufungua tovuti ya tume ili wananchi wasome hizo randama. Serikali ilikuwa na lengo gani kufunga tovuti ya tume? Nia yake ilikuwa nini?Je,walikuwa na nia njema au mbaya?
 
Back
Top Bottom