Rasimu ya II ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Rasimu ya II ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mimi naona serikali ishinikizwe kufungua tovuti ya tume ili wananchi wasome hizo randama. Serikali ilikuwa na lengo gani kufunga tovuti ya tume? Nia yake ilikuwa nini?Je,walikuwa na nia njema au mbaya?
Unauliza kama serikali ilikuwa na nia njema au mbaya katika kuifunga tovuti ya Tume ya Warioba?

Hapo jibu liko obvious, kuwa hao maccm na serikali yao, waliifunga huyo tovuti ya Tume, ikiwa ni mkakati maalum wa hao maccm, kufanya wananchi wasiwe na access ya randama zinazoelezea sababu za msingi, kwa nini Tume ilifikia kuandika ibara hizo, zilizomo kwenye Rasimu ya Katiba.

Tatizo kubwa la CCM, ni kupenda kuchakachua each and everything, lengo lao kubwa ni kutaka kuichakachua rasimu ya Tume ya Warioba, ili 'watuchomekee' rasimu yao mbadala, waliyoi-draft pale mtaani Lumumba!
 
Mimi Dr Cyril August Chami, Mbunge wa Moshi Vijijini (CCM) napenda kueleza masikitiko yangu kwa taarifa za uzushi na za kutunga kuwa eti mke wangu asiye na jina amemuua mfanyakazi wetu Mwislamu kwa sababu "marehemu" alikataa kwenda kanisani.

Mimi sina mfanyakazi wa jina hilo la Mariamu. Wala sina mfanyakazi mwenye umri wa miaka 16. Hatuna tatizo lolote la mfanyakazi yeyote kupigwa, achilia mbali kuuawa.

Lakini taarifa hizo ambazo ni za uongo mtupu zimewashtua wengi kwa sababu zimejengwa katika misingi ya chuki za kidini. Mwandishi alilenga kuifanya jamii iamini kwamba mke wangu ambaye ni Mkristo anawalazimisha wafanyakazi wetu wasio Wakristu waikane dini yao na kuwa Wakristo. Alilenga kuibua chuki dhidi ya Waislamu na familia yangu.

Kwa hakika, mikakati hii ya kuichafua familia yangu inasababishwa na harakati za ubunge Moshi Vijijini 2015. Wapinzani wangu wanajua wazi kuwa hawana hoja ya msingi ya kuwafanya wapiga kura wasinirudishe kwenye nafasi ya ubunge. Kwenye jukwaa na hata kwenye medani ya maendeleo wanakwama. Kwa mfano, kabla ya barabara za lami kuanza kujengwa walisema mimi sina ushawishi wa kuifanya Serikali kuzijenga. Sasa zimejengwa na zinaendelea kujengwa wanajenga hoja kuwa sihusiki wala Serikali ya CCM haihusiki, bali ni Benki ya Dunia inajenga!!! Wananchi wanawauliza kwani kabla ya Dr Chami kuwa mbunge Benki ya Dunia haikuwepo? Wanakosa hoja! Hivyo hivyo kwa mashule, maji, vyuo vya ufundi nk.

Kwa hiyo kwa upeo wao wanaona silaha pekee waliyo nayo ni kuzua kashfa dhidi yangu. Miezi michache iliyopita walizua nimeuza shamba la KNCU kwa shilingi bilioni 4 wakati mimi sina wadhifa wowote KNCU. Eti nimeuza nyumba mbili za Coffee Curing Moshi wakati mimi sina wadhifa wowote Coffee Curing.

Walipoona tuhuma hizo za kutunga hazijakubalika masikioni mwa wapiga kura wa Moshi Vijijini, sasa wamezua hili la mke wangu kuua ili Waislamu wa Moshi Vijijini wanione mtu nisiyefaa.

Sasa mimi napenda kuwauliza maswali haya:

Huyo mke wangu muuaji anaitwa nani? Inaingia akilini kweli kwamba mke huyo muuaji hafahamiki jina kwa hao "majirani" wetu wa kufikirika?

Binti Mariamu kauawa mji upi? Kwa nini majirani hao wenye uchungu hawajatoa taarifa kwa RPC wa mkoa au kanda husika?

Maiti kahifadhiwa hospitali ipi? Au "mke" wangu amekaa naye ndani baada ya kumuua na majirani wamekaa kimya tu?

Kwa desturi za dini ya Kiislamu binti huyo angeshazikwa sasa maana kwa mujibu wa habari hiyo ya kizushi, "aliuawa" usiku wa kuamkia jana. Je, kazikwa makaburi yapi na yako mji gani? Nani kahudhuria hayo mazishi? Kwa nini vyombo vya habari visituonyeshe hayo mazishi?

Kwa nini RPC mhusika asimkamate huyo mke wa mbunge fedhuli namna hiyo na muuaji asiyevumilika?

Kwa nini polisi hawajaniita mimi Dr Chami kunihoji kuhusu huyo "mke" wangu? Si wanajua niko jimboni Moshi Vijijini na RPC Boaz wa Kilimanjaro anafahamu niko jimboni, tena jana nimeutembelea msikiti mmoja kwa minajili ya kuutafutia umeme na maji?

Sote tunafahamu kuwa kuna mkuu mmoja wa mkoa alimuua mtu kwa kumpiga risasi na alikamatwa akapelekwa mahabusu. Huyo mke wa Dr Chami ni maarufu kuliko Mkuu wa Mkoa? Kwa nini asikamatwe tuione sura yake magazetini?

Majibu ya maswali haya HAYAPO kwa sababu kila kitu kimetungwa kwa kujenga chuki tu. Hakuna Mariamu, hakuna kipigo, hakuna kifo. Ila kuna UBUNGE WA MOSHI VIJIJINI. Ndio unaopiganiwa, hamna kingine.

Napenda kuwaasa wanasiasa wenzangu kuwa Watanzania wa leo si wa jana. Si jambo rahisi kuwaghilibu kwa staili hii. Waende kwa wananchi wachape kazi. Wasipofanya hayo wakadhani uongo wa mitandao utawapa ubunge watashangazwa mwaka kesho 2015.

Mimi naendelea kuwaahidi wapiga kura wangu utumishi wa dhati. Nawapa pole ndugu zangu wa Kiislamu kwa usumbufu walioupata. Waislamu wa Moshi Vijijini wananifahamu kama kiongozi nisiyewabagua kwa sababu ya dini yao. Wanafahamu kuwa nawapenda na nafahamu kuwa wananipenda sana. Ndiyo maana wengi wamejiuliza iweje tena mke wangu amwage damu ya Mwislamu kwa sababu iliyotajwa. Naendelea kuwaahidi Waislamu wote upendo na ushirikiano siku zangu zote za kuwatumikia.

Wasalaam

Dr Chami.
 
Kweli tumuombe slowslow atutumie kwenye mtandao.
 
Jaman naombeni ufafanuzi juu ya kauli ya MWIGULU. RAISI HAKUSAINI RASIMU ALISAINI TANGAZO LA SERIKALI
 
Kwani kwa sasa bado tuna Muungano wa Serikali mbili? Au tunadanganyana tu? Viongozi wetu wote kuanzia na rais, wabungr, mawaziri na viongozi wa dini zote waache UNAFIKI na UWONGO, walinde maslahi ya Taifa, waanze kuwa wakweli na wajue watanzania wasasa si wale wa mwaka 47.
 
Nashangaa. Ni kweli wote wanaozungumza na kuandika, hawaoni kwamba tatizo ni kundi la Tanzania Kwanza (CCM) na sio UKAWA. CCM wakikubali kujadili Rasimu ya Tume, na kukubali ukomo wa madaraka ya Bunge la Katiba, UKAWA watarudi bungeni na mchakato utaendelea.
TATIZO NI CCM SIO UKAWA.
 
Sasa watakwenda bila mkubaliano ili waka buruzwe kama mang'ombe UKAWA wanasimamia maslahi ya taifa na ndo s7b wako nje
 
kinachohitajika ni bunge ccm kukubali kujadili risimu ya matakwa ya wananchi . hii ndo itakuwa suluisho la mgogoro mana UKAWA watarudi bungeni
 
Ya leo yanatosha. Wazee ("wanaongoja kufa") na vijana wao wameeleza yote kwa marefu na mapana. CCM ikubali kujadili Rasimu la sivyo mchakato uairishwe, yafanyike marekebesho ya kufanya uchaguzi huru na wa haki. Halafu mchakato urudiwe baadaye.
 
mbona haifunguki au umeweka ile ya CCM maana wanasema yenyewe ilifichwa
 
Hatimaye hii hapa wadau! Jisomeeni.

Unayo maelezo ya ufafanuzi wa hii rasimu Mkuu? katika soft copy? Maelezo ambayo nasikia yapo yaliyoongezwa kuweka ufafanuzi kwenye vipengele mbalimbali? Naiomba hiyo kama unayo tafadhali.
 
Wazanziba huu ni wakati wenu kujinyakuli nchi kilaini maana muda mrefu mmekuwa mukipita mlango wa nyuma kutaka ka nchi kenu sasa mambo yapo hadharanu mshindwe wenyewe. Mkumbuke baada ya hapa hakuna tena kudai nchi . Tatawanyanganya bendera yenu ,hakuna tena wimbo wa taifa mtajiju !!!!!.
 
Ahsante mdau kwa kutupatia rasimu hii jamvini hapa

Hivi ni nani aliyeifunga tovuti ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba (Tume ya Warioba)? Maana hata wenyewe jana walikuwa wanashangaa! Na ameifunga kwa madhumuni gani?
 
Back
Top Bottom