Kwanza tujue walioanzisha serikari moja lengo ilikuwa nini
naninyi munaoanzisha serikari tatu lengo
ni nini
Ipo wazi tu kwamba Nyerere kama alivyo Karume walijua umhimu wa kuwa na nchi moja serikali moja. Lakini tujiulize kwamba ni kwa nini Nyerere alikataa wakati Karume alikubali ?
Tukifikiria kwa undani tutagundua kwamba Nyerere akigundua kuwa patakua na mgogoro wa madaraka kati yake na Karume; Je,Karume angekubali moja kwa moja kumwachia Nyerere urais wa hiyo serikali moja wakati Nyerere alitamani kuwa rais wa maisha wa ?Je,Nyerere angekubali kumwachia Karume Urais wakati alijua fika kwamba elimu yake ilika ndogo?
Na alipofikiria kuhusu serikali tatu aliona pia patakua na mgogori wa kimadaraka;
Je,awe rais wa Tanganyika ?Nani atakua bosi wake,yaani rais wa muungano,na je, atazipeleka wapi hizo nchi mbili ?
Je,aachie Tanganyika yake aliyoipigania mpaka ikapata Uhuru ili awe rais wa Muungano ? na je Muungano ukivunjika atakua mgeni wa nani wakati hana ardhi?
Aliwaza,Nani atawachagua marais wa Tanganyika na wa Zanzibar wakati hakuamini katika Demokrasia ya vyama vingi kwa wakati huo na uchanga wa nchi zote mbili?
Nyerere aliona serikali mbili zinafaa kwasababu alijua kwamba atatawala Tanganyika na Muungano . Ndio maana alijivika koti la Muungano. Pia alijua kwamba Muungano ukivunjika ataendelea kuwa rais wa Tanganyika.Ni ukweli kwamba muungano wa serikali mbili haukuzingatia suala la uchumi kabisa. Ndio maana Zanzibar wanachangia pato la Muungano wanapoamua tu na wala sio suala la kisheria,na kwamba wanaposhindwa kulipa inakuaje?
Mfano tu Zanzibar wana bili kubwa sana ya umeme na hawana mpango wa kulipa.Hakuna mtu yeyote anayeona kwamba huo ni mzigo kwa watu wa bara.
SMZ hailipi kwa sababu ya kutokua na mchanganuo kamili wa kiuchumi kwa sababu watendaji wamejikita zaidi kutafuta vyanzo vya fedha Tanzania Bara.Mafisadi wamejikita bara.
Tujiulize kama kweli Nyerere aliwaza juu ya Zanzibar kumezwa ni kwa nini Rais wa Zanzibar asiwe ndiye Rais wa Jamhuri ya Muugano?
Utagundua kua mfumo wa serikali mbili ni wa kiutawala zaidi sio kiuchumi kwa sababu Zanzibar isipolipa chochote hakuna hatua inayochukuliwa ,na imefanywa kama mwanamke kwenye nyumba. MUUNGANO WA SASA NI WA WATU KUPEANA MADARAKA TU,NDIO MAANA HAWAKO TAYARI KUSIKILIZA MAONI YA WANANCHI.
SUBIRINI KIFUNGU CHA KUPUNGUZA MADARAKA YA RAIS MTAJUA WATAWALA WANATAKA NINI.