RASIMU ya Katiba Mpya Tanzania yazinduliwa


mbona unaonekana huna unachojua,viti maalumu hakuna isipokuwa viti maalum vitakuwa kwa wenye ulemavu,wananchi wanauwezo wa kumfukuza mbunge kama wataona hafai,mbunge wa kuchaguliwa akifa kama alitokana na chama hakuna uchaguzi chama kitapendendeza mwingine,kama alikuwa ni mgombea binafsi uchaguzi mdogo utakuwepo.
 
Yaani wamependekeza serikali 3
Ya shirikisho...
Ya Tanzania bara...
Ya Zanzibar...

Alafu wakajiamulia kutengeneza katiba ya serikali moja (shirikisho) peke yake!!! Sasa hizo mbili wamemuachia nani?!!! Ebo!

wewe ni pimbi kweli? hujui kama zanzibar ina katiba yake? katiba ya tanzania bara itatengenezwa na watanzania bara wenyewe. sasa wewe unataka mambo ya bara yajadiliwe na wazanzibar? ebo
 
Ninaomba nichukue fursa hii kumpongeza joseph sinde warioba kwa kumaliza kukamilisha rasimu ya katiba na hasa kututengenezea katiba isiyolenga kutubagua watanzania kwa misingi mbalimbali mf. ukabila,udini nk. Japokuwa kunamapungufu ya hapa na pale lakini ninaimani mabaraza ya katiba yatafanya kazi yake vizuri na kurekebisha mapungufu hayo. HONGERA SANA WARIOBA
 
Mi nadhani hii tume ilazimishwe kutengeneza katiba za Tanzania bara na Zanzibar haraka sana, tena kwa gharama zao wenyewe. Haiwezekani watumie hela yote kufanya upuuzi kama huu!!!
Aisee wewe kumbe ni Genius ehee!! katiba ya Tanganyika iandikwe kwa ushirikiano na Wazanzibar? au hujui tume ya Warioba ina wajumbe kutoka Zanzibar? tushirikishe akili kabla ya kucomment na tujifunze ku- appliciate pale kazi nzuri inapofanyika.
 
Huwezi kukuta Lumumba project akichangia mada kama hizi..............wao ni udaku na habari za watu tu!

Upo sawa kabisaa mkuu! litle minded people discusses people not issues!
 
Zanzibar wana katiba yao, na ndiyo wataitumia kufanya uchaguzi 2015. Tanzania bara mbona hatuna? au raisi aunde fasta tume nyingine ya Tanzania bara...
 

Wanawake wenyewe waliopo bungeni hawafanyi kitu! Wachache ndio wanakuwa na hoja za msingi. Sasa wakiwajaza humo si itakuwa kero? Nadhani hao wawili kila jimbo ni kwa Muungano. Bara inakuwa na majimbo 25 wanatoka wawili, na Zanzibar majimbo 10 wanatoka wawili. Sidhani kama inahusu wabunge wa bara au zanzibar ambao wao katiba zao inabidi zitamke idadi ya wabunge!
 
Last edited by a moderator:
Pamoja na mapendekezo mengi kwenye TUME kuwa mazuri, lakini bado kuna mapangufu makubwa, mfano madaraka ya rais bado hayajaainishwa vizuri, RAIS kuteua majaji, kwanini huo Mhimili usiteuwe wenyewe na mambo mengine mengi.

Swali langu je hii rasimu inaweza kufanyiwa marekebisho kabla ya kupigiwa kura ya NDIYO NA HAPANA?
 
Hongera Warioba kwa rasimu

Serikali 3
Tume huru
BUNGE huru
 
Yaani wamependekeza serikali 3
Ya shirikisho...
Ya Tanzania bara...
Ya Zanzibar...

Alafu wakajiamulia kutengeneza katiba ya serikali moja (shirikisho) peke yake!!! Sasa hizo mbili wamemuachia nani?!!! Ebo!

naona una hasira sana baada ya sera yenu ya majimbo kupigwa chini
 
madaraka ya rais yameachwa juu mno,.tume ya uchaguzi bado sio huru, kinga ya rais bado ipo!!
 
Mh Bilal anasema wale ambao mapendekezo yao hayamo kwenye rasimu wasifadhaike.Kama kila maoni yangeandikwa kwenye rasimu,tungekuwa na kitabu kikubwa sana.Anashukuru kwa wananchi kushiriki.
 
Hata mi najiuliza. Na hizo serikali mbili (Tanganyika na Zanzibar), zitakuwa na mamlaka gani kimataifa?
mkuu nimekushauri ufiche aibu yako, tulia tumia akili usitumie uji kuandika..hapa tunazungumzia katiba sio sheria
 
bethlehemu warushe draft yote kwennye mtandao watu tuwe mbele kwenye kuchambua. Unaweza kukuta taarfia inachukua wiki nzima kabla ya kuweka kwenye mtandao.Watu wengi hivi sasa hawana access na tv kutokana na ukirittimba wa kisimbusi
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…