RASIMU ya Katiba Mpya Tanzania yazinduliwa

RASIMU ya Katiba Mpya Tanzania yazinduliwa

Labuda!!

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Hii katiba ikikamilika narudi kuishi bongo, naiona Tanzania yangu mpyaaaaa!
 
kama tutakuwa na majimbo 25 tanzania bara na 10 zanzibar hii inamaana sawa na tanzania bara kuwa na majimbo kulingana na mikoa 25 ya zamani na ukitazama kwa ujumla ccm inachukua majimbo mengi katika kila mkoa ukilinganisha na wapinzani ambao wanaambulia jimbo moja or mawili na kwa tanzania visiwani cuf na ccm watagawana nusu kwa nusu

endeleza umburura wako
 
mkuu hiyo ni kwa bunge la muungano, na bado kutakuwa na bunge la tanganyika, na sijui kwenye katiba itasemaje kuhusu bunge la tanganyika!

Bunge la Tanganyika litazungumzwa kwenye katiba ya Tanganyika ambayo haipo kwa sasa so kuna task nyingine ya kuunda katiba ya Tanganyika wenzetu wa Zanziba wao tayari wana katiba yao ni swala tu la kuirekebisha iendane na katiba mpya ya jamhuri ya muungano wa Tanzania!
 
Kinga ya rais bado ni utata pamoja na uteuzi wa majaji ni utata mtupu hapa naona viraka mi siafikiani na rasimu hii.
 
Twakimu zako zinazingatia nini?

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
Watanzania inabidi tuichambue hii rasmu kwa tahadhari kubwa, maana bila kuwa makini, hayo mataifa mawili ndani ya muungano yataleta shida, mathalani rais wa muungano wa atachaguliwa kwa uwiano upi wa kura? Kati ya bara na zanzibar! Bila kuweka vizuri itakuwa hatari mbele...
 
Wadau, sijui kama tumeliona hili. Rasimu ya leo ni ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. kazi iliyo mbele yetu bila shaka ni ya kuandaa Katiba ya Tanzania Bara (Tanganyika). Je, muda huu unatosha kabla ya mwaka 2015?
 
kama tutakuwa na majimbo 25 tanzania bara na 10 zanzibar hii inamaana sawa na tanzania bara kuwa na majimbo kulingana na mikoa 25 ya zamani na ukitazama kwa ujumla ccm inachukua majimbo mengi katika kila mkoa ukilinganisha na wapinzani ambao wanaambulia jimbo moja or mawili na kwa tanzania visiwani cuf na ccm watagawana nusu kwa nusu
usilolitilia maanani ni kuwa mfumo wa uchaguzi utabadfilika pia. kubwa zaidi ni mfumo utakaoongoza serkali ya tanganyika/bara.
 
Back
Top Bottom