RASIMU ya Katiba Mpya Tanzania yazinduliwa

RASIMU ya Katiba Mpya Tanzania yazinduliwa

Kizungumkuti naona anyway inawezekana JK akaendelea kuwa madarakani hadi 2017!

Muda wa Rais ukifika mwisho Bunge ikibidi litachagua Kati ya Marais wastaafu kuwa Rais wa mpito...

Au ndani ya tume ya katiba...Warioba au Salim ...ashike kwa Muda au Jaji Mkuu.
 
Pamoja na mapungufu ya hapa na pale lakini kwa kiasi kikubwa Tume ya Warioba imefanya kazi kubwa.Lazima ukweli usemwe.
 
Hapo umeneno wana assume kama vile hakutakuwa na mgombea binafsi asiyekuwa na chama huyo nani atamrithi, au watatakiwa kuacha wasia wa nani atarithi kiti chake, hili jambo ni la ovyoo, demicrasia lazima iheshimiwe, watu wachague viongozi hii nchi democrasia ndo inakua hata kupiga tu kura watu bado hawajitokezi kuache kuweka vichocheo vya kukuza voter apathy nchini ni kosa kubwa! Akifa/akijihudhuru au kwa namna yoyote nafasi ya kuchaguliwa yoyote ikibaki wazi lazima uchaguzi ufanyike, hii ndo gharama ya democracy!
Kasema uchaguzi utakuwepo tu endapo mbunge alikuwa ni mgombea binafsi.
 
Hii rasimu imeandaliwa kwa jicho la uchaguzi wa 2015. Bado haijaangalia kwa undani matatizo ya msingi ya muda mrefu ya wananchi.Taasisi muhimu za kutoa haki hazijaguswa(kiutendaji na kiwajibikaji).'Conduct' za 'members' wa hizi Taasisi bado utata.Masuala ya rasilimali,ardhi,maliasili,uraia nayo utata. Hii rasimu imetengenezwa kukipa Chama cha mapinduzi (CCM )
'fake Political Bonhomie' machoni kwa wananchi..

ungesubiri kwanza kwanza uisome yote ndipo ulaumu ule ufafanuzi aliotoa warioba ni kwa kiwango kidogo sana kuwa mpole mkuu.
 
Haswa hapo kwenye serikali tatu rasimu imekuwa sikivu mbunge kutokuwa waziri hzo nimezipenda
 
Sijaona rasimu yote, ila kwa haya machache yaliyondikwa hapa bado naona kuna vitu muhimu vya kuangalia upya:

1. Separation of power. Bila kufanya Mahakama kuwa huru basi Katiba mpya ni bure. Rais asiwe na mkono kwenye huu mhimili. Uteuzi wa majaji uwe chini ya kamati maalum lakini muhimu sana majaji waombe hizo nafasi. Mtindo wa sasa Rais anateuwa majaji na tayari tunaona ni jinsi gani kumekuwepo na migongano. Sioni umuhimu wa kuwa na katiba mpya kama Mahakama itaendelea kuwa 'koloni' la serikali.

2. Urais - kuna post inasema kuwa imependekezwa ukomo wa urais uwe awamu tatu! Hili ni tatizo kubwa, tena kubwa sana. Awamu mbili zinatosha.

2. Mamalaka ya wananchi kuwasimimia viongozi na hasa viongozi wa juu serikalini, yameminywa. Ingefaa rais amependekeze majina ya baraza la mawiziri lakini uthibithisho wa mawaziri hayo utoke kwa wananchi kupitia kwa bunge. Hili ni muhimu sana ili kuepuka mawaziri mzigo!
 
Leo katiba mpya imezinduliwa na kusambazwa kwa makundi mbalimbali. Naomba mwenye rasimu hiyo iweke humu ili tuisome na kuijadili
 
Lisu bado hajapona ule ugonjwa wa mwisho wa mwezi

Wewe gamba tena la mamba, unaleta uccm wako hata kwenye mambo ya kinchi. Kama ugonjwa wewe unaumwa UBONGO na ndio maana unaandika bila hata kufikiri!
 
Katiba inapaswa iweke sawa mambo uliyo dodosa pamoja na yafuatayo ambayo ni tatizo kwa Taifa:
1. Itaratibu wa kusign yenye maslahi ya kitaifa.
2. Speaker wa bunge asiwe mbunge. apigiwe kura na wananchi.
3. Mawazir wasiwe wabunge.
4. Tume ya uchaguzi iwe huru, isiwekwe na rais. iwekwe na kamati ya Bunge kisheria.
5. Iwe marufuku masuala ya dini kuingilia katiba. Mambo ya imani yatatuliwe ndani ya mipaka ya kidini bila kuingilia wala kukwaza imani ya yeyote.

Just kwa ufupi.
 
kweli mkuu hata mi nimeona itabidi watanganyika tuanze mchakato wa katiba ya bara.

Watanganyika inatulazimu kuachana na mchakato wa Katiba ya Tanzania badala yake tuanze kuifuta vumbi ile katiba ya Tanganyika na kuipulizia uhai upya.

Hatuhitaji katiba ya bara, tunahitaji katiba ya Tanganyika.

Link https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/125524-nchi-yetu-inaitwa-tanganyika.html

Link https://www.jamiiforums.com/jf-chit-chat/127716-tanzania-kuna-serikali-tatu.html
 
hii rasimu wazanzibar tunaikataa sababu imkuja na yale yale ukoloni zanibar ndani ni nchi kimataifa sio nchi na tanganyika ndani ni nchi kimataifa sio nchi

kwa maana hiyo zanzibar haitaweza kujiunga na jumuiya za kimataifa wala kuwa na uhusino na taifa lolote lile na tanganyika haiwezi kujiunga na jumuiya yoyote ile ya kimataifa

kwa maana hiyo basi serekali kuu moja tu tanzania na kuifanya nchi wahusika kuwa kama ni majimbo

hili wazanzibar hatulikubali hivyo mambo ya nje na uhusiano wa kimataifa lazima vitolewe kwenye muungano uhamiaji lazima utolewe kwenye muungano hivyo

paspot itabakiya kuwa ya muungano ila kila nchi iwe nanembo yake kwenye passport hiyo na kusimamia sera zake za uhamiaji

muungano huu ni ukoloni ila tutahakikisha tunauvunja
 
kama tutakuwa na majimbo 25 tanzania bara na 10 zanzibar hii inamaana sawa na tanzania bara kuwa na majimbo kulingana na mikoa 25 ya zamani na ukitazama kwa ujumla ccm inachukua majimbo mengi katika kila mkoa ukilinganisha na wapinzani ambao wanaambulia jimbo moja or mawili na kwa tanzania visiwani cuf na ccm watagawana nusu kwa nusu
 
Mkuu naelewa. Ninachoona mimi ni kuwa huu mchakato wa katiba umefanywa ovyo kabisa ili 2015 ama tusiwe na uchaguzi, au tutumie ile ile katiba ya zamani.
Hebu jiulize; Mwaka 2014 hii katiba ya shirikisho ikikamilika, je 2015 Watanganyika tutapiga kura kuchagua viongozi wetu kwa kutumia sheria ipi? Tutatumia katiba ipi? Hiyo katiba itatengenezwa lini? Tume ya kutengeneza hiyo katiba itaundwa na nani? Endapo "Tanganyika" hatutafanya uchaguzi 2015, Je tutachagua raisi wa shirikisho na wa Zanzibar? Baada ya hapo Tanganyika itakuwa inaongozwa na nani (Kumbuka serikali ya shrikisho itahusika na mambo 7 tu)?

Labda ndiyo ile kitu ilisemwa na Lipumba ................. mipango ya kumuongezea Mkuu wa Kaya Ulaji mpaka 2017!!
 
Back
Top Bottom