RASIMU ya Katiba Mpya Tanzania yazinduliwa

RASIMU ya Katiba Mpya Tanzania yazinduliwa

bunge la muungano litakuwa na wabunge 75 tu. baraza la wawakilishi litakuwa kama kawa na tanganyika itakuwa na wabunge wake ambao watakuwa na bunge lao kama lilivyo baraza la wawakilishi zenji

Mabunge ya nchi za Muungano pia lazima ziwe na wabunge wachache na idadi kubwa ya wabunge siyo justfication ya uwakilishi au demokrasia bora.Ulazima wa kuwa na wabunge wachache ni muhimu sana wakati huu
 
Watanzania wanapenda mazingaombwe sana; kwa kadiri ambavyo nimefuatilia kwa juu juu na nikiendelea kusubiri kuona rasimu yenyewe ya hiyo Katiba mwitikio wangu ni tahadhari.

mkuu subiri kwanza uipate ondoa hofu mimi nimeipata kwa kutoa kopi toka kwa wanahabari iko poa.
 
Ninaomba nichukue fursa hii kumpongeza joseph sinde warioba kwa kumaliza kukamilisha rasimu ya katiba na hasa kututengenezea katiba isiyolenga kutubagua watanzania kwa misingi mbalimbali mf. ukabila,udini nk. Japokuwa kunamapungufu ya hapa na pale lakini ninaimani mabaraza ya katiba yatafanya kazi yake vizuri na kurekebisha mapungufu hayo. HONGERA SANA WARIOBA

Natofautiana kidogo sana na wewe. Mimi natoa pongezi zangu kwa Tume ya katiba kwa ujumla na sio kwa mtu mmoja.
 
kifo cha ccm kimewadia,sasa rais kushtakiwa na bunge,viti maalum hakuna, pamoja na mengi mazuri kali ni kuwa mbunge akifariki,mrithi atatoka chama alichokuwa aliyefariki,hapa kuna tatizo kwani ni sawa na kuamini wananchi walichagua chama na si mtu kwa sifa na uwezo wake,pia ni kuamin anayepewa nafasi anakubalika na pia ni kuwanyima haki za msingi watu wanaopenda na wenye nia ya kuleta maendeleo. My intake: Tusitishwe na gharama za uchaguzi kwa kumteua mtu asiyefaa.

hata katika katiba iliyopo, bunge lina nafasi / uwezo wa kumshitaki rais. Issue ni kuwa hali halisi ya mambo na ulindanaji hauwezeshi rais kishitakiwa. Wanambeba ila uwezo wanao kikatiba.
 
Hapo umeneno wana assume kama vile hakutakuwa na mgombea binafsi asiyekuwa na chama huyo nani atamrithi, au watatakiwa kuacha wasia wa nani atarithi kiti chake, hili jambo ni la ovyoo, demicrasia lazima iheshimiwe, watu wachague viongozi hii nchi democrasia ndo inakua hata kupiga tu kura watu bado hawajitokezi kuache kuweka vichocheo vya kukuza voter apathy nchini ni kosa kubwa! Akifa/akijihudhuru au kwa namna yoyote nafasi ya kuchaguliwa yoyote ikibaki wazi lazima uchaguzi ufanyike, hii ndo gharama ya democracy!

Kama alikuwa mgombea binafsi (huru), akifariki uchaguzi unaruitishwa upya. Nadhani hapa cha msingi ingekuwa kwamba, badala ya kurudia uchaguzi. Basi yule aliyemfatia kwa wingi wa kura za wananchi ndiye apitishwe kuwa Mbunge.

Halafu nahisi biashara ya waganga wa kienyeji ikiongezeka maradufu...Mtu akishika nafasi ya pili kwenye kura za maoni wakati mmeshatolea bastola kwenye kugombea hiyo nafasi, basi ''anatengeneza'' tu huyo aliyeshinda!
 
what is this animal "tanzania bara"????????????????????????????????????????
We need our tanganyika, i cant wait kuwa mwana tanganyika jaman.
Jina Tanganyika lisikuchanganye kwani hata hilo jina lenyewe ni la wajerumani (siyo waafrika waiolichagua) na sijui walitoa wapi hilo jina hawa wajerumani! Nchi nyingi zimebadili majina ya nchi zao na hivyo jina si hoja ya msingi sana tunaweza hata kuwa na jina lingne badala ya hilo la tanganyika ambalo pengine hata wewe hujui asili yake ila unashahabikia tu! Hoja ya msingi hapa ni taifa huru lenye katiba bora na uongozi madhubuti! na nadhani hata kwenye maoni hili suala la jina la nchi (Tanganyika) lijadiliwe na kutoa nafasi ya kupendekeza jina lingine kama itaonekana kuna sababu za msingi za kufanya hivyo!
 
Rasimu imeacha mambo ya msingi mengi tu kubainisha kwa maoni yangu
1. Rasilimali za Nchi (Ardhi na Madini, Mafuta, gesi) haina budi kutamka bayana umiliki na faida zake
2. Mawaziri kutokuwa wanasiasa hili lazima liwe open bila chenga
3. Sioni mantiki ya kutaja umri wa Rais pasipo kutaja kiwango cha elimu yake; kwa kifupi hatutarajii kuwa na Rais au watendaji wakuu ambao ni 'undergraduate' (kujua kusoma na kuandika) ikiwa directors tu lazima wawe postgraduates
4. Imetaja kiswahili kama tunu ya taifa kwa maana inaleta umoja, lakini ilikuwa itaje wazi Kiingereza ni Lugha ya kufundishia katika level zote za elimu na pia official language, hii tusipepese macho-dunia iko katika vita ya utawazi ambao msingi mkubwa ni elimu na nguzo ya elimu ya utandawaizi ni kimombo
5. Haina maana kutaja wabunge wanaume au wanawake then kuacha sifa ya kujua kusoma na kuandika ili wakaendelee kupiga meza; kiwango cha elimu ya mbunge kibainishwe
6. Tume iliambiwa iandae Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania sio katika ya muungano, kwa maana ilitakiwa mambo yalioko ndani ya muungano yabainishwe au yatolewe ushauri (U-DC, RC Division Officers etc) maana kwa sasa kuna mlundikano mkubwa sana wa vyeo katika eneo moja; Tume watoe majibu isjie kuwa Pesa zote walizokula wameenda kuandaa misingi ya mambo saba tu, uhuni huu
7. Katiba ijibu kilio cha uwazi na upatikanai wa taarifa za Serikali katika masuala yote (hususan Mikataba ya Rasilimali za nchi isiwe siri, ijadiliwe na chombo mahsusi ili ikifanywa kisanii tunaju ni hicho chombo ndio kimefanya "uchenge" na iwekwe wazii, hakuna sababu za kuficha mikataba ya rasilimali ni janga)
8. Kada zote za juu zisiwe za kuteuliwa bali ziwe za kushindaniwa
9. Hili la wabunge 2 kwa jimbo siliungi mkono lakini nashawishika kulikubali kwa kuwa sina "alternative ya kuwa na mfumo bora wa kuweza kupata wabunge wanawake jimboni) na idadi yao inanishawishi. Hata hivyo, inategemea na muundo wa Serikali za tanganyika na Zanzibar ili kujua wapiga meza watakuwa wangapi
10. Katiba iwe wazi katika kulinda na kutetea haki za wananchi ili kuepusha ubabe wa polisi kwa raia simply wanachukuliana mabwana/mabibi; hili lianishwe vema haki za raia
11. Muundo wa mamlaka za juu za uongozi wa nchi kwanini hazina mapendekezo?
Kwa kifupi, Raimu ni tupu, ingefaa hata kuboresha iliyopo kama haitataja maeneo ya msingi kama baadhi hapo juu.
 
Hapo ni ujinga mtupu. Jimbo kuwa na wabunge wawili kwa maslahi ya nani na kuwakilisha nani? na raisi anakuwa na wabunge kuwakillisha nini?. inamaana tutakuwa na wbunge zaidi ya 700 na gharama za kufuga wadudu hao zitalipwa nani.Wanawake wanaweza na wamekwisha jiwezesha waingie kupambana.Lazima mihimili hii iwe tofauti.
Acha kukurupuka kanga weee!!! Siyo kudandia gari kwa mbele! Sikiliza lecture yote kwanza kabla ya kuanza kuuliza ugolo!
 
There are currently 1325 users browsing this thread. (256 members and 1069 guests)

 
Mkuu naelewa. Ninachoona mimi ni kuwa huu mchakato wa katiba umefanywa ovyo kabisa ili 2015 ama tusiwe na uchaguzi, au tutumie ile ile katiba ya zamani.
Hebu jiulize; Mwaka 2014 hii katiba ya shirikisho ikikamilika, je 2015 Watanganyika tutapiga kura kuchagua viongozi wetu kwa kutumia sheria ipi? Tutatumia katiba ipi? Hiyo katiba itatengenezwa lini? Tume ya kutengeneza hiyo katiba itaundwa na nani? Endapo "Tanganyika" hatutafanya uchaguzi 2015, Je tutachagua raisi wa shirikisho na wa Zanzibar? Baada ya hapo Tanganyika itakuwa inaongozwa na nani (Kumbuka serikali ya shrikisho itahusika na mambo 7 tu)?

Link 1. https://www.jamiiforums.com/habari-na-hoja-mchanganyiko/100638-shirikisho-ndani-ya-shirikisho.html

Link 2. https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/334649-tundu-lissu-na-kiinimacho-cha-muungano.html

Leo ni siku ambayo Jaji Warioba ameamua/amelazimika kuondoa usanii wa "Tanzania bara"/"wabara". Warioba anaondoka na ukiini macho wake. Tanganyika inasikika tena.

Leo ni siku mbaya kwa MJJ na Maalim Nguruvi3. Naomba mjizoeshe tena kuitaja "Tanganyika"

Wadanganyika tunabadili jina hili rasmi na kuchukua hadhi yetu,"Watanganyika"

Tanganyika Tanganyika, nakupenda kwa moyo wote.

Je shirikisho la Tanzania litatokana na majimbo mawili au nchi mbili?

Tanganyika na Zanzibar zitakuwa nchi ndani ya muungano au zitakuwa ni majimbo ya muungano?

Mizengo Pinda-"Zanzibar si nchi"
J: Kikwete " Zanzibar ni nchi ndani, sio nchi nje"

"Tanganyika ni nchi.Tanganyika si nchi ndani, ni nchi nje." - Rasimu ya Katiba mpya.
 
Hapo kwenye mawaziri nakupinga kidogo. Raisi lazima awezekupanga safu yake. Muhimu ni bunge liweze kuthibitisha uteuzi huo. Sasa hata akishindwa kuteua mawaziri itakuwaje hapo?

Huyu tatizo lake hajujua kwamba Urais ni Taasisi hivyo inabidi uwe na nguvu Kitaifa Tatizo lililopo anaogopa Raisi kuwa na madaraka makubwa anadhani tutaendelea kuwa na maraisi weoesi kama Kikwete
 
Kizungumkuti naona anyway inawezekana JK akaendelea kuwa madarakani hadi 2017!
 
Sasa Katiba ya Tanganyika itatengezwa lini? ama ndio hiyo? hahahahahah, kazi kweli kweli, ikiwa ni serikali tatu. sasa hapa ndio niliposema Think Tank hii inaiona Zanzibar Nachingwea, Zanzibar Kwanza kubembelezana baadae.
 
tumebimefanya kazi nzuri ila hapo kwenye wabunge wawili kila jimbo hapana hatuwezi kukubaliana na upuuzi wa namna hii, hii ni katiba kwa miaka 50 ijayo isiandikwe kuwasaidia kina sophia simba kurudi bungeni na kuwaachia watoto zetu urithi mbaya kana kwamba tulikuwa mazezeta. Nasema no wabunge wawili kwa jimbo moja.

nakubalina na tume kwa idadi ya wabunge 75 na idadi ya majimbo ya uchaguzi. Nadhani hii inamaana idadi iliyopo sasa itapungua. Nisichokubaliana nao ni uwiano sawa kati ya me na ke.
 
Tunaomba watuwekee hiyo rasimu online. Au kama kuna mtu anayo soft copy atumwagie hapa
 
''kiwango cha kura mtu kuchaguliwa kuwa rais............kwa sasa ni mtu kuwa na kura nyingi
tume inapendekeza mgombea lazima apate asilimia zaidi ya 50''....Hapa ni PATAMU sana!
 
Link 1. https://www.jamiiforums.com/habari-na-hoja-mchanganyiko/100638-shirikisho-ndani-ya-shirikisho.html

Link 2. https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/334649-tundu-lissu-na-kiinimacho-cha-muungano.html

Leo ni siku ambayo Jaji Warioba ameamua/amelazimika kuondoa usanii wa "Tanzania bara"/"wabara". Warioba anaondoka na ukiini macho wake. Tanganyika inasikika tena.

Leo ni siku mbaya kwa MJJ na Maalim Nguruvi3. Naomba mjizoeshe tena kuitaja "Tanganyika"

Wadanganyika tunabadili jina hili rasmi na kuchukua hadhi yetu,"Watanganyika"

Tanganyika Tanganyika, nakupenda kwa moyo wote.

Je shirikisho la Tanzania litatokana na majimbo mawili au nchi mbili?

Tanganyika na Zanzibar zitakuwa nchi ndani ya muungano au zitakuwa ni majimbo ya muungano?

Mizengo Pinda-"Zanzibar si nchi"
J: Kikwete " Zanzibar ni nchi ndani, sio nchi nje"

"Tanganyika ni nchi.Tanganyika si nchi ndani, ni nchi nje." - Rasimu ya Katiba mpya.
Tungevunja na Muungano kabisa ili hawa Wazanzibar waendelee na mambo yao kule visiwani ikiwemo Serikali kulazimisha watu hata wasio waislam kushirika mambo ya Waislam kama kufunga biashara za chakula, kutokula hadharani as if ni nchi ya Kiislam, GO ZANZIBAR GO!!!!!!!!
 
Sasa Katiba ya Tanganyika itatengezwa lini? ama ndio hiyo? hahahahahah, kazi kweli kweli, ikiwa ni serikali tatu. sasa hapa ndio niliposema Think Tank hii inaiona Zanzibar Nachingwea, Zanzibar Kwanza kubembelezana baadae.

Kuwa na serikali tatu ni kuuzika Muungano! R.I.P MUUNGANO
 
Back
Top Bottom