RASIMU ya Katiba Mpya Tanzania yazinduliwa

hapa cha msingi ni Let Zanzibar go, hakuna cha serikali tatu hilo ndio suluhisho...

Demokrasia ina gharama zake. Mfumo huo mpya wa serikali tatu ni cheaper(una gharama nafuu) kuliko wa sasa kwasababu:
1.Mfumo mpya una mawaziri wachache kuliko wa sasa.
2.Mfumo mpya una wabunge wachache kuliko wa sasa(375).
3.Mfumo mpya utakuwa na wafanyakazi wachache kwenye wizara husika kuliko wa sasa.
4.Mfumo mpya utakuwa na wafanyakazi wachache kwenye ofisi za bunge kuliko wa sasa.
5.Mfumo mpya utakuwa na uwajibikaji mkubwa kuliko wa sasa, ambao mamilioni ya pesa za walipa kodi yanapotea.

Hivyo basi, mfumo mpya wa dola unapunguza kwa kiasi kikubwa gahrama za uendeshaji wa dola.

Naipongeza tume kwa kufanya mambo kisayansi.
 

Peleka maoni yako kwenye baraza la katiba wilayani kwako, kama mzigo tumbo lako mzigo kwa nchi hii
 
 
Pale uliposema wahuni wenye kuongea kwa sauti ya juu ulikuwa unamaanisha sugu,lema na msigwa????? Funguka plz

nimejitahidid kutumia lugha ya kifasihi lakini watanzani wanawajua wabunge wenye tabia za kihuni bungeni na kwenye jamii.
 
aisee kama unayo soft kopy ya hiyo rasimu tutupie na sie tuipate,

mkuu ni kweli ninayo lakini tangu saa kumi na mbili najitahidi kuitumbukiza inagoma sijui kama ni mtandao uko down au la.
 
Watanzania wakati umefika ni lazima tuondokane na mawazo mgando ya serikali mbili, ambazo utekelezaji wake ni mgumu sana kwa nyakati zetu hizi. Lazima tuambatane na fikra mpya na chanya za kuwa na taasisi zilizojengewa misingi ya kikatiba ya uwajibikaji. Demokrasia inayosemwa, sasa inatakiwa iingie kwenye matendo, kuliko kubaki nadharia tuu.

Mfumo huo mpya wa dola utapunguza sana gharama za uendeshaji wa Serikali na Bunge la Muungano kwa kiasi kikubwa, hivyo kuwapunguzia wananchi mzigo. Mfumo huo mpya wa serikali tatu ni cheaper(una gharama nafuu) kuliko mfumo wa sasa, kwasababu:
1.Mfumo mpya una mawaziri wachache(15) kuliko wa sasa(56).
2.Mfumo mpya una wabunge wachache(75) kuliko wa sasa(375).
3.Mfumo mpya utakuwa na wafanyakazi wachache kwenye wizara husika kuliko wa sasa.
4.Mfumo mpya utakuwa na wafanyakazi wachache kwenye ofisi za bunge kuliko wa sasa.
5.Mfumo mpya utakuwa na uwajibikaji mkubwa kuliko wa sasa, ambao mamilioni ya pesa za walipa kodi yanapotea.
6.Mfumo mpya hauna ofisi ya wazili Mkuu, hivyo gharama zote zilizopo sasa za kuiendesha ofisi ya PM na makandokando yake hazitakuwepo.

Hivyo basi, mfumo mpya wa dola unapunguza kwa kiasi kikubwa gahrama za uendeshaji wa dola.
Huu mfumo mpya ni mzuri na unaotekelezeka kirahisi, bila kuhitaji gharama kubwa. Mfumo huo upo Ujerumani,Marekani, Afrika kusini, Uingereza, India Nk

Mfumo huu mpya utatoa ajira nyingi kwa vijana wetu wasomi, kwasababu upatikanaji wa fursa za kazi hautakuwa unatawaliwa na mfumo wa kikilitimba, miungu watu, na kupendeleana kama ulivyo sasa. Kwani kwa sasa kupata kazi lazima uwe ulizaliwa ktk familia ya mwanasiasa fulani au unafahimia na mtu fulani maarufu, au utoe rushwa.

Naipongeza tume kwa kufanya kazi kisayansi.
 
Mkuu acha kuwapotosha watu! tulia soma vizuri rasimu! hao 15 ni wa shirikisho tu, bado wa Tanganyika! upo hapo?
 
nakubaliana nawe hakuna haja kabisa ya kuwa na serikali ya shirikisho kabisa kwani unazo tayari serikali pande zote mbili. hakuna haja ya kuunda serikali kwa ajili ya kusimamia mambo saba ni wasting of money badala yake kungeundwa kamisheni kwa ajili ya kusimamia mambo haya ya muungano.hakuna haja ya kuwa na wabunge wa kuchaguliwa na rais na suala la wabunge wawili mwanamke na mwanaume lifutwe pia kwani wanawake kila siku wamekuwa wakilalamka kutodharauliwa kwa kupewa vitu vya dezo kwahiyo katiba hii itaendeleza kumdharau kwa kumtengenezea nafasi wakati anao uwezo wa kugombania kama wengine na kushinda mifano ipo kibao.suala la Madaraka ya urais inabidi liangaliwe upya kwani itaendeleza urais wa kifalme ambao unazalisha viongozi ambao badala a kuumikia nchi wanamtukuza na kumtumikia rais wa nchi.
 
Hapa chenga tupu, kinga ya rais palepale ili aendelee kujiridhisha na masela wake, uteuzi wa mawaziri still chini ya rais japo inafuata professional na kupendekezwa na hao utumishi so either wapendekezaji waweke ndugu zao au wapendekeze majina ya masela wa rais. Nimeona mabadiliko ila sio kwenye maeneo yanayotuletea shida sahv.
 
Kuna wabunge flani wamewateua ndugu zao kuwa wabunge wa viti maalumu...mmoja amempa shemeji na dada yake, mwengine amempa mtoto wake na mkwe wake na mwengine kawapa nyumba kubwa na ndogo zake mbili zipo mjengoni....nadhani sasa tutaheshimiana

hii ndiyo uovu ambao ulikuwa unafanywa na wenye nafasi ya kuteua kwa kugawa viti maalumu kwa watu wao,kwa matakwa yao waliyokusudia.
 
mkuu ni kweli ninayo lakini tangu saa kumi na mbili najitahidi kuitumbukiza inagoma sijui kama ni mtandao uko down au la.
ikikubali irushe na nistue ninahamu nao niisome , na tume sijui kwa nini hawajaiweka kwenye website yao ! utafikiri tupo kwenye karne ya 47.
Hata hivyo nadhani mtu wa IT ya tume ya katiba hayupo makini haiwezekani kwenye website yao habari latest ni ya november 2012
 
Mkuu acha kuwapotosha watu! tulia soma vizuri rasimu! hao 15 ni wa shirikisho tu, bado wa Tanganyika! upo hapo?

Nashukura sana kwa comment yako isiyo na utafiti na yenye woga, mawazo mgando yasiyozingatia hitaji la wakati.

Zanzibar toka mwaka 1964 wanayo serikalia yao ambayo inaendesheka mpaka leo.
Tanzania bara(Tanganyika) inatakiwa iunde serikali yake kadiri ya uwezo na hitaji la kweli, siyo kupeana vyeo kwa hoja za kirafiki au kisiasa. Katika ulimwengu wa leo ambapo mambo mengi yanaendeshwa na private sector huhitaji kuwa na serikali kubwa.
Unless unataka kuwapa kazi ndugu na rafiki zako. Kwa Tanzania bara mawaziri 12 watosha kabisa. Idara katika wizara zepewe mamlaka makubwa ya kuamua mambo. This to me is the best solution.
 
Can we let zanzibar go please we cant afford to hve another gvt just for pleasing some people
 
Jamani naomba mwenye soft copy ya rasimu ya katiba mpya atututupie na sie tuisome.
mapemaaa tuanze kuitafakari.
 
 

wamejitahidi sana yani latest ni nov? Mie nilijua itakuwa ileile ya april 2012,hyo ya jana uzinduzi wa rasimu wataiweka mwaka 2015 mwanzoni.
 
Bwana!! bwana!!! hebu mtu mwenye soft copy haitupie humu tuione.

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…