nimesoma kwa makini rasimu ya katiba mpya kama itapita basi yawezekana ni kitanzi kikubwa kwa wanasiasa wengi na vyama vyao vya siasa,ni wazi kuwa ule utitili wa wabunge kwanza utakoma kwani hapo awali mtu yeyote hata kama ni muhuni lakini akiwa na uwezo mkubwa wa kuongea kwa sauti na hasira aliweza kuchaguliwa,lakini wengine waliweza kuteuliwa kushika ubunge kutokana na kuwa na mahusiano fulani mazuri na wanaoteua hali hii ilifanya wateuzi wengi kuteua hata watu wa hovyo kabisa.
lakini pia badhi ya vyama vimejaza wabunge wa viti maalumu kutoka maeneo fulani na kushindwa kuzingatia uwezo muhimu wa mhusika na hata uadilifu wake,kwa sasa majimbo yatakuwa machache na hata wabunge nao watapugua ambapo inatarajiwe kuwe na majimbo ishirini ya uchaguzi hali hii itafanya wapatikane wabunge wenye sifa stahiki hata kutoa rushwa haitawezekana mtu mwenye sifa stahiki na uadilifu uliotukuka ndiye atakayechaguliwa.
kwa mfano kutakuwa na wagombea wa urais watatu kwa maana ya tanzania zanzibar,tanzania bara na rais wa shirikisho,kwa vyama venye uhaba wa watu wenye uwezo wa kuongoza vitapata wakati mgumu sana najaribu kufikiri kutoka chadema nani atagombea zanzibar,nani atagombea bara,na nani atagombea urais wa shirikisho.hali hii pia yaweza kukikuta chama cha nccr mageuzi na vyama vingine pia vichanga.[/QUOTE
MMh mimi ninavyo kutazama katika ulichokiandika nikwamba wewe rasimu yenyewe hujaielewa na possibly wewe ni slow learner....Anyway hii rasimu inaelezea wabunge wa bunge la jamhuri ya muungano na sio Tanganyika wala Zanzibar