RASIMU ya Katiba Mpya Tanzania yazinduliwa

Kama jambo hujui ya nini kuandika au ni lazima kuandika thread maana sijawahi kusikia wilaya ya zanzibar mjini magharibi A au B na nyingine nyingi umekosea kuliko ulizopatia utafikiri ulilazimishwa kuziandika! Andika ulichonacho uhakika tu, maandiko hayafutiki unaweza ukaendelea kudharaulika daima kwa andishi la leo tu
 

Mkuu upeo wako uko vzur sana!
 
Ki ufupi tunachokitaka sasa ni Tanganyika yetu tu. Tuache kujifanya hatuoni gharama za kuendesha serikali tatu na hii hasa ni kwa faida ya nani? Wazanzibari kwa hali yoyote hawawezi kukubali serikali moja, sasa sisi waTanganyika tunajipendekeza nini. Hata mimi nimegundua kwamba kinachohitajika kufanyika sasa ni kupata katiba ya Tanganyika hata kabla ya hii ya Muungano. Bahati nzuri sehemu kubwa ya maoni yetu juu ya katiba ya Tanganyika tunayo tayari tunahitaji muda kidogo tu ili kupata maoni ambayo yatahusu uendeshaji wa serikali ya Tanganyika. Tumechoka kuendeshwa na waZanzibari!
 

Hahahahahahaa! Haya mkubwa, ila usitumie maneno makali sana bwana. Click hapo kwenye hayo maandishi, utakuta Kaskazini A, Kaskazini B
 
Hiko kipengele cha kulitaka kila Jimbo kuwakilishwa na Wabunge wawili kwa kweli kina walakini.Kichambueni kwa makini hiko kipengele mkikihusishanisha na mfumo wa kisiasa [Demokrasia] tunaoishi ndani yake na mtaniunga mkono kwamba hiki kipengele kimelazimishwa kuingizwa katika hii RASIMU ya KATIBA mpya kutokana na msukumo flani labda kutoka kwa WAHISANI au ndio hiyo RATIFICATION kutokana na maagizo ya Jumuiya za Kimataifa na za Kiukanda kama vile UN,AU,SADC & EAC kuhusu kuongeza idadi ya Wanawake kwenye Vyombo vya Kimaamuzi.Lakini namna tunavyo lishughulikia hili ndio tumechamka.
 
eti kila jimbo liwe na wabunge 2,mke na mume..hapo ni chenga tupu,bora wangesema kila mkoa kuwe na majimbo mawili lakin kila mbunge ambayo watu wagombee bila kuangalia jinsia...na huko zanj kungekuwa na wabunge hata watano tu wanatosha.. Serikali za majimbo ni very muhimu tatizo ubishi wa sisi WADANGANYIKA ooh sorry WATANGANYIKA.....
 

Kwa jinsi ilivyo hatuwezi kuwa na nchi moja na vijinchi viwili ndani yake. Ilipaswa kuwe na federal government na nchi moja (hizi nchi mbili lazima zife ile uweze kuwa na nchi moja, nje ya hapo tusipoteze muda tuuvunje muungano kila nchi iendelee na mambo yake), then tunakuwa na majimbo yenye serikali za majimbo (states)!! Hapa tungekuwa tunajadili namna ya kuunda katiba ya nchi moja, na jinsi tutakavyo pata hayo majimbo kwa mujibu ya hiyo katiba, katiba iyatamke na mipaka yake na jinsi yatavyoendeshwa kikatiba.

Ila kwa kuona sijui itaonekana wamekubali wazo la CHADEMA la sera ya majimbo hata hawakuliangalia hili. Hii aina ya serikali serikali tatu inayopendekezwa na TUME "ITS AN ABSOLUTE PATH TO BREAK THE UNION". Sasa kama tumechagua path tunayojua tunaenda kuvunja muungano kwanini tusiuvunjilie mbali sasa ili tusipoteze muda zaid.

NB: Ishu ya muungano ni moja ya issues zilizokuwa fiercly debated kabla na wakati wa mchakato. Tusiichukulie kirahisi rahisi.
 

Halafu utendaji utakuwaje endapo mmoja anatoka chama kimoja na mwingine chama kingine ilani gani itafuatwa? Imagine mmoja anatoka chadema na mwingine anatoka CCM vipi watafanya kazi vipi??
 

Sasa na wewe kama unazijua badala ya kuishia kukosoa tuu ungeziorodhesha kwa usahihi ili yeye na wengine tujifunze maana jukwaa hili pia tunaelimishana pia sio kukosoana tuu!!
 
Dr Mvungi alipokua anahojiwa bbc ameidhalilisha znz kwa kusema kisehemu kile chenye watu mil.1.6 hakiwezi kuwa sawa na sehemu yenye watu mil 45. Iv tujiulize dr Mvungi amezaliwa mwaka gani mpaka amejisahaulisha kuwa znz ilikua nchi huru? Kwaiyo hata kama ilikua na watu elfu 10 na imeungana na nchi nyengine thamani yake ni sawa. Hizi ndizo dharau wanazoziendleza vichogo kwa ZnZ yetu. Mmetubip lakini tuna vocha za kutosha tutawapigia.
 
Tatizo watanzania tunakuwa wepeso mno wa kupongeza na kulaumu bila kutafakati kwanza. Juzi Jaji Warioba alipotoa Muhtasari wa Rasimu ya Katiba mpya, wengi walishamngilia na kupongeza bila kuiona. Ukiisoma utagindua kuwa mazuti mengi yanayodifiwa ya muungano serkali tatu na mbgombea binafsi yanamezwa na mengi yadiyoridhisha. Kwa mfano madaraka ya Rais yamebaki vile vile na kuongezewa hadi kuingilia mhimi,li mwingine. Uhuru wa Mahakama umeminywa kinyume na maoni ya wengi wakiwemo majaji na jaji mkuu. Kinachonishangaza kwa hili ni kuwa Tume inaonbgozwa na majaji (akiwemo Jaji Mkuu mstaafu) na wanasheria waliobobea! Someni Rasimu kabla ya kuimba wimbo wa kusifu au kulalamika.
 
Kuna umuhimu wa kuwa na tume ya kuratibu mishahara ili kuondoa malalamiko kwa wafanyakazi wa umma.
 
WAJUMBE WA MABARAZA YA KATIBA NAOMBA CHONDECHONDE MFANYE KAZI KWA MAKINI NA WELEDI MKUBWA ILI TUPATE MOYO WA NCHI ULIO MZURI VINGINEVYO UCHAMBUZI WENU UKIJAA MAMBO BINAFSI UTUMIKAJ NAWATU FULANIFULANI AU VYAMA FULANIFULANI UNAWEZA KUZAA TAIFA LISILO NA MVUTO MBELE YETU NAMBELE YAWENZETU PIA. RAI YANGU NIKUWAOMBA UMAKINI MKUBWA UTAKAOSAIDIA KUPATA KATIBA NZURI YENYE KUTULETEA TZ MPYA KWELIKWELI. MAWAZO KUTOKA KTK MABARAZA YENU NDIO YATAKAYOTOA MWONGOZO KWANI HII HATUA NI MIHIMU SANA KUWAPA WANATUME KUONA NINI WATU WENGINE WAMEIPOKEA RASIMU HII YENYE SURA YAKUIZALISHA TZ MPYA YENYE MATAMANIO NA KILA MTZ ENDAPO YALE MAMBO YA MSINGI YALIYOPENDEKEZWA YATAENDLEA KUUNGWA MKONO NAWTU NA PIA YALE YENYE KUHITAJI MAREKEBISHO YATAFANYIWA MNAREKEBISHO VEMA NAKULETA MUSTAKABALI WA MAANA NAKUTATUA KERO ZAMDA MREFU ZA WATANZANIA. HASA KITU NACHOONA TUME ILITELEZA NIKUACHA TENA RAIS KUTEUA WAKUU WA WILAYA NA MIKOA,HAPA NAONA MATATIZO YAMEBAKI HILI BADO NI JANGA KUBWA SANA MANAKE HAWA MA DC's&RC's WANATUMIKA VIBAYA NA WATAWALA WAJUU NA KUFANYA WATEKELEZE MABO YAO KWA AMRI ZAWAKUBWA .SO NAOMBA MABARAZA MLIANGALIE HILO PIA,,PILI NI SULA LA KUMTEUA JAJI WA MAHAKAMA YA JUU BADO HALIJI AKILINI KWAMAB JAJI ALIYETEULIWA NA RAIS ENDAPO RAIS ANAWANIA KWA AWAMU YAPILI MANAKE ALIMTEUA HUYO JAJI AWAMU YA1, SASA HAIWEZEKANI HUYO JAJI AKAMHUKUMU MWAJIRI WAKE ENDAPO MATOKEO YA URAIS YATAPINGWA MAHAKAMANI,,HAPA NAONA MBUZI KAFUNGWA KAMBA NA KUUZWA NDANI YA GUNIA,HILI SIYO SWALA JEMA HATA KIDOGO BORA ACHAGULIWE NA JOPO LA MAJAJI NASIO ATEULIWE NA RAIS, HAYA YOTE BADO NIMAJANGA. CHAMBUENI RASIMU KWA UMAKINI MKUBWA MSIKUBALI KUBURUZWA NAMTU YEYOTE WALA CHAMA CHOCHOTE. KAZI HII INAHITAJI WELEDI NA STAHA YA HALI YAJUU,UMAKINI,UTULIVU WA KUFIKIRIA NASIO KUKURUPUKA. VOX POPULII VOX DEI-SAUTI YA WENGI NI SAUTI YA MUNGU.(MUNGU IBARIKI TANZANIA,MUNGU BARIKI MCHAKATO HUU UFANIKIWE KADIRI YA MPANGO WAKO-AMINA)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…