Nadhani mtoa hoja ameweka bayana maoni yake, na point yake ni nzito!
UKianagalia pendekezo la SERIKALI TATU, ambalo naamini watu wengi walikuwa wakilipigania, bahati mbaya hatukutazama mbali! Yes, NI GHARAMA KUENDESHA SERIKALI! Na kwa viongozi hawa wenye tamaa za kufuja mali ya nchi tutatokomea kwenye umasikini uliokithiri!!
- Kila serikali na bajeti yake! Kwa rasilimali gani tulizonazo? Serikali ya Tanganyika (Rais, mawaziri,Bunge watendaji, etc); Serikali ya Zanzibar (Rais, Mawaziri, Bunge, Watendaji n.k); Serikali ya Muungano/Shirikisho (Rais, mawaziri, bunge etc)!! Nchi masikini kama Tanzania na maraisi watatu, mawaziri kibao, wabunge kibao, watendaji.....Tutazihudumiaje hizi serikali? Tuna resources? Tunahitaji nchi yenye karibu asilimia kubwa ya wananchi ni "VIONGOZI"!!??
- TUFANYE NINI?- Kwanza tujadiliane, bil akuoneana haya tuamue JE TUNAHITAJI MUUNGANO AU LA? Mimi, kwa mtazamo wangu, nchi hii inahitaji ama SERIKALI MOJA (Muungano kamili) au SERIKALI MBILI....kila mtu ajue lwake