Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mkuu,Wapo wengi sana tena kuna wengine hata kura hawataki kupiga wanasema hivi vyama vya siasa wote wizi tu.
Tija ipo mkuu. Kwa sababu hizo katika zingine (za Tanganyika na Zanzibar) zitatungwa kwa kufuata/kuzingatia katiba hii ya muungano.Hii rasimu mbona tunaifurahia sana? Ngoma nzuri ni KATIBA ya TANGANYIKA a.k.a TANZANIA BARA. Hii ya MUUNGANO kama zitakuwepo serikali tatu haina tija sana. Tusubiri ya Tanganyika
Mkuu,
Unaweza kutupa mifano, maana jambo kama hili halina siri.
Yawezekana wewe ukamjua kuwa si mshabiki wa chama fulani, lakini mimi nikawa na ushahidi wa yeye kuegemea itikadi fulani.
Ni sawa kabisa uliyoandika, na hasa hili la Rushwa. Viongozi hawa ni wala Rushwa wakubwa na wanajiwekea kinga kila wanapopata mwanya. Suala la ruswha kwa makusudi hawajaliwekea mkakati kikatiba, ni makusudi yao na makosa makubwa sana kwa wananchi. Inatakiwa tulisimamie hili mpaka katiba iweke misingi thabiti ya kupambana na rushwa katika katiba, hasa ile ya wao viongozi. Kadili maendeleo yanapokuja ndivyo suala la rushwa linapokuwa kubwa na kuathiri maendeleo ya nchi na wananchi. Katiba hii ni ya miaka mingi ijayo so tukifanya makosa tu muda huu ndio tumekwisha kushney!HABARI WANA JF!
Jana tume ya mabadiliko ya katiba iliwasilisha kwa wananchi rasimu sifuri ya katiba ya Jamhuri ya shirikisho la Tanzania kwa kimombo The federal republic of Tanzania.
Kwa mujibu wa rasimu hii, binafsi naona mambo muhimu ambayo hayajatajwa au kwekwa kwa discusion.
1. Rais kutoshtakiwa-Ni makosa kumwacha rais huru kwa kumwekea kinga kisheria. Hii inapelekea wengi wawe wajeuri, wasiotii kuwa dola inatoka na inaanzia kwa wananchi. Ni wazi wataendelea kujificha chini ya kivuli cha kinga ya kutoshitakiwa. Ni heri iwe rais anaweza kushitakiwa ili hata wale wanoona Ikulu mi mahala pa kwenda kuficha maovu yao waone kuwa bado hawatakuwa wamekimbia mkono wa sheria. kama watu wote ni sawa kama ilivyoainishwa katika Rasimu sifuri ya katiba ya Jamhuri ya shirikisho la Tanzania, rais naye ashtakiwe kwa makosa aloyafanya kabla na hata baada ya kipindi chake cha urais mara inathibitika kuwa kulikuwa na matumizi mabaya ya ofisi au namna yoyote ya ukiukaji wa sheria za nchi na ndio maana anaapa kuilinda na kuitetea katiba husika.
2.Suala la wakuu wa wilaya na mikoa-natamani au naonelea kusiwe na nafasi hizi maana zimekuwa za kisiasa tu na hazitusaidii katika kusogeza gurudumu la maendeleo.badala yake kuwe na mameya na wakurugenzi tu. Mameya waendelee kuchaguliwa miongoni mwa madiwani katika halmashauri husika.
3.katiba kutamka tu kuwa Viongozi wasishiriki Rushwa, ufisadi, na kuwa na maslahi binafsi kabla ya yale ya taifa, haitoshi.haya hata sasa hivi yapo kwenye nyaraka mbali mbali za utendaji wa serikali yetu lakini hayafanyiwi kazi.
Kaitba iweke hukumu ikibidi ya kifo kwa wale watakaoshiriki maovu haya.
4.
hivi sasa, ni matangazo ya moja kwa moja (live) kutoka ukumbi wa mikutano wa karimjee yakirushwa na tbc1. Mgeni rasmi ni rais wa jamhuri ya muungano wa tanzania jakaya mrisho kikwete... Katiba mpya kwa tanzania yenye neema
tufuatilie
- KINGA YA RAIS
Tume baada ya kupitia maoni ya Wananchi, inapendekeza Rais abaki na kinga kama ilivyo sasa na anaweza kushitakiwa na Bunge kama ilivyo Katiba ya sasa.
Kila Jimbo la Uchaguzi litakuwa na Wabunge Wawili mmoja mwanamke na mwingine mwanamume.
Tume inapendekeza kwamba, Mbunge akifukuzwa na Chama cha Siasa abaki kuwa Mbunge lakini akihama Chama atapoteza Ubunge wake
. mfumo wa Serikali tatu. Yaani Serikali ya Shirikisho, Serikali ya Tanzania Bara na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
Hiyo Se3rikali ya Muungano itakuwa na kazi gani sasa, mapambo tuu au?