RASIMU ya Katiba Mpya Tanzania yazinduliwa

RASIMU ya Katiba Mpya Tanzania yazinduliwa

Wapo wengi sana tena kuna wengine hata kura hawataki kupiga wanasema hivi vyama vya siasa wote wizi tu.
 
Wapo wengi sana tena kuna wengine hata kura hawataki kupiga wanasema hivi vyama vya siasa wote wizi tu.
Mkuu,
Unaweza kutupa mifano, maana jambo kama hili halina siri.
Yawezekana wewe ukamjua kuwa si mshabiki wa chama fulani, lakini mimi nikawa na ushahidi wa yeye kuegemea itikadi fulani.
 
Hii rasimu mbona tunaifurahia sana? Ngoma nzuri ni KATIBA ya TANGANYIKA a.k.a TANZANIA BARA. Hii ya MUUNGANO kama zitakuwepo serikali tatu haina tija sana. Tusubiri ya Tanganyika
Tija ipo mkuu. Kwa sababu hizo katika zingine (za Tanganyika na Zanzibar) zitatungwa kwa kufuata/kuzingatia katiba hii ya muungano.
 
Mkuu,
Unaweza kutupa mifano, maana jambo kama hili halina siri.
Yawezekana wewe ukamjua kuwa si mshabiki wa chama fulani, lakini mimi nikawa na ushahidi wa yeye kuegemea itikadi fulani.

Nimeona kwa jamaa zangu wa karibu hawana habari kabisa na vyama vya siasa, labda nikuuliza wale ambao wanaharibu kura zao kwa makusudi unawaweka kwenye kundi gani?
 
Wana Jf,

Nime penda sana sehemu hii ya rasimu (nimeicopi na kupesti hapo chini). Hii itazuia wabunge kujipendelea kama tulivyo shudia hive karibuni shinikizo la wabunge wa kenya kutaka kujiongezea mishahara hadi Uhuru Kenyata alipoingilia kati. Kama kipengele hiki kitapitishwa itakuwa ni hatua kubwa sana katika kuhakikisha wabunge na watumishi wenye mamlaka kutojipendelea wao na kuwasahau wananchi wa chini waliowengi.

Je bunge la katiba litaipitisha? iatakuwaje kama bunge hilo halitapitisha kipengele hiki? Bunge maalum la katiba kwa muundo wake ni pamoja na wabunge wote waliopo sasa ambao ndio wengi na huu ni mwiba kwao hivyo kuwa na maslahi binafsi hata katika kuijadili hoja yenyewe. si vyema hoja hii ijadiliwe na wajumbe wengine ambao hawamo katika bunge hili la sasa?



SURA YA TATU​
MAADILI NA MIIKO YA UONGOZI NA UTUMISHI WA UMMA



(3) Itakuwa ni marufuku kwa Kiongozi yeyote wa Umma,kushiriki kuongeza au kwa namna yoyote ile, kuboresha maslahiyanayohusu wadhifa alionao, na endapo atashiriki, basi masharti hayomapya yataanza kutumika kwa Kiongozi atakayekuja baada ya yeyekuondoka au kumaliza muda wa kukaa madarakani.​
Nawakilisha.

 
HABARI WANA JF!

Jana tume ya mabadiliko ya katiba iliwasilisha kwa wananchi rasimu sifuri ya katiba ya Jamhuri ya shirikisho la Tanzania kwa kimombo The federal republic of Tanzania.

Kwa mujibu wa rasimu hii, binafsi naona mambo muhimu ambayo hayajatajwa au kwekwa kwa discusion.

1. Rais kutoshtakiwa-Ni makosa kumwacha rais huru kwa kumwekea kinga kisheria. Hii inapelekea wengi wawe wajeuri, wasiotii kuwa dola inatoka na inaanzia kwa wananchi. Ni wazi wataendelea kujificha chini ya kivuli cha kinga ya kutoshitakiwa. Ni heri iwe rais anaweza kushitakiwa ili hata wale wanoona Ikulu mi mahala pa kwenda kuficha maovu yao waone kuwa bado hawatakuwa wamekimbia mkono wa sheria. kama watu wote ni sawa kama ilivyoainishwa katika Rasimu sifuri ya katiba ya Jamhuri ya shirikisho la Tanzania, rais naye ashtakiwe kwa makosa aloyafanya kabla na hata baada ya kipindi chake cha urais mara inathibitika kuwa kulikuwa na matumizi mabaya ya ofisi au namna yoyote ya ukiukaji wa sheria za nchi na ndio maana anaapa kuilinda na kuitetea katiba husika.

2.Suala la wakuu wa wilaya na mikoa-natamani au naonelea kusiwe na nafasi hizi maana zimekuwa za kisiasa tu na hazitusaidii katika kusogeza gurudumu la maendeleo.badala yake kuwe na mameya na wakurugenzi tu. Mameya waendelee kuchaguliwa miongoni mwa madiwani katika halmashauri husika.

3.katiba kutamka tu kuwa Viongozi wasishiriki Rushwa, ufisadi, na kuwa na maslahi binafsi kabla ya yale ya taifa, haitoshi.haya hata sasa hivi yapo kwenye nyaraka mbali mbali za utendaji wa serikali yetu lakini hayafanyiwi kazi.
Kaitba iweke hukumu ikibidi ya kifo kwa wale watakaoshiriki maovu haya.

4.
Ni sawa kabisa uliyoandika, na hasa hili la Rushwa. Viongozi hawa ni wala Rushwa wakubwa na wanajiwekea kinga kila wanapopata mwanya. Suala la ruswha kwa makusudi hawajaliwekea mkakati kikatiba, ni makusudi yao na makosa makubwa sana kwa wananchi. Inatakiwa tulisimamie hili mpaka katiba iweke misingi thabiti ya kupambana na rushwa katika katiba, hasa ile ya wao viongozi. Kadili maendeleo yanapokuja ndivyo suala la rushwa linapokuwa kubwa na kuathiri maendeleo ya nchi na wananchi. Katiba hii ni ya miaka mingi ijayo so tukifanya makosa tu muda huu ndio tumekwisha kushney!
Nashangaa mtu kama Warioba kushindwa kuweka mkazo katika suala la kupambana na Rushwa katika Katiba ambalo ni muundo mbinu mkubwa wa umaskini ama maendeleo. Huwezi kuendelea bila kupambana na rushwa hata kidogo.
Tchao
 
hivi sasa, ni matangazo ya moja kwa moja (live) kutoka ukumbi wa mikutano wa karimjee yakirushwa na tbc1. Mgeni rasmi ni rais wa jamhuri ya muungano wa tanzania jakaya mrisho kikwete... Katiba mpya kwa tanzania yenye neema

tufuatilie

tunakushukuru sana mkuu
 
Hakuna cut-off point ya kusema beyond this huyu ana affiliation na chama Fulani au la zaidi ya kuwa na kadi ya chama hicho!
 
Hii Katiba ni nzuri lakini inajaza nafasi nyingi za ubunge bila sababu ya msingi (wabunge wawili kila jimbo ni gharama kwa taifa)! Pili imesahau swala la uwajibikaji (accountability), transparency kwenye mikataba ya ardhi na kilichoko chini na juu yake inayofanywa na serikali, kuvua madaraka viongozi wa umma waliopitishwa na Bunge kwa kulihusisha bunge, uhuru wa vyombo vya usalama katika kutenda majukumu yake, misingi ya elimu ya taifa, etc. Haya ni mambo ya msingi kuzingatiwa.
 
Eneo hili bado halija kaa sawa.Kushitakiwa kwa Raisi kupitia Bunge hakutoshi Katiba inatakiwa itamke wazi kuwa mara baada ya Bunge kuridhia mashitaka ya Raisi kwamba amefanya Kosa basi Raisi huyo anafutiwa kinga yake na Bunge na Mwendesha Mashitaka Mkuu wa JM Tanzania anachukua nafasi yake kumfikisha Mahakamani mara moja.

  • KINGA YA RAIS

Tume baada ya kupitia maoni ya Wananchi, inapendekeza Rais abaki na kinga kama ilivyo sasa na anaweza kushitakiwa na Bunge kama ilivyo Katiba ya sasa.


Hili nalo kunashida na halijakaa sawa.
Kuna haja ya kuweka na kuongeza maneno kadhaa.
(Mbunge kama ataacha kuwa Mwanachama wa Chama Chocote cha Siasa ataendelea kuwa Mbunge) hadi kipindi chake cha kuwa Mbunge kitakapoishia
)


Kila Jimbo la Uchaguzi litakuwa na Wabunge Wawili mmoja mwanamke na mwingine mwanamume.

Tume inapendekeza kwamba, Mbunge akifukuzwa na Chama cha Siasa abaki kuwa Mbunge lakini akihama Chama atapoteza Ubunge wake


Huku ni kuongezeana gharama.
Na pia kurudisha nyuma juhudi ya Kuelekea Shirikisho la Afrika Mashariki.



. mfumo wa Serikali tatu. Yaani Serikali ya Shirikisho, Serikali ya Tanzania Bara na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
 
Hii rasimu imemsahau spika nje. Haielezi atabanwa vipi na atawajibika vipi kinyume na ilivyo fanya kwa Raisi, Jaji na wazito wengine. Na baya zaidi imemuongezea kushiriki katika kumchagua mwenyekiti wa tume a uchaguzi
 
Tume ya Marekebisho ya Katiba imependekeza muundo wa shirikisho wenye serikali tatu (i) Tanganyika (ii) Zanzibar (iii) Muungano, ikimaanisha ongezeko la serikali nyingne zaid ambayo itaongeza matumizi kwa walipakodi na rasimali za taifa. Kama kweli tuna nia ya kuungana bas serikali tatu zenye kutuongezea mzigo wa bajeti na matumizi zina haja gani? Nashawishika kusema tume ya warioba imefikia namba mbili kabla ya kuanza na moja. Jambo la msingi na la kwanza tulitaka serikali iitishe kura ya maoni juu ya Muungano/Shirikisho wananchi waseme kwa ridhaa yao je wanataka Muungano/Shirikisho? Je wanataka Serikali tatu? Je Watanganyika na Wanzibari tuwe na tuwe taifa moja lenye wimbo mmoja, bendera moja, Rais mmoja na tuvunje mataifa ya tanganyika na zanzibar? Halaf baada ya hapo kile watakacho amua wananchi ndio kifanyiwe kaz na Tume. Kura ya shirikisho ikipita bas warioba atutengenezee katiba ya shirikisho kama alivyofanya lakini pia Watanzania wangeweza kupiga kura ya Tanganyika huru na Zanzibar huru bila shirikisho na hapa Warioba asingekua na tabu yoyote ya kufanya mikutano 1942 nchi nzima ila sisi watanganyika tungemuomba atutengenezee katiba yetu.
Tume ya warioba imewapa watanzania chakula wakati wana kiu ya maji na kiu hii ni kura ya maoni juu ya Muungano. Ndio maana baada ya uzinduzi wa rasimu Utanganyika na Uzanzibari umetawala vinywa vya watanzania na wala si utanzania chini ya shirikisho moja kwasababu weng wao wako kwenye namba moja ambayo ni kura ya maoni juu ya Muungano na warioba karukia namba mbili (rasimu ya shirikisho)
I remain to be corrected!
 
Pamoja na juhudi zote za CHADEMA na akina Lissu ndani na nje ya bunge hawakusikia! Kilichopo ni kuwa watumie data za bara kudraft ya bara na za nchi jirani ya Zanzibar wawape. What is Billal with all his wives doing, leave our country! Gooooo
 
Hiyo Se3rikali ya Muungano itakuwa na kazi gani sasa, mapambo tuu au?
 
musitoke mapovu ya mdomo ndugu zangu.mimi nilizani muna akili na maarifa kumbe hamna mpango wowote.pigania tanganyika wachana na muungano.
 
Step imerukwa kwa mujibu wa Hadidu zipi za Rejea au kwa mujibu wa Sheria ipi?
 
Kwa maoni yangu naona kuwa uko sahihi kwamba watanzania wanahitajika kwanza kuulizwa wanahitaji mfumo gani wa muungano maeneo gani yawe ktk muungano na baada ya hapo kwa kufikirika kuwa mfumo unaotakiwa ni serikali tatu, iundwe serikali ya mpito ambapo katika kipindi hicho watanganyika wataandika katiba yao na Wazanzibar vivyo hivyo na pia ile ya shirikisho yenye mambo yatakayokubalika kuwa ya muungano na mwisho tutakwenda kwenye uchaguzi. Rasimu hii naiona kuwa ime-cover mambo yote yaliyoko kwenye mfumo wa serikali mbili isipokuwa tu kwamba inapendekeza kupunguza mambo ya muungano kuwa 7 badala ya 22. Vinginevo watuambie kuwa hayo yote ni ya serikali ya Tanganyika ukiondoa hayo mambo saba as Zanzibar ina katiba yake tayari and baada ya katiba kuandikwa kila kitu kitakuwa cha Tanganyika isipokuwa hayo mambo saba ya muungano na baadaye itaundwa serikali ya shirikisho ikiwa na hayo mambo saba na mfumo wa kutuunganisha katika muungano mpya.
 
Tume Huru tunataka sio ya Uteuzi wa rais, ujinga wa Bunge linathibitisha hatutaki, maana kule nako kuna ile ya wanaoafiki ndiyooooo hata km sauti zao ni chache inapita tuu
 
Back
Top Bottom