RASIMU ya Katiba Mpya Tanzania yazinduliwa

RASIMU ya Katiba Mpya Tanzania yazinduliwa

Step imerukwa kwa mujibu wa Hadidu zipi za Rejea au kwa mujibu wa Sheria ipi?

Hapa ukiuliza hadidu za rejea na Sheria ipi itakua ni siasa za bungeni nikuulize swali ndugu yangu huu Muungano tulionao uliuchagua kwa kura ipi? na kama sio wewe ni mtanzania gani aliyeshirikishwa kuuanzisha?
 
Kwanini asiruke step ,Zanzibar hadidu rejea za katiba zimechanwa hadharini baada kushtukia swala la muuungano lisijadiliwe. Poor Warioba in no uncertain term ameambiwa aache "wazimu" wake. Ndio Zanzibar hio baba, zanzibar ya wana mapinduzi.
 
Suala la Muungano wa nchi hizi mbili lina asili yake ambayo kimsingi kwa nyakati za sasa relevance yake inastahili kufanyiwa tafakariya kina.Tatizo tlilo nalo hapa nchini ni utaratibu upi wa kutumia kupata maoni ambayo yatakuwa yanawakilisha mapendezeo halisi ya Watanzania. Kura ya maoni nyakati Fulani huyumbishwa sana na "political party influences" na kiwango cha uelewa cha wanaopiga kura hizo. Anagalia vizuri mazingira ya Tanzania na tuna mifano mizuri toka nchi za jirani pia.Hii Tume ya Katiba kufikia mapendekezo haya ya the so called "serikali ya shirikisho' yanaashiria pia kuwa hata wajumbe wake wana mitazamo isiyo adequately objective, bali kumekuwa na dalili za kutaka kuwaridhisha baadhi ya wanasiasa. Tuwe wakweli: ukiwauliza Watanzania walio wengi watakuambia muungano hauna faida yoyote kwetu zaidi ya nyimbo na sherehe ili kuionyesha dunia kwamba tuna umoja sana/historia yetu moja/tunapendana na upuuzi wa aiana hiyo!
Tusaidiane kupata kwanaza namna ya kuweka wazi mitazamo ya Watz dhidi ya muungano ambayo haina unafiki wala shinikizo la kisiasa.
 
"Jaji Warioba alisema Tume imependekeza kuwapo kwa majimbo 25 ya uchaguzi kwa Tanzania Bara na 20 kwa Zanzibar ambayo kila moja litakuwa na wabunge wawili, mwanamke na mwanamume. Kwa mujibu wa rasimu hiyo, majimbo hayo ni mikoa 25 ya Tanzania Bara na wilaya 10 za Zanzibar. Kwa maana hiyo, Bunge la Muungano litakuwa dogo lenye wabunge 75."

1.Uwakili ukoje hapa?? Zanzibar ambayo kwa ukubwa na wingi wa watu iwe na uwakilishi sawa na tanganyika??? Kwanza mikoa ya bara ambayo kwa zanziba ni Jimbo tu iwe na uwakili almost sawa na Jimbo la Zanzibar?? Kwa hili bado tutarudi kwenye kero za muungano tu.

2. Wabunge wawili kila Jimbo-kwanza wa nini? Tunamfurahisha nani?? kama tiba inatoa haki sawa kwa kila raia, watu wote wagombee na wachaguliwe si kwa misingi ya Jinsia zao. Tukifikia hapa hata kwenye kazi na tutataka kuwe na watu wawili kwenye kila position, MME na MKE. kwanza hawa wawili watafanya kazi kwa misingi ipi kama si kushindanisha ushawishi tu na malumbano.

Nawasilisha
 
Naungana na mtoa mada juu ya hiyo hoja,hiki ndicho akina Lissu walikipigia kelee;ni kuhusu nani aliandaa hadidu rejea ambazo tume ya Warioba walikuwa wakitumia ktk kukusanya maoni ya kuandaa rasimu hii.
 
wewe hata hujui kinachoendelea, unakimbilia kuanzisha thred uchwara hapa...znz majimbo matano bara majimbo 20 jumla 25....acha kukurupuka
 
Mkuu Mossad007, Mbona hiyo rasimu ni matokeo ya maoni ya wananchi, ni step gani imerukwa? Wananchi wametoa maoni yanaoonyesha kuwa wanataka serikali tatu. Kura ya maoni itapigwa kwa ajili ya kuihubali au kuikataa katiba, na bila shaka wale wale wasioridhika na katiba kwa ajili ya kipengele hicho cha muungano wataikataa. tuipe tume nafasi imalize kazi!
 
"Jaji Warioba alisema Tume imependekeza kuwapo kwa majimbo 25 ya uchaguzi kwa Tanzania Bara na 20 kwa Zanzibar ambayo kila moja litakuwa na wabunge wawili, mwanamke na mwanamume. Kwa mujibu wa rasimu hiyo, majimbo hayo ni mikoa 25 ya Tanzania Bara na wilaya 10 za Zanzibar. Kwa maana hiyo, Bunge la Muungano litakuwa dogo lenye wabunge 75."

1.Uwakili ukoje hapa?? Zanzibar ambayo kwa ukubwa na wingi wa watu iwe na uwakilishi sawa na tanganyika??? Kwanza mikoa ya bara ambayo kwa zanziba ni Jimbo tu iwe na uwakili almost sawa na Jimbo la Zanzibar?? Kwa hili bado tutarudi kwenye kero za muungano tu.

2. Wabunge wawili kila Jimbo-kwanza wa nini? Tunamfurahisha nani?? kama tiba inatoa haki sawa kwa kila raia, watu wote wagombee na wachaguliwe si kwa misingi ya Jinsia zao. Tukifikia hapa hata kwenye kazi na tutataka kuwe na watu wawili kwenye kila position, MME na MKE. kwanza hawa wawili watafanya kazi kwa misingi ipi kama si kushindanisha ushawishi tu na malumbano.

Nawasilisha

Hapo kwenye Bold naomba pasomeke majimbo 10 kwa Zanzibar.
 
wewe hata hujui kinachoendelea, unakimbilia kuanzisha thred uchwara hapa...znz majimbo matano bara majimbo 20 jumla 25....acha kukurupuka

Hapo Juu kwenye " " nimenukuu toka mwananchi gazeti, rasimu ninayo ila sijaisoma yote. Kama kuna makosa ya Gazeti liloandika basi nafuatilia. Ila usilete uliberali wako hapa wa kuita threas uchwara. Jadili hoja.
 
Majimbo ya Zanzibar yatakuwa wilaya, nazo ziko kumi kama ifuatavyo:
1. Wilaya ya Wete
2. Wilaya ya Micheweni
3. Wilaya ya Chake Chake
4. Wilaya ya Mkoani
5. Wilaya ya Zanzibar Kati
6. Wilaya ya Zanzibar Kusini
7. Wilaya ya Zanzibar Mjini Magharibi "A"
8. Wilaya ya Zanzibar Mjini Kaskazini "B"
9. Zanzibar Mjini
10. Wilaya ya Zanzibar Mjini Magharibi
Pamoja na kuwa wabunge kutoka Zanzibar watawakilisha wananchi wachache sana, mimi sioni ubaya wowote hapo. Mbunge kutoka mkoa wa Dar es Salaam atakuwa anawakilisha wananchi milioni tano, wakati Mbunge kutoka wete atawakilisha watu chini ya 50,000, au kutoka maeneo kama Kusini Zanzibar ambapo kuna watu chini ya laki moja.
 
Mkuu Mossad007, Mbona hiyo rasimu ni matokeo ya maoni ya wananchi, ni step gani imerukwa? Wananchi wametoa maoni yanaoonyesha kuwa wanataka serikali tatu. Kura ya maoni itapigwa kwa ajili ya kuihubali au kuikataa katiba, na bila shaka wale wale wasioridhika na katiba kwa ajili ya kipengele hicho cha muungano wataikataa. tuipe tume nafasi imalize kazi!

Msengapavi ninachosema mimi ni kua kwanza ilibidi tuuhoji Muungano kwa kura ya maoni hapo tungepata jibu zur iwapo tuwe na katiba ya shirikisho au kila nchi ( Tanganyika na Zanzibar ) iwe huru, au tubaki na serikali mbili kama ilivyo sasa, ni kweli maoni haya yametoka kwa wananchi lakini Muungano lilikua swala zito la kwanza lililohitaj ufumbuz km majority ya Wanzanzibar wangesema hawautak na sisi watanganyika tukasema hivyo bas shirikisho linatoka wap? Tumefumbwa macho sana kwamba ishu ya muungano haikua na uzito katika maoni na haikupaswa kuchanganywa na mchakato wa mabadiliko ya katiba kwasababu ilikua na uzito wa kipekee na ndio maana tunai support ipigiwe kura ya maoni lakini umeshawah sikia badiliko jingne katika katiba linashutishwa kupigiwa kura ya maoni zaid ya Muungano?
 
Ratio ya uwakilishi bado si nzuri kwa ustawi wa muungano. 1:50,000 zanzibar kwa 1:400,000-5,000,000 kwa bara.
 
"Jaji Warioba alisema Tume imependekeza kuwapo kwa majimbo 25 ya uchaguzi kwa Tanzania Bara na 20 kwa Zanzibar ambayo kila moja litakuwa na wabunge wawili, mwanamke na mwanamume. Kwa mujibu wa rasimu hiyo, majimbo hayo ni mikoa 25 ya Tanzania Bara na wilaya 10 za Zanzibar. Kwa maana hiyo, Bunge la Muungano litakuwa dogo lenye wabunge 75."

1.Uwakili ukoje hapa?? Zanzibar ambayo kwa ukubwa na wingi wa watu iwe na uwakilishi sawa na tanganyika??? Kwanza mikoa ya bara ambayo kwa zanziba ni Jimbo tu iwe na uwakili almost sawa na Jimbo la Zanzibar?? Kwa hili bado tutarudi kwenye kero za muungano tu.

2. Wabunge wawili kila Jimbo-kwanza wa nini? Tunamfurahisha nani?? kama tiba inatoa haki sawa kwa kila raia, watu wote wagombee na wachaguliwe si kwa misingi ya Jinsia zao. Tukifikia hapa hata kwenye kazi na tutataka kuwe na watu wawili kwenye kila position, MME na MKE. kwanza hawa wawili watafanya kazi kwa misingi ipi kama si kushindanisha ushawishi tu na malumbano.

Nawasilisha

katika makilaza wa Tanganyika wewe ndio mkubwa wao, mbona hamjaiambia Burundi na Rwanda kwenye ubunge wa Afrika Mashariki wana wabunge wengi katika bunge na eneo lao la ardhi dogo, kunya anye kuku akinya bata kahara?, we are equal partner katima muungano no matter Zanzibar tuna eneo dogo la ardhi, actual tunataka idadi sawa ya wabunge 50/50 na ndio maoni tunayopeleka katika mabaraza ya katiba Zanzibar, acheni porojo watanganyika mna kibarua kipevu kuaanda katika yenu ya Tanganyika kabla ya 2015. fanyeni ya muhimu kwenu acheneni na sisi, wazanzibari hawajapoteza asili ni watanganyika.
 
Nadhani mtoa hoja ameweka bayana maoni yake, na point yake ni nzito!

UKianagalia pendekezo la SERIKALI TATU, ambalo naamini watu wengi walikuwa wakilipigania, bahati mbaya hatukutazama mbali! Yes, NI GHARAMA KUENDESHA SERIKALI! Na kwa viongozi hawa wenye tamaa za kufuja mali ya nchi tutatokomea kwenye umasikini uliokithiri!!

  1. Kila serikali na bajeti yake! Kwa rasilimali gani tulizonazo? Serikali ya Tanganyika (Rais, mawaziri,Bunge watendaji, etc); Serikali ya Zanzibar (Rais, Mawaziri, Bunge, Watendaji n.k); Serikali ya Muungano/Shirikisho (Rais, mawaziri, bunge etc)!! Nchi masikini kama Tanzania na maraisi watatu, mawaziri kibao, wabunge kibao, watendaji.....Tutazihudumiaje hizi serikali? Tuna resources? Tunahitaji nchi yenye karibu asilimia kubwa ya wananchi ni "VIONGOZI"!!??
  2. TUFANYE NINI?- Kwanza tujadiliane, bil akuoneana haya tuamue JE TUNAHITAJI MUUNGANO AU LA? Mimi, kwa mtazamo wangu, nchi hii inahitaji ama SERIKALI MOJA (Muungano kamili) au SERIKALI MBILI....kila mtu ajue lwake
 
Back
Top Bottom