"Jaji Warioba alisema Tume imependekeza kuwapo kwa majimbo 25 ya uchaguzi kwa Tanzania Bara na 20 kwa Zanzibar ambayo kila moja litakuwa na wabunge wawili, mwanamke na mwanamume. Kwa mujibu wa rasimu hiyo, majimbo hayo ni mikoa 25 ya Tanzania Bara na wilaya 10 za Zanzibar. Kwa maana hiyo, Bunge la Muungano litakuwa dogo lenye wabunge 75."
1.Uwakili ukoje hapa?? Zanzibar ambayo kwa ukubwa na wingi wa watu iwe na uwakilishi sawa na tanganyika??? Kwanza mikoa ya bara ambayo kwa zanziba ni Jimbo tu iwe na uwakili almost sawa na Jimbo la Zanzibar?? Kwa hili bado tutarudi kwenye kero za muungano tu.
2. Wabunge wawili kila Jimbo-kwanza wa nini? Tunamfurahisha nani?? kama tiba inatoa haki sawa kwa kila raia, watu wote wagombee na wachaguliwe si kwa misingi ya Jinsia zao. Tukifikia hapa hata kwenye kazi na tutataka kuwe na watu wawili kwenye kila position, MME na MKE. kwanza hawa wawili watafanya kazi kwa misingi ipi kama si kushindanisha ushawishi tu na malumbano.
Nawasilisha