Kwa muhtasari tu mpaka hapa wamejitahidi sana, sijasikia kuhusu mahakama ya kadhi au OIC coz haya ni mambo ya kupingwa haraka sana.
Katika muhtasari huu mambo ambayo napendekeza tuyapinge ni;
1. Wabunge awe mmoja tu kila jimbo na si wawili kama walivyosema. Coz hii itaongeza ukubwa wa bunge na ghalama za kuliendesha zitakuwa kubwa sana na watanzania kuendelea kuwa masikini.
2. Mawaziri wasiteuliwe moja kwa moja na Rais bali watume maombi ya kuomba nafasi hizo na wasiwe wanasiasa au wasiwe na vyama vyao ila waende kama watanzania, na wafanyiwe open interview watakaoshinda ndo rais awatangaze na bunge lithibitishe.
3. Muungano uwe wa serikali tatu yaani JMT, Zanzibar na Tanzania bara au Tanganyika. Na rais wa JMT ndo awe na mamlaka ya nchi.
Kwa sasa nimeyaona haya naomba kuwasilisha