RASIMU ya Katiba Mpya Tanzania yazinduliwa

RASIMU ya Katiba Mpya Tanzania yazinduliwa

Aisee wewe kumbe ni Genius ehee!! katiba ya Tanganyika iandikwe kwa ushirikiano na Wazanzibar? au hujui tume ya Warioba ina wajumbe kutoka Zanzibar? tushirikishe akili kabla ya kucomment na tujifunze ku- appliciate pale kazi nzuri inapofanyika.

Kwa hiyo mwaka 2015 tutachagua serikali ya shirikisho peke yake? Je, serikali ya Tanzania bara itachaguliwa kwa utaratibu upi, uliowekwa na nani?
Hebu nisaidie hapo mkuu...
 
Kifo cha ccm kimewadia,sasa rais kushtakiwa na bunge,viti maalum hakuna, pamoja na mengi mazuri kali ni kuwa mbunge akifariki,mrithi atatoka chama alichokuwa aliyefariki,hapa kuna tatizo kwani ni sawa na kuamini wananchi walichagua chama na si mtu kwa sifa na uwezo wake,pia ni kuamin anayepewa nafasi anakubalika na pia ni kuwanyima haki za msingi watu wanaopenda na wenye nia ya kuleta maendeleo. My intake: Tusitishwe na gharama za uchaguzi kwa kumteua mtu asiyefaa.

Hapo nafikiri labda hujapaelewa vizuri, mimi nafikiri wana hoja ya maana kwamba, kama Mbunge akifariki basi hakuna haja ya Uchaguzi ili kuokoa gharama, basi mrithi wake atatoka Chama kile kile tu, hivyo ina maana Chama chake watateua tu, badala ya uchaguzi kufanyika, kwa maana nyingine tunapaswa tuchague Sera za Chama na SIO mtu!
 
Kuna hatari naiona hapa! Kama tukikubaliana na katiba hii maana yake itabidi bara tuanze mchakato wa katiba yetu! Hapo ndio naona kale kampango ka JK kuongezewa muda! Maana there is no way tutaingia uchaguzi bila katiba
 
Tumsikie Bilal, mbona Jk kachimba kwenye hili? Something fishing ......

969038_4123397462243_788457331_n.jpg
 
Tume ya uchaguzi , majkumu yawe ni pamoja na ya msajili wa vyama vya siasa, no more Tendwa,
wajumbe wa tume sifa kuteuliwa ktk tume ziwekwe kwenye katiba nani mwenye sifa

Mkuu Huyo Jamaa utastaajabu ukisikia kaibukia kwenye Tume ya Uchaguzi
 
Safi hii,sasa wale wanaowarubuni Naniino kwa ubunge wa vitu maalum vp?
Tume imepitisha serikali tatu yaani Tanganyika,zanziber na muungano. Rais kapunguziwa mamlaka,mambo ya muungano yamepungua toka 22 na kubaki saba tu.viti maalum wanawake vimefutwa na Wabunge wa kuteuliwa na rais wamepunguzwa toka kumi hadi 5 na watakaoteuliwa na Rais wanapaswa wawe Walemavu tuuuu. Tume huru ya katiba
 
Hapo kwenye red tuipinge hii idea kwa nguvu zote, nani ataingia gharama kuwalipa lundo lote la wabunge hawa comedy show? idadi ya wabunge wa sasa inatosha sana.
Kabisa Mkuu, tena sio wabunge wa sasa wanatosha tu bali wapunguzwe kwa sababu tafiti zinabainisha wazi wabunge ambao ni productive ni wachache mno; so wapungue japo kwa 25%
 
mambo yatakuwa tofauti kama tulivyozoea katika katiba ya zamani, tusiikasirikie tume, tutoe hoja za kuboresha.
tuongozwe na maelekezo aliyotoa baba wa taifa wakati nchi imepata uhuru, aliposema toa hoja usipige kelele, ie argue dont shout!!!!
 
Hata mi najiuliza. Na hizo serikali mbili (Tanganyika na Zanzibar), zitakuwa na mamlaka gani kimataifa?

mambo ya kimataifa ni suala la muungano kwa hiyo rais wa muungani ndiye atakuwa mhusika mkuu.
 
good......zikiwepo katiba tatu Tanganyika yetu itarudi tujimwaye mwaye na kutakuwa hakuna mivutano ya kuchafua hali ya hewa kwa maslahi ya watu fulani fulani.Hiyo katiba ya Tanganyika tutaunda tume nyingine itafune pesa kuiandaa
 
Katiba ya Muungano inaweza kuwa safi lakini za nchi husika, viz. Zanzibar naTanganyika zikawa na mambo yaleyale yaliyokuwa kwenye katiba mfu tunayopigania, kama itabidi kuwa na katiba hizo kabla ya uchaguzi wa 2015. La sivyo hoja ya 2017 inagonga kengele kichwani!
 
Tume hii ni ya kuunda Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania sio ya kuunda katiba ya Tanganyika kwani kwa sasa Tanganyika haipo, au hata ingekuwepo wasingeunda rasimu ya katiba ya Tanganyika kwani hawana mamlaka hayo kisheria. Kama rasimu hii waliyopendekeza itapita kwenye mabaraza ya katiba na bunge maalum la katiba na suala la shirikisho likabaki kwenye rasimu, kisha wananchi wakaipitisha kuwa katiba hapo ndipo serikali ya Tanganyika itakuwa imeanzishwa rasmi. Hivyo mchakato wa kutengeneza katiba ya Tanganyika utaanza. Kwa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ambao wana katiba yao wanachoweza kufanya ni kufanya marekebisho na kuona ni kwa namna gani katiba yao itaendana na Katiba ya shirikisho lililoanzishwa.
 
mkuu nimekushauri ufiche aibu yako, tulia tumia akili usitumie uji kuandika..hapa tunazungumzia katiba sio sheria

We tukana tu, lakini baadaye utajiona mjinga wenyewe... Zanzibar wana katiba yao. Ya shirikisho ndio hiyo tunaitengeneza. Ya Tanzania bara iko wapi, itatengenezwa lini?, na nani? na 2015 Watanzania bara watachagua raisi wao, wabunge wao na viongozi wengine kwa kutumia katiba gani. Huwezi kutengeneza sheria kama huna sheria mama (katiba)...
 
rasimu hii sasa rasmi imezinduliwa na jaji warioba mwenyekiti wa tume ya katiba amemkabidhi makam wa rais rasimu za katiba mpya ambapo zingine zitagawaiwa kwa viongozi na wananchi
 
madaraka ya rais yameachwa juu mno,.tume ya uchaguzi bado sio huru, kinga ya rais bado ipo!!

Kwa nini madaraka ya Raisi yapunguzwe, mimi kama Mtanzania sitaki yapunguzwe na nina haki, hivyo ni sawa tu kwa Upande wangu!
 
Back
Top Bottom