RASIMU ya Katiba Mpya Tanzania yazinduliwa

RASIMU ya Katiba Mpya Tanzania yazinduliwa

Hii itakuwa demokrasia ya Tanzania, tutakipinga hiki kipengele hadi kibadirishwe kabla ya kura ya NDIYO NA HAPANA

Tutakipinga, wewe nani? Mbona unawasemea watu wote wa TZ?

Sio kweli ukiangalia kwa undani zaidi utaona kwamba, kama ikiwa hivyo ina maana wananchi watakikataa Chama kwenye Uchaguzi unaofuata, hivyo ili Chama kiweze kushinda ni lazima kihakikishe kinakuja na Sera nzuri na zinazokubalika na pia kuweka Mgombea ambaye anaweza kuzisimamia, chama ambacho kitaweka Wasanii basi Wananchi watakikataa Uchaguzi Mkuu!

Hivyo ni mfumo mzuri sana tu, hasa huko mbeleni.Hizo gharama za Uchaguzi ni kubwa sana tunaweza kuzifanyia mambo mengine!

Jamani, kuna chama chenye sera nzuri zaidi ya hiki kinachotawala sasa???? Nini kinafanyika, mambo hovyooooo kabisa lol
 
Kifo cha ccm kimewadia,sasa rais kushtakiwa na bunge,viti maalum hakuna, pamoja na mengi mazuri kali ni kuwa mbunge akifariki,mrithi atatoka chama alichokuwa aliyefariki,hapa kuna tatizo kwani ni sawa na kuamini wananchi walichagua chama na si mtu kwa sifa na uwezo wake,pia ni kuamin anayepewa nafasi anakubalika na pia ni kuwanyima haki za msingi watu wanaopenda na wenye nia ya kuleta maendeleo. My intake: Tusitishwe na gharama za uchaguzi kwa kumteua mtu asiyefaa.

Kama ni kweli basi balaa tupu.....nakumbuka wakati wa kupokea mawazo ya wananchi nilishauri likitokea hili basi aliyeshika nafasi ya pili awe mbunge kama watakuwa hawakupishana kwa zaidi ya asilimia 10% ya kura zilizopigwa vinginevyo ifanyike by election
 
Mbona mengi yanayochambuliwa ni uchaguzi pamoja na tume? Ina maana rasimu ya katiba nzima imejaa uchaguzi?
 
Ndio maana inaitwa rasimu siyo final inapelekwa kwenye mabaraza ya Katiba kujadiliwa, ila ndo hivyo hayo mabaraza 98% ni makanda wa CCM! tegemea vyeo vya ukuu wa mikoa na wilaya kuibuka with flying clours!
Hata kama wangekuwa 100% hii rasimu ya katiba itawanyonga wenyewe.
 
Wabunge wa sasa ni wajumbe pia katika bunge la katiba. Ninaamini kabisa wataipinga hoja ya kuwa na bunge lenye wabunge 75, kwani wengi wao bado hawajalipa mikopo ya hela walizotumia kwenye kampeni
 
Tuko ngoja nikusaidie kidogo, angalia mbali usiangalie karibu hawa Wazanzibar wameshatusumbuwa muda mrefu sana, sasa shortcut ya kuvunja muungano tumeshaipata, CCM haijawahi hata siku moja kuwaza serikali 3 wait n see hii ni zaidi ya movie.

Mkuu naelewa. Ninachoona mimi ni kuwa huu mchakato wa katiba umefanywa ovyo kabisa ili 2015 ama tusiwe na uchaguzi, au tutumie ile ile katiba ya zamani.
Hebu jiulize; Mwaka 2014 hii katiba ya shirikisho ikikamilika, je 2015 Watanganyika tutapiga kura kuchagua viongozi wetu kwa kutumia sheria ipi? Tutatumia katiba ipi? Hiyo katiba itatengenezwa lini? Tume ya kutengeneza hiyo katiba itaundwa na nani? Endapo "Tanganyika" hatutafanya uchaguzi 2015, Je tutachagua raisi wa shirikisho na wa Zanzibar? Baada ya hapo Tanganyika itakuwa inaongozwa na nani (Kumbuka serikali ya shrikisho itahusika na mambo 7 tu)?
 
Je kama Mbunge alitoka upande wa Mgombea binafsi ambaye pia nimesikia Rasimu inapendekeza awepo mara baada ya kupitishwa kuwa Katiba ni nini kitafanyika?.
 
Hakuna kitu kama Tanganyika Dunia hii, zaidi ya jina la Ziwa!

Alichokuwa anatamka Maalim uwanja wa kibanda maiti jana hukusikia?
Magamba ndiyo wanasema hakuna Tanganyika, na ndiyo wanaong'ang'ania Muungano! Hushangai Zanzibar wenyewe hawautaki?
 
Ndio maana inaitwa rasimu siyo final inapelekwa kwenye mabaraza ya Katiba kujadiliwa, ila ndo hivyo hayo mabaraza 98% ni makanda wa CCM! tegemea vyeo vya ukuu wa mikoa na wilaya kuibuka with flying clours!

Kama hayo mabaraza ya kata yatarudisha takataka hizo zinazoitwa RCs, DCs, tutahamasishwa wananchi kupiga kura ya HAPANA.

Hawa watu (RCs & DCs) is a wastage of our meagre resources
 
Jamani, kuna chama chenye sera nzuri zaidi ya hiki kinachotawala sasa???? Nini kinafanyika, mambo hovyooooo kabisa lol

Sasa hilo ni jukumu letu Wananchi kukikataa kama kinafanya mambo hovyo, na kutafuta mbadala wake kama upo!
Vinginevyo mimi kwangu ni jambo zuri kwani hakuna kitu kinatumaliza kama gharama zisizokuwa na ulazima, hivyo kama tumeweza kupata jinsi ya kuzipunguza basi yote Heri mimi kwangu!
 
Mkuu naelewa. Ninachoona mimi ni kuwa huu mchakato wa katiba umefanywa ovyo kabisa ili 2015 ama tusiwe na uchaguzi, au tutumie ile ile katiba ya zamani.
Hebu jiulize; Mwaka 2014 hii katiba ya shirikisho ikikamilika, je 2015 Watanganyika tutapiga kura kuchagua viongozi wetu kwa kutumia sheria ipi? Tutatumia katiba ipi? Hiyo katiba itatengenezwa lini? Tume ya kutengeneza hiyo katiba itaundwa na nani? Endapo "Tanganyika" hatutafanya uchaguzi 2015, Je tutachagua raisi wa shirikisho na wa Zanzibar? Baada ya hapo Tanganyika itakuwa inaongozwa na nani (Kumbuka serikali ya shrikisho itahusika na mambo 7 tu)?
Wewe unapendekeza iweje.
 
Serikali tatu safi maoni yangu huenda yakawaimplemented,
wabunge 20, 50, 5 walemavu sio mbaya. Kiukweli naona mambo yatakuwa safi sana.
 
Ndio maana inaitwa rasimu siyo final inapelekwa kwenye mabaraza ya Katiba kujadiliwa, ila ndo hivyo hayo mabaraza 98% ni makanda wa CCM! tegemea vyeo vya ukuu wa mikoa na wilaya kuibuka with flying clours!

Wakuu mliokabithiwa nakala.... TUWEKEE hapa jf... tuone kwa macho yetu....
 
Je kama Mbunge alitoka upande wa Mgombea binafsi ambaye pia nimesikia Rasimu inapendekeza awepo mara baada ya kupitishwa kuwa Katiba ni nini kitafanyika?.

Atarithiwa na mkewe(Joke) Hii ni moja ya changamoto mkuu
 
Back
Top Bottom