RASIMU ya Katiba Mpya Tanzania yazinduliwa

RASIMU ya Katiba Mpya Tanzania yazinduliwa

madaraka ya rais tume ya warioba imeyaachia mabaraza ya katiba na bunge la katiba nao wamalizie kwani warioba na tume wake ni wateule wa rais ulitegemea wasukumie shimoni boss wao.for sure wanajua kwenye mabaraza halitapita lazima madaraka yapunguzwe, wapo kina LISSU watamalizia match wakati wa substitution.

Mpaka hapo bro. tume ya warioba kodi zetu zimejibu
 
Hapo ni ujinga mtupu. Jimbo kuwa na wabunge wawili kwa maslahi ya nani na kuwakilisha nani? na raisi anakuwa na wabunge kuwakillisha nini?. inamaana tutakuwa na wbunge zaidi ya 700 na gharama za kufuga wadudu hao zitalipwa nani.Wanawake wanaweza na wamekwisha jiwezesha waingie kupambana.Lazima mihimili hii iwe tofauti.

bunge la muungano litakuwa na wabunge 75 tu. baraza la wawakilishi litakuwa kama kawa na tanganyika itakuwa na wabunge wake ambao watakuwa na bunge lao kama lilivyo baraza la wawakilishi zenji
 
Uko wa raisi uwe miaka 8 na Wabunge miaka 12. Cant wait kuona Mkwe re anaondoka tumsahau
 
Mimi naona kama ni kamtego Fulani kwa Wazenj(sensitizing them from their longtime claim).Hebu ngoja tusubiri wao Watasema nini.
 
Naomba atakaepata softcopy atuwekee hapa jamvini ili tupate muda wa kuipitia vizuri
 
Hapo nafikiri labda hujapaelewa vizuri, mimi nafikiri wana hoja ya maana kwamba, kama Mbunge akifariki basi hakuna haja ya Uchaguzi ili kuokoa gharama, basi mrithi wake atatoka Chama kile kile tu, hivyo ina maana Chama chake watateua tu, badala ya uchaguzi kufanyika, kwa maana nyingine tunapaswa tuchague Sera za Chama na SIO mtu!

Kwa nini asipewe aliefuatia kwa wingi wa kura!
 
Kwa nini madaraka ya Raisi yapunguzwe, mimi kama Mtanzania sitaki yapunguzwe na nina haki, hivyo ni sawa tu kwa Upande wangu!
mkuu unaneemeka na huu mfumo nini? nivizuri yapunguzwe ili watu wawe makini na kazi maana ukijua kwamba ukifanya fyongo watu hawatacheka na wewe hali itakuwa nzuri.
 
Kama ni kweli basi balaa tupu.....nakumbuka wakati wa kupokea mawazo ya wananchi nilishauri likitokea hili basi aliyeshika nafasi ya pili awe mbunge kama watakuwa hawakupishana kwa zaidi ya asilimia 10% ya kura zilizopigwa vinginevyo ifanyike by election

Life at risk....
 
Sasa mfumo wa hiyo serikali ya muungano ni upi na hizo nyingine pia? au ndio kuunda tume ingine tena?
 
Ninaomba nichukue fursa hii kumpongeza joseph sinde warioba kwa kumaliza kukamilisha rasimu ya katiba na hasa kututengenezea katiba isiyolenga kutubagua watanzania kwa misingi mbalimbali mf. ukabila,udini nk. Japokuwa kunamapungufu ya hapa na pale lakini ninaimani mabaraza ya katiba yatafanya kazi yake vizuri na kurekebisha mapungufu hayo. HONGERA SANA WARIOBA
Umempongeza kwa lipi? kipi umekifurahia kwenye rasmu ya katiba ? weka vitu,siyo unapongeza kumalizika kazi bila kujua/kueleza imekamalizikaje!!! je kama ameweka kwenye rasm yake pendekezo kwa mfano,mtanzania haruhusiwi kumiliki ardhi,hapo unampongeza kwa lipi?
 
Hapo kwenye red tuipinge hii idea kwa nguvu zote, nani ataingia gharama kuwalipa lundo lote la wabunge hawa comedy show? idadi ya wabunge wa sasa inatosha sana.

Ni kweli, hapo itakuwa ni kutafutiana mapatna wa kukaa viti virefu tu baada ya kupiga porojo pale mjengoni. BIG NO!!
 
Yaani wamependekeza serikali 3
Ya shirikisho...
Ya Tanzania bara...
Ya Zanzibar...

Alafu wakajiamulia kutengeneza katiba ya serikali moja (shirikisho) peke yake!!! Sasa hizo mbili wamemuachia nani?!!! Ebo!
wewe ni meshakwambia huna kitu kichwani, unaishia kukurupuka tu. watu wenye akili timamu hukaa na kufikiri kisha kupambanua mambo hawakurupuki
 
Wewe ni CCM mambo ya Chadema yanakuwashia nini? naona hii rasimu imewachoma na msumari wa mwisho ipatikane tume huru ili muunde kambi imara ya upinzani, hakuna namna ya CCM kurudi madarakani kwa mfumo huu, Si Tanganyika wala si Zanzibar na wala si Federal Government

Katiba yenyewe ikapatikana kwa mapendekezo haya nitakuwa mwenye furaha sana kwani mimi sio mchumia tumbo bali napenda kuona kila mtanzania anapata haki sawa.
 
Wenye akili timamu wamemuelewa sana warioba namnukuu:

"Kuna wale waliotaka kuwepo na serikali ya mkataba, walikuwa ni wengi sana na walikuwa na hoja zenye nguvu mno, lakini miongoni mwa hadidu za rejea tulizopewa ni kutokuvunja muungano na ikumbukwe kuwa ili kuwa na serikali ya mkataba itakubidi uvunje kwanza muungano............utengeneze serikali washirika kisha ...........mkataba.........., hivyo basi ..................Serikali tatu"

Tafsiri yake ni kuwa kuwa na serikali washirika i.e tanganyika, zanzibar na shirikisho ni one step toward kuuvunja muungano.
 
hii rasimu naweza pata copy yake yote nkakeshe leo nkiisoma kabla sijapotoshwa kesho na magazeti?
sem2708 hasa gazeti la Uhuru na Jambo Leo yanahaririwa ofisi ndogo Lumumba, Dar es salaam na Mhariri Mtendaji Napelila
 
Last edited by a moderator:
Yaani wamependekeza serikali 3
Ya shirikisho...
Ya Tanzania bara...
Ya Zanzibar...

Alafu wakajiamulia kutengeneza katiba ya serikali moja (shirikisho) peke yake!!! Sasa hizo mbili wamemuachia nani?!!! Ebo!
warioba alikuwa anazindua rasimu ya katiba ya nchi sio ya mikoa wala ya majimbo..wala hakuzindua sheria.amezindua katiba ya jamhuri ya muungano wa tanzania
 
mkuu unaneemeka na huu mfumo nini? nivizuri yapunguzwe ili watu wawe makini na kazi maana ukijua kwamba ukifanya fyongo watu hawatacheka na wewe hali itakuwa nzuri.

Sio kweli, Kenya wamefanya hayo, umesikia sasa hivi Wabunge wamegoma wanataka walipwe milioni 20 kwa Mwezi vinginevyo patakuwa hapatoshi, kitu ambacho Katiba yao Mpya inayosifika kwa Ubora imekataza, imepanga kila kitu mpaka ukomo wa mishahara ya Wabunge, lkn wapi nachomaanisha ni kwamba tatizo sio Madaraka ya Raisi, kufikiri hivyo ni kujidanganya, tatizo ni SISI, nakuhakikishia hata leo wakiondoa madaraka ya Raisi kabisa hakuna litakalobadilika!
 
-tume ya jaji Warioba yapendekeza sekali tatu.
-serkali ya zanzibar, ya tanganyika na ya muungano.
mambo ya muungani ni 7 ambayo ni:
1)katiba ya jamhuri ya muugano wa tanzaia
2)sarafu na benki kuu
3)mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa
4)ushuru
5)ulinzi na usalama
6)usajili wa vyama vya siasa
7)uraiya na uhamiaji

Maoni yangu.

Mambo saba yaliyopendekezwa kuwa ya muungano, ni sawa na kumi namoja,mambo hayo ndio ambayo wazanzibari kwao ndo kero kubwa za muungano.

Uraia na uhamiaji (ni mambo mawili)
Ulinzi na usalama (ni mambo mawili)
Mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa( ni mambo mawili0
sarafu na bank kuu ( haya ni mambo mawili)

Kwa mapendekekezo hayo ni mambo kumi na moja yalio pendekezwa, bado Warioba hajaondoa kero za muungano, tunarudi kule kule ambako tunakotoka, tunataka Mamlaka kamili ya zanzibar itakayo jiamulia mambo yake ya nje na ya ndani, hata tanganyika vile vile.

Rasimu hii ipo wezekano wazanzibari kuikata asilimia 66 wanaotaka mkataba, haitapita,

haya ni mawazo yako siyo ya wazanzibar subiri wazanzibar watoe maoni yao.
 
Back
Top Bottom