RASIMU ya Katiba Mpya Tanzania yazinduliwa

RASIMU ya Katiba Mpya Tanzania yazinduliwa

Wanaj
yafuatayo ni baadhi ya maoni ya watanzania waliyotegemea kuyaona katika rasimu ya katiba mpya lakini giza;
  • kutambuliwa kwa kiswahili kama lugha ya taifa
  • mikataba yote kujadiliwa bungeni

ongeza na yako tuone

Sikumsikia Warioba akiitaja Tanganyika kabisa bali Tanzania Bara (sijui ni nchi gani hii).....maoni yangu hata moja halikuchukuliwa
 
Mkuu, endapo 2014 hii katiba itakamilika na kutambua uwepo wa Tanganyika, je watanganyika watachagua viongozi wao 2015? Watatumia katiba gani? Hiyo katiba itatengenezwa na nani? Je, itakuwa sawa kufanya uchaguzi wa shirikisho kisha wa Tanganyika baadae?
Mkuu hebu fikiria hapo...

Acha kuwa na maono mafupi sana mkuu, kuwa flexible. Uchaguzi unaweza kuahirishwa hata kwa miaka miwili mbele kwa manufaa ya kizazi hki na kijacho. Mawazo yako ni mafupi mno kwani yameishia 2015. Kumbuka maslahi ya taifa ni zaidi ya uchaguzi wa 2015 unaowaza wewe ndugu. Elimu yako form four nini?
 
Oh, you mean hana ruhusa ya kuongeza wala kupunguza bila kuomba ruhusa bungeni? Maybe that.
but kusema leo hii constitution i-fix a number of ministry in the constitution itakua ngumu (IMO)

Ningependa kuona asiwe na power ya kuongeza wala kupunguza bila bunge kuruhusu
sina uhakika but under Bush walipotaka kuunda wizara ya internal security
kila kitu kilijadiliwa bungeni...sina tu uhakika now ilikuwaje...
 
mbona sioni elimu ,afya utalii,mikataba,rasilimali za taifa....?
 
Marekani Rais hawezi ongeza wizara au punguza bila kuomba ruhusa ya bunge
au kuvunja na kuunga wizara fulani

Tanzania right now as we speak kuna waziri asie na wizara maalum..

hapo ndo tunafanya makosa siyo kila kitu tuige twaweza kuwa na mfumo wetu pekee duniani kuwa na mawaziri 15 then rais mweyewe ndo ajue namna ya kucheza na wizara
 
sijapenda jimbo la uchaguzi kuwa na wabunge 2,nafasi za wakuu wa mikoa na wilaya zingeondolewa wakabaki wakurugenzi tu,nafasi za makatibu wakuu na wasaidizi zipatikane kwa watu kupeleka cv zao,majaji nao wasipendekezwe na tume ya utumishi wa mahakama ila waombe na kuhojiwa na bunge na kupitishwa.
 
Ningependa kuona asiwe na power ya kuongeza wala kupunguza bila bunge kuruhusu
sina uhakika but under Bush walipotaka kuunda wizara ya internal security
kila kitu kilijadiliwa bungeni...sina tu uhakika now ilikuwaje...

Ni Department of Homeland Security na iliundwa November 25, 2002 kutokana na yale mashambulizi ya 9-11.

  • Introduced in the House as H.R. 5005 by Dick Armey on June 24, 2002
  • Passed the House of Representatives on November 19th, 2002 (295-132)
  • Passed the Senate on November 19th, 2002 (90-9)
  • Signed into law by President George W. Bush on November 25th, 2002
 
Naona sasa tunaelekea kupata KATIBA. Heko Jaji Waryoba na wajumbe wengine wa Tume ya KAtiba kwa kazi mujarabu. Hii ni Rasmu ya katiba ni nzuri sana.
 
Binafsi kwa haraka haraka mapendekezo ya tume ninayaunga mkono isipokuwa madaraka ya raisi lazima yafyekwe.
Sikubaliani na pendekezo la kiongozi wa mhimili wa serikali kumteua kiongozi mkuu wa muhimili wa mahakama. Raisi afanye mambo mengine kama kuteua mawaziri na manaibu wao lakini si kumteua jaji mkuu.
Nakubaliana nao kwamba raisi ateue wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama lakini sikubaliani na pendekezo la raisi kuteua wabunge watano hata kama ni walemavu, hilo ninalipinga.
Uwekwe utaratibu wa kisheria kuwawezesha walemavu wenyewe kuchagua wawakilishi wao wenyewe, vingineyo walemavu watakosa wawakilishi wanaojua shida zao watakaotetea maslahi yao.
pSasahivi kuna mbunge mmoja wa ccm Margreth Mkanga anatajwa kwamba anawakilisha walemavu lakini sijawahi kumsikia akiwasemea walemavu hata mara moja.

Mkuu Mwita

Nakubaliana na point zako hapo juu. Niwaombe pia jf members tutumie nafasi tuliyonayo (access ya mtandao) kutoa maoni yetu-

this is a unique chance for us. Tusikubaliane kwanjia yoyote ile mwingiliano wa mihimili hii: Mahakama na Rais. Pls pls.....ili lisiwepo vinginevyo haki haitawezakutendeka tanzania hii.
 
Hili swala katika jimbo wagombea awe wanamke na mwanaume ?

usijali ishu ni 50/50. By the way tanzania bara yatakuwepo majimbo 25 tu (wabunge 50 jumla) huku visiwani ni majimbo 10 (wabunge 20) na watano wanobaki wakuteuliwa na raisi ambao watakuwa ni walemuvu tu.
 
Mkuu, endapo 2014 hii katiba itakamilika na kutambua uwepo wa Tanganyika, je watanganyika watachagua viongozi wao 2015? Watatumia katiba gani? Hiyo katiba itatengenezwa na nani? Je, itakuwa sawa kufanya uchaguzi wa shirikisho kisha wa Tanganyika baadae?
Mkuu hebu fikiria hapo...

Mbona Jaji Waryoba ametaja Serikali ya Tanzania Bara na si kuitaja kinagaubaga Serikali ya Tanganyika? Nadhani inatakiwa iwe serikali ya Jamhuri ya Tanganyika
 
Ni Department of Homeland Security na iliundwa November 25, 2002 kutokana na yale mashambulizi ya 9-11.

  • Introduced in the House as H.R. 5005 by Dick Armey on June 24, 2002
  • Passed the House of Representatives on November 19th, 2002 (295-132)
  • Passed the Senate on November 19th, 2002 (90-9)
  • Signed into law by President George W. Bush on November 25th, 2002

thank you
 
Wanaj
yafuatayo ni baadhi ya maoni ya watanzania waliyotegemea kuyaona katika rasimu ya katiba mpya lakini giza;
  • kutambuliwa kwa kiswahili kama lugha ya taifa

ongeza na yako tuone

Katiba yetu ya sasa haina sehemu inayoelezea tunu za Taifa (National Values). Wananchi wengi walitoa maoni kwamba Katiba itaje Tunu za Taifa. Tume imependekeza Tunu zifuatazo zitajwe ndani ya Katiba. Tunu hizo ni;- Utu, Uzalendo, Uadilifu, Umoja, Uwazi, Uwajibikaji na Lugha yetu ya taifa ya Kiswahili.
 
Wanaj
yafuatayo ni baadhi ya maoni ya watanzania waliyotegemea kuyaona katika rasimu ya katiba mpya lakini giza;
  • kutambuliwa kwa kiswahili kama lugha ya taifa
  • mikataba yote kujadiliwa bungeni

ongeza na yako tuone

Tuwe makini na mada zetu jamani.
kiswahili ni tunu ya taifa. hapa kuna mataifa mawili kila moja ndio litapanga lugha ipi iwe ta taifa. au ulitaka waseme kiswahili angali wewe wanao umempeleke english media kutokana na dunia ya sasa. kila serikali itaamua.
suala la mikataba unataka wajadili nini angali madini,ardhi mali asili sio ya muungano. serikali za kila nchi ndio zitashugulikia hayo.
 
Rasimu inasema:
"Mawaziri wasizidi 15,I guess hiyo ndio itayoreflect idadi ya wizara"

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums

Kiwango cha juu kabisa cha safari za raisi nje ya nchi kwa mwaka:yell:
 
Back
Top Bottom