RASIMU ya Katiba Mpya Tanzania yazinduliwa

RASIMU ya Katiba Mpya Tanzania yazinduliwa

hapo ndo tunafanya makosa siyo kila kitu tuige twaweza kuwa na mfumo wetu pekee duniani kuwa na mawaziri 15 then rais mweyewe ndo ajue namna ya kucheza na wizara


acheze na wizara kwa pesa ya nani?
we hujui ni mabilioni yanatumika kuvunja na kuunga wizara ovyo ovyo?
 
Yapo mengi sana

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Wanaj
yafuatayo ni baadhi ya maoni ya watanzania waliyotegemea kuyaona katika rasimu ya katiba mpya lakini giza;
  • kutambuliwa kwa kiswahili kama lugha ya taifa
  • mikataba yote kujadiliwa bungeni

ongeza na yako tuone

Serikari Tatu ni Gharama Kwa walipa kodi huku serikari ya majimbo ikiwa ni serikari nafuu isiyo na gharama kubwa wajifunze toka USA huko majimbo yanaongozwa ma Magavana na hakuna kero za Muungano huko aina ya muungano wetu ni aina ya muungano ambao umejaa mapungufu mengi hivyo ili kuepuka Malalamishi ya wazenji ni lazima kero zao ziondoshwe
 
Pia kuna suala la kuwa na spika wa bunge aliyechaguliwa, labda na wananchi asiye na mafungamano na chama chochote cha siasa kati ya vilivyo bungeni.

Inapendekezwa Spika na Naibu Spika wasitokane na Wabunge na wasiwe Viongozi wa vyama vya Siasa.
 
kufutwa kwa vyeo vya wakuu wa wilaya, wakuu wa mikoa, & regional adminstrative secretary
 
Wanaj
yafuatayo ni baadhi ya maoni ya watanzania waliyotegemea kuyaona katika rasimu ya katiba mpya lakini giza;
  • kutambuliwa kwa kiswahili kama lugha ya taifa
  • mikataba yote kujadiliwa bungeni

ongeza na yako tuone


Jitahidi kusoma kwanza umalize na uache haraka mkuu,hayo uliyoandika hapo juu nimeyaona kwenye TUNU ZA TAIFA kama ifuatavyo:
Nanukuu
"TUNU ZA TAIFA

Katiba yetu ya sasa haina sehemu inayoelezea tunu za Taifa (National Values). Wananchi wengi walitoa maoni kwamba Katiba itaje Tunu za Taifa. Tume imependekeza Tunu zifuatazo zitajwe ndani ya Katiba. Tunu hizo ni;- Utu, Uzalendo, Uadilifu, Umoja, Uwazi, Uwajibikaji na Lugha yetu ya taifa ya Kiswahili."

Sasa hayo ya kujadiliwa bungeni yatakuwa ndani ya sheria za madini na mambo ya tamaduni maana yatakuwa yameishatamkwa kwenye katiba yetu
~seen today~
 
Chezea zenji wewe bila utawala wa Magavana Itakuwa ngumu kuzitokomeza kero za muungano
 
Acha kuwa na maono mafupi sana mkuu, kuwa flexible. Uchaguzi unaweza kuahirishwa hata kwa miaka miwili mbele kwa manufaa ya kizazi hki na kijacho. Mawazo yako ni mafupi mno kwani yameishia 2015. Kumbuka maslahi ya taifa ni zaidi ya uchaguzi wa 2015 unaowaza wewe ndugu. Elimu yako form four nini?

Hii ndio akili yenu magamba ya kutaka Kikwete aongezewe muda wa kukaa madarakani hadi 2017 kwa kisingizio cha kutengeneza katiba ya Tanganyika. Kikwete ni raisi wa Tanzania hatuwezi kuruhusu aiongoze Tanganyika kutokea mlango wa uani.
 
Wabunge wa sasa ni wajumbe pia katika bunge la katiba. Ninaamini kabisa wataipinga hoja ya kuwa na bunge lenye wabunge 75, kwani wengi wao bado hawajalipa mikopo ya hela walizotumia kwenye kampeni

Kuna uwezekano huo, maana wabunge wote Chadema, Ccm , cuf nk ni waroho wa mishahara na posho za ubunge. Hoja ya wabunge 75 inatishia nafasi za wengi wao, so wengi ktk wabunge watapinga
 
DPP kuwa na madaraka makubwa hadi ya kuingilia uhulu wa mahakama, kuzuia dhamana za watu kwa masilahi ya watu fulani.
 
wasn't the president himself supposed to be present in this event?
 
Naona dalili za Kikwete kuongezewa muda wa miaka miwili au zaidi ili kujipanga na katiba mpya.
 
Wabunge hao mkuu ni wabunge wa jamhuri ya muungano si wabunge waTANGAYIKA
Kuna uwezekano huo, maana wabunge wote Chadema, Ccm , cuf nk ni waroho wa mishahara na posho za ubunge. Hoja ya wabunge 75 inatishia nafasi za wengi wao, so wengi ktk wabunge watapinga
 
mbona sioni elimu ,afya utalii,mikataba,rasilimali za taifa....?

Mambo ya msingi sana haya. Matumaini yangu ni kwamba mambo haya yatakuwa yametajwa ndani ya katiba tuendelee kuipitia taratibu bila shaka yatakuwemo.

Kilichosomwa na Jaji Warioba leo ni kama executive summary lakini mambo mengi yako ndani ya rasimu yenyewe. Ibara za katiba 240 ni dhahiri kuwa itakuwa imesheheni mambo mengi sana.
 
Kuna uwezekano huo, maana wabunge wote Chadema, Ccm , cuf nk ni waroho wa mishahara na posho za ubunge. Hoja ya wabunge 75 inatishia nafasi za wengi wao, so wengi ktk wabunge watapinga
Wabunge watakaopingwa twawashauri wagombee uwakilishi kwenye bunge la Tanzania Bara....
 
Naona kuna msamiati mpya. Washirika wa Muungano. Kina nani hawa?
Halafu hiki kipengele kimekaaje?
Tume pia, inapendekeza haki mpya ziingizwe kwenye Katiba ikiwa ni pamoja na haki ya wafanyakazi, , haki ya mtoto, haki za Watu wenye Ulemavu, Haki za Wanawake, Haki za Wazee, Haki za Makundi Madogo katika Jamii, Haki ya Elimu na Kujifunza, Haki ya kupata habari, Haki na uhuru wa habari na vyombo vya habari na kadhalika.
 
Kitendo cha kutomshtaki Rais akimaliza muda wake kimenikera sana,pamoja na swala la chief justice kuteuliwa na Rais,Hii rasimu bado sana
 
Back
Top Bottom