RASIMU ya Katiba Mpya Tanzania yazinduliwa

RASIMU ya Katiba Mpya Tanzania yazinduliwa

kwa hali fulani inaridhisha ila bado rais kapewa majukumu makubwa sana,pia swala la majimbo wameliagalia kisiasa zaidh na sio kiuhalisia,ngoja tuendelee kuitathimini
 
Kuhusu vitu maalum. Kuna wasiwasi kiwa idadi ya wabunge wanawake ikapungua sana bungeni. Kwa sababu hiyo ninashauri hao waendelee lakini wateuliwe kwa umakini mkubwa ili kuhakikisha kweli wanaleta tija bungeni na siyo ngonjera na mashindano ya kuvaa tunayoona sasa. Waweze kujenga hoja na wawe na elimu ya zaidi ya
Stashahada.

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
kwa mtazamo wangu mie naona angalau imegusa mambo ya msingi kwa hiyo naiunga mkono ingawa bado nahitaji sana uchambuzi wa wadau wengi wenye elimu ya sheria na katiba. toeni michango ya kujenga wapendwa ili mtusaidie sis wengine tulio na uelewa mdogo kuhusu sheria na katiba
nawaombeni sana wasomi wetu na wanafunzi wa vyuo vya sheria mtusaidie kuichambua ili tujue cha kuamua kama ni kupigia kura au hapana
 
ukiangalia kiundani uyasemayo ni sahihi kabisa mie nadhani suala hapa ni kukomaa tu kuwa na serikali moja zenji yao na Bara yao usanii wa kuongeza muda hautakuwa na nafasi
 
yanatokana na maoni ya Katibu Mkuu Kiongozi ambaye alitaka madaraka ya Rais yasipunguzwe.
 
mzee tupatupa hebu iweke hapa jamvini tuidadavue. nna hamu nayo kweli kweli ukitilia maanani nilienguliwa ujumbe wa baraza la katiba la kata yangu ingawa wenye nchi walinichagua.
 
Hili la rasimu ya katiba kutowagusa wakuu wa wilaya na mikoa nalo si zuri hivi vyeo ni vya kundoka kabisa....ndo maana ya rasimu lakini...? bado inatakiwa ipigwe brush kidogo...?
 
Rais na wabunge wana kikomo cha mamlaka yao kwa mujibu wa katiba. Wanapewa mamlaka hayo na wananchi kupitia sanduku la kura. Kupiga kura si matakwa ya Rais, Bunge, Mahakama wala Tume ya Uchaguzi, ni matakwa ya Katiba.

Katiba mpya inawezekana kutumika 2015 kama nia ya dhati ipo. Ucheleweshaji wowote ni mipango ya kidhalimu. Tumeona haya katika nchi nyingine.

a) Uchaguzi wa Madiwani uwe sawa na Rais na Wabunge December 2015.
b) Rasimu ya mwisho ya Katibu baada ya wadau kushiriki iwe ni December 2013.
c) Kura ya Maoni iwe June 2014. Ikishindwa Kura nyingine ya maoni iwe December 2014.
 
Nanukuu:

Kila Jimbo la Uchaguzi litakuwa na Wabunge Wawili mmoja mwanamke na mwingine mwanamume.
Yaani hawa wapuuzi tumewalipa mapesa yote hayo halafu wanatuletea upuuzi huu. Wabunge wawili jimboni wanafanya kazi gani? Shenzi zao.
 
Mikataba kujadiliwa bungeni ni suala la kuwekewa kipao mbele kwa maslahi ya taifa maana hii mikataba inayosainiwa kisiri inatugarimu vizazi hadi vizazi

Mie ndio kitu nilikua ninasikilizia,mwanzo mwisho nimetoka kapa.
 
Rasimu hii bado mambo mengine yanahitajiufafanuzi, pamoja na viti maalumu kuondolewa lakini inapendekezwa kila jimbo litakuwa na wabunge wawili wa kike na kiume, sasa wanapatikanaje? au kila mgombea atakuwa na mgombea mwenza? wenye rasimu watfafanulie.

halafu pia najiuliza kwenye majukumu hawataingiliana???
Au mmoja atakuwa tu mwakilishi wa wanawake?(hapa kabisaa ndo sielewi)
 
hapa sijapapenda.. ningependa Tanganjika irudi... na si Tanzania Bara..Tume ilifikia uamuzi wa kupendekeza mfumo wa Serikali tatu. Yaani Serikali ya Shirikisho, Serikali ya Tanzania Bara na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
 
Nchi iliyo laaniwa imelaaniwa tu. Yaani pamoja na pesa zote zile walizo lipwa hawa watu, hapa ndio upeo wao wa kutoka na Rasimu ya namna hii? Kwamba hata maoni ya waTanganyika haya kutiliwa maanani? Kulikuwa na haja gani kuzunguka na kuhoji wananchi na hatima yake ni kutoka na madudud ya namna hii?

Ingekuwa afadhali wangejifungia ndani ya ukumbi wa mikutano na kuiandika bila kujidai eti hayo ndiyo maoni ya waTanganyika.

Naamini wameanza na mguu mbaya.
 
Rasimu hii bado mambo mengine yanahitajiufafanuzi, pamoja na viti maalumu kuondolewa lakini inapendekezwa kila jimbo litakuwa na wabunge wawili wa kike na kiume, sasa wanapatikanaje? au kila mgombea atakuwa na mgombea mwenza? wenye rasimu watfafanulie.
Ukienda kupiga kura unachagua mbunge mwanaume alafu unachagua mbunge mwanamke .....among best candidates
 
Washindwa wa nne ni watanganyika,mpaka sasa hawana identity yao.
 
Hahaha, Wewe EMT vipi bana,

There's no hurry in Tanzania. Take walking.

Umenifanya nikakimbilia haraka thread yako nikijua umeipata kumbe ndugu yangu umekuwa frustrated kama mimi.
 
  • Thanks
Reactions: EMT
Back
Top Bottom