RASIMU ya Katiba Mpya Tanzania yazinduliwa

RASIMU ya Katiba Mpya Tanzania yazinduliwa

hii itakuwa nzuri kwanini tuwabebe tuuuuu na kuleta mlundikano wa vilaza bungeni??tunataka wanawake wenye uwezo kama akina Prof Tibaijuka, anna Kilango, halima Mdee....etc sio kwasababu ana matiti na anavaa sketi basi apewe free ride kuenjoy kiyoyozi na kodi zetu bungeni......
 
Tusijadili kama hii ni katiba jamani. It's just a first draft. Bado kuna room kubwa ya kuirekebisa na hususan KUICHAKACHUA kupitia mabaraza ya katiba na bunge la katiba na kujikuta maslahi ya manyang'au yanalindwa na kuimarishwa. Mkumbuke nafasi ya wengi iliyobaki ni kuipigia kura katiba na kama mjuavyo voters wengi wa Tanzania vote without making a rational choice!
 
nimesoma kwa makini rasimu ya katiba mpya kama itapita basi yawezekana ni kitanzi kikubwa kwa wanasiasa wengi na vyama vyao vya siasa,ni wazi kuwa ule utitili wa wabunge kwanza utakoma kwani hapo awali mtu yeyote hata kama ni muhuni lakini akiwa na uwezo mkubwa wa kuongea kwa sauti na hasira aliweza kuchaguliwa,lakini wengine waliweza kuteuliwa kushika ubunge kutokana na kuwa na mahusiano fulani mazuri na wanaoteua hali hii ilifanya wateuzi wengi kuteua hata watu wa hovyo kabisa.

lakini pia badhi ya vyama vimejaza wabunge wa viti maalumu kutoka maeneo fulani na kushindwa kuzingatia uwezo muhimu wa mhusika na hata uadilifu wake,kwa sasa majimbo yatakuwa machache na hata wabunge nao watapugua ambapo inatarajiwe kuwe na majimbo ishirini ya uchaguzi hali hii itafanya wapatikane wabunge wenye sifa stahiki hata kutoa rushwa haitawezekana mtu mwenye sifa stahiki na uadilifu uliotukuka ndiye atakayechaguliwa.

kwa mfano kutakuwa na wagombea wa urais watatu kwa maana ya tanzania zanzibar,tanzania bara na rais wa shirikisho,kwa vyama venye uhaba wa watu wenye uwezo wa kuongoza vitapata wakati mgumu sana najaribu kufikiri kutoka chadema nani atagombea zanzibar,nani atagombea bara,na nani atagombea urais wa shirikisho.hali hii pia yaweza kukikuta chama cha nccr mageuzi na vyama vingine pia vichanga.
 
Rasimu ya katiba iliyozinduliwa jana inatupa matumaini bali binafsi naona serikali tatu ni mzigo kwa wananchi. Serikali ya muunganoitakua na wabunge 75 na mawaziri wasiopungua 15. Lakini serikali hii itategemea mapato yake kutoka serikali ya Tanzania Bara na Zanzibar. Watakaoumia zaidi kuibeba ni Tanzania Bara. Sielewi kabisa bunge na mawaziri wa muungano watakua wanafanya nini wakati kila upande wa hizo serikali mbili kuna wabunge na mawaziri wao. Naona pengine tuchague tu rais wa muungano halafu kila upande kuwe na waziri mkuu mtendaji atakaechaguliwa na wabunge wa serikali hiyo. Kwa staili hiyo tutaepuka mzigo mkubwa.
 
Kinga ya rais na issue ya wakuu wa wilaya na mikoa viangaliwe upya. yaliyomo kwenye rasimu si matarajio ya watanzania
 
Mkuu kivipi kwani wananchi wanaziongoza serikali au unataka kusema nini.
 
hapa cha msingi ni Let Zanzibar go, hakuna cha serikali tatu hilo ndio suluhisho...
 
Pale uliposema wahuni wenye kuongea kwa sauti ya juu ulikuwa unamaanisha sugu,lema na msigwa????? Funguka plz
 
Wanapopendekeza Serikali tatu, hii Katiba itakuwa kwa ajili ya Serikali shirikisho au serikali zote tatu? Na kama ni ya Serikali ya shirikisho Zanzibar tayari wana katiba yao ya Tanganyika itaanza kuandaliwa lini?
 
Kuna wabunge flani wamewateua ndugu zao kuwa wabunge wa viti maalumu...mmoja amempa shemeji na dada yake, mwengine amempa mtoto wake na mkwe wake na mwengine kawapa nyumba kubwa na ndogo zake mbili zipo mjengoni....nadhani sasa tutaheshimiana
 
aisee kama unayo soft kopy ya hiyo rasimu tutupie na sie tuipate,
 
Tusitegemee la maana. Sanasana ni kukamilisha ratiba tu, maana ni kama bora liende!
Kama Tundu Lissu anaundiwa mzengwe wa kumwagwa Bungeni kwaajili ya katiba hii, unategemea kuna jema lolote kwa Mtanzania humo?
Its sadenning, maana nchi zingine kama zinatokea kuwa makini kupita kiasi, basi ni wakati wa kuandaa katiba. Lakini hawa wenzetu issue ni kuangalia maslahi ya makundi katika katiba!
The move is Kill Them Before They Grow!
Tunaongozwa na hisia na ushabiki wa kitoto
 
Wanapopendekeza Serikali tatu, hii Katiba itakuwa kwa ajili ya Serikali shirikisho au serikali zote tatu? Na kama ni ya Serikali ya shirikisho Zanzibar tayari wana katiba yao ya Tanganyika itaanza kuandaliwa lini?
Umepaka jina lako rangi nyekundu lakini hoja zako ni dhaifu..pole sana!!! Mchakato unaendelea, for your information.
 
Uhuru wa Bunge, uhuru wa mahakama na uhuru wa Tume ya Taifa ya uchaguzi bado vina utata mkubwa katika rasimu hii hasa kwa kuwa bado involvement ya Executive ni kubwa katika vyombo hivi kupitia mamlaka ya rais. Kama tuna nia njema haya yarekebishwe.

Pia sioni maantiki ya kuwa na wabunge wawili kwa kila jimbo la uchaguzi. Hii ni gharama kubwa kwa watanzani kinyume na nia ya kupunguza gharama za uendeshaji kama ilivyo katika mapendekezo ya kupunguza baraza la mawaziri.
 
Kinga ya rais na issue ya wakuu wa wilaya na mikoa viangaliwe upya. yaliyomo kwenye rasimu si matarajio ya watanzania

Wewe ni msemaji wa watanzania??? Mimi binafsi nimeridhika na rasimu hii, imejibu maswali ya muda mrefu yaliyokwa yananitesa mfano tume huru ya uchagusi, kupinga matokeo ya urais, serikali tatu, mahakama ya juu ie supreme court na mengine mengi tu.
 
Uhuru wa Bunge, uhuru wa mahakama na uhuru wa Tume ya Taifa ya uchaguzi bado vina utata mkubwa katika rasimu hii hasa kwa kuwa bado involvement ya Executive ni kubwa katika vyombo hivi kupitia mamlaka ya rais. Kama tuna nia njema haya yarekebishwe.

Pia sioni maantiki ya kuwa na wabunge wawili kwa kila jimbo la uchaguzi. Hii ni gharama kubwa kwa watanzani kinyume na nia ya kupunguza gharama za uendeshaji kama ilivyo katika mapendekezo ya kupunguza baraza la mawaziri.

Mkuu kuhusu idadi ya wabunge wala sio tatizo, wabunge waliopo sasa ni 351 lakini rasimu hii imependekeza wabaki 75 wa kiume na kike. Huoni ni idadi pungufu tano??? Think big
 
Back
Top Bottom