Rasmi Ben Affleck amchumbia tena Jennifer Lopez

Rasmi Ben Affleck amchumbia tena Jennifer Lopez

Ili iweeje,!!!? Yani wanataka enda gundua kipya kipi!? Hovyo kabisa!! All f*cked up
 
View attachment 2182761

Baada ya kuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi kwa muda, hatimaye staa wa muziki Jennifer Lopez na muigizaji wa filamu za Hollywood, Ben Affleck wametangaza kuwa wachumba baada ya kuvalishana pete.

Wawili hao walirudiana mwaka 2021 baada ya uchumba wao wa awali kuvunjika mwaka 2004.

Lynda Lopezambaye ni dada wa Jennifer alipost picha ya wawili hao na kuwapa pongezi kwa maamuzi waliyochukua huku Jennifer akionekana kuwa na pete kidoleni.

Ikiwa watafunga ndoa itakuwa ni mara ya nne kwa Lopez, 52, na ya pili kwa Affleck, 49.

Jennifer aliwahi kufunga ndoa na Ojani Noa, Cris Judd na Marc Anthony ambaye alizaa naye watoto wawili pacha ambao ni Max na Emme wenye umri wa miaka 14.

Affleck alifunga ndoa na muigizaji Jennifer Garner na wawili hao wana watoto ambao ni Violet, 16, Seraphina, 13, na Samuel, 10.

Source: People
Kwa hiyo tufanyeje na wanatuhusu nini hawa?
 
Ben afleck hajawahi cheat ktk urafik wake yeye na mwanae Matt Damon tu, zaid ya hapo kila uhusiano lazima acheat..bahat yake ana pesa huyo jamaa ni wa hovyo

Matt Damon sio mtoto wa Ben Aflek; hawa ni marafiki!!!
 
Back
Top Bottom