Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kwa hiyo tufanyeje na wanatuhusu nini hawa?View attachment 2182761
Baada ya kuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi kwa muda, hatimaye staa wa muziki Jennifer Lopez na muigizaji wa filamu za Hollywood, Ben Affleck wametangaza kuwa wachumba baada ya kuvalishana pete.
Wawili hao walirudiana mwaka 2021 baada ya uchumba wao wa awali kuvunjika mwaka 2004.
Lynda Lopezambaye ni dada wa Jennifer alipost picha ya wawili hao na kuwapa pongezi kwa maamuzi waliyochukua huku Jennifer akionekana kuwa na pete kidoleni.
Ikiwa watafunga ndoa itakuwa ni mara ya nne kwa Lopez, 52, na ya pili kwa Affleck, 49.
Jennifer aliwahi kufunga ndoa na Ojani Noa, Cris Judd na Marc Anthony ambaye alizaa naye watoto wawili pacha ambao ni Max na Emme wenye umri wa miaka 14.
Affleck alifunga ndoa na muigizaji Jennifer Garner na wawili hao wana watoto ambao ni Violet, 16, Seraphina, 13, na Samuel, 10.
Source: People
Akitoka p.didy itabidi McAnthony nae arudishe majeshi hapoKoloni lake la zamani ilo
Wakiachana, p.didy nae arudishe majeshi kiporo chake Cha zaman icho[emoji4]
Mh!!!Utasikia oooh ukirudiana na ex wako ni ujinga mnayajua mapenz nyie
Unamanisha huyu wa kumbi la moto?Jenifer na Dida ni wamoja...
Yani siwezi kurudia kitabu nilicho kisoma wakati mwisho wake nna ujua.
[emoji23][emoji23]Aliyeelewa hapa anifafanulie
Ebu funguka kidogo...kuna jambo unalo kubwa la kutuelezaUtasikia oooh ukirudiana na ex wako ni ujinga mnayajua mapenz nyie
Jlo hana tofaut na dada zetu wa kimbulu
Nahis atakuwa ni wa kateshi au dareda paleJlo ni mbulu aliechangamka [emoji23]
Ben afleck hajawahi cheat ktk urafik wake yeye na mwanae Matt Damon tu, zaid ya hapo kila uhusiano lazima acheat..bahat yake ana pesa huyo jamaa ni wa hovyo
Matt Damon sio mtoto wa Ben Aflek; hawa ni marafiki!!!
Nimecheka sana mi mwenyewe sijaelewa [emoji23][emoji23]Aliyeelewa hapa anifafanulie