Rasmi Dar yakumbwa na uhaba wa Maji, RC Makalla athibitisha uwepo wa Mgao

Rasmi Dar yakumbwa na uhaba wa Maji, RC Makalla athibitisha uwepo wa Mgao

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Akizungumza baada ya kutembelea vyanzo vya Ruvu Chini na Juu, Mkuu wa Mkoa Amos Makalla amesema mgao wa Maji umesababishwa na kupungua kwa uzalishaji kunakotokana na ukame.

Makalla amesema hali ya Maji sio nzuri kwenye kina cha maji cha vyanzo hivyo huku uzalishaji ukipungua kutoka lita za ujazo milioni 466 kwa siku hadi kufika lita milioni 300 sawa na 64% ya uzalishaji wote wa maji.

Amesema "Naomba niwaambie wananchi kuwa mgao haupekuki kutokana na ukame ambao unatokana na kunyesha kwa mvua chache msimu uliopita na kuchelewa kunyesha kwa mvua katika msimu huu wa vuli."

======================

Wakati Serikali ikitangaza kuanza kwa mgawo wa maji jijini Dar es Salaam, sababu ya kutokea shida ya maji kila unapofika mwisho wa mwaka imeelezwa.

Akizungumza leo Jumanne Oktoba 25 baada ya kutembelea vyanzo vya vya kuzalisha maji vya Ruvu Chini na Ruvu Juu, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla amesema sababu ni kupunguza kwa uzalishaji wa maji unaotokana na ukame.

Makalla aliyewawakilisha pia wakuu wa mikoa ya Pwani na Morogoro amesema hali sio nzuri kwani kina cha maji cha vyanzo hivyo vyote kimepungua huku uzalishaji ukipungua kutoka lita za ujazo milioni 466 kwa siku hadi kufika lita milioni 300 sawa na asilimia 64 ya uzalishaji wote wa maji.

"Naomba niwaambie wananchi kuwa mgao haupekuki kutokana na ukame ambao tayari TMA ilishatangaza kuwepo kwa hali hii muda mrefu kulikosabbisha na kunyesha kwa mvua chache msimu wa mvua uliopita na kuchelewa kunyesha kwa mvua katika msimu huu wa vuli.

"Pia watu waelewe hali hii haisababishwi na Serikali wala sera za CCM bali ni mipango ya Mungu, hivyo asitokee mtu huko akaanza kupotosha huko, kikubwa tuendelee kumuomba Mungu atuletee mvua za vuli na vyanzo vyetu vya maji viweze kujaa,” alisema Makalla.

Aidha jitihada nyingine ambazo serikali imezifanya Makalla alisema kuanzi Mkoa wa Morogoro, Pwani na Dar es Salaam, kamati zote za ulinzi na usalama zimewadhibiti watu wote ambao walikuwa wakichepusha maji na sasa kisingizo cha kuwa ni wao wanaosababisha uhaba wa maji hakipo.

Pia kwa wakazi wa Dar es Salaam na Pwani amewaomba kutumia vizuri maji yanayopatikana ili yaweze kuwafaa kwa nyakati hii.

Kwa upande wake Ofisa Mtendaji wa Dawasa, Cyprian Luhemeia alisema watatoa ratiba za mgao huo siku sio nyingi.

Kwa mujibu wa Dawasa kupitia maofisa Mtendaji wake, Luhemeja, Maji yanayohitajika kwa jiji la Dar es Salaam kwa siku ni lita za ujazo milioni 500 hivyo kufanya kuwa na uhaba wa lita 200 kwa sasa.

Katika ziara hiyo, Makalla aliongozana na bodi ya Dawasa pamoja na Wakuu Wilaya ne Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Lubigija, Mkuu wa Wilaya Kigamboni, Fatma Almas, Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Heri James na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Godwin Gondwe.

Alipotafutwa Naibu Waziri wa Maji Maryprisca Mahundi kuzungumzia mikakati ya Serikali kukabiliana na adha hiyo ambayo inaonekana kuanza kuwa sugu katika miezi ya mwisho wa mwaka alijibu kwa kifupi,

“Kama ulimsikiliza vizuri aliyetangaza hiyo, majibu yako wazi hiyo ni natural calamities (majanga ya asili), hata hivyo nipo kikaoni,” alisema na kukata simu.

MWANANCHI
 
Hizi ni sera za CCM ndio maana hakuna maji ya kutosha, akili mbovu za CCM hawajawahi kuweka investment yeyote ya maana kwenye maji, wanatumia sytem iliyojengwa na mkoloni ambayo ilikuwa una hudumia watu laki moja na sasa jiji lina watu milioni zaidi ya nne, jiji limekuwa mara zaidi ya 40, wanajua mitambo ya Ruvu haina uwezo hata wa kuhudumia watu milioni 1, Rufiji kuna maji kuliko Ruvu na inaweza kuhudumia jiji lote bila matatizo lakini akili fupi za kimaskini za watawala wa CCM haziwezi kuona hilo, nchi tajiri ina kila kitu lakini tumeponzwa na vilaza wa CCM.
 
Kutegemea maji ya Ruvu kwa Dar ni hatari sana, Dar inahitahi chanzo cha maji cha uhakika , either watoe maji hata Mwanza, ikishindikana hata Kigoma lake Tanganyika au Ziwa nyasa, au wasafishe maki ya Bahari ya hindi

Ila yale pale Ruvu ni hatari ya kufa mtu na vipi mvua zisipo nyesha hadi mwakani hali itakuwaje kwa Dar huko?
Screenshot_20221025_192427_com.facebook.katana.jpg
 
Kutegemea maji ya Ruvu kwa Dar ni hatari sana, Dar inahitahi chanzo cha maji cha uhakika , either watoe maji hata Mwanza, ikishindikana hata Kigoma lake Tanganyika au Ziwa nyasa, au wasafishe maki ya Bahari ya hindi

Ila yale pale Ruvu ni hatari ya kufa mtu na vipi mvua zisipo nyesha hadi mwakani hali itakuwaje kwa Dar huko?View attachment 2397755
Alafu sisi ndo tunajifanya kuwavimbia mabeberu fu....k shit hole,yaani tz na watz wake ni kituko cha karne!!
 
Hizi ni sera za CCM ndio maana hakuna maji ya kutosha, akili mbovu za CCM hawajawahi kuweka investment yeyote ya maana kwenye maji, wanatumia sytem iliyojengwa na mkoloni ambayo ilikuwa una hudumia watu laki moja na sasa jiji lina watu milioni zaidi ya nne, jiji limekuwa mara zaidi ya 40, wanajua mitambo ya Ruvu haina uwezo hata wa kuhudumia watu milioni 1, Rufiji kuna maji kuliko Ruvu na inaweza kuhudumia jiji lote bila matatizo lakini akili fupi za kimaskini za watawala wa CCM haziwezi kuona hilo, nchi tajiri ina kila kitu lakini tumeponzwa na vilaza wa CCM

Ni jambo la aibu sana hata baada ya miaka 60 ya uhuru bado tuna hangaika na migao ya maji na umeme
 
RC Makalla amesema wakazi wa Jiji la DSM watumie Maji kwa uangalifu mkubwa kwani uzalishaji umepungua huko Ruvu ambako wanazalisha 64% tu

Makalla amesema uhaba huo imesababishwa na mvua kuwa chache hivyo Dawasa wasilaumiwe kwa chochote

Source ITV habari
 
RC Makalla amesema wakazi wa Jiji la DSM watumie Maji kwa uangalifu mkubwa kwani uzalishaji umepungua huko Ruvu ambako wanazalisha 64% tu

Makalla amesema uhaba huo imesababishwa na mvua kuwa chache hivyo Dawasa wasilaumiwe kwa chochote

Source ITV habari
Kwa hiyo kaishia hapo.
Hawajali kwa sababu wanajua Rais hawezi kufanya kitu.
Maisha yangu yote sitakuja kumsahau JPM .....kwa hakika Makala angeshatumbuliwa asubuhi tu..hayuko serious...
 
Hivi hamna mechanism yoyote kisayansi kutumia maji ya bahari na kuyageuza kuwa maji salama kwa matumizi ya mwanadamu,?

Miaka nenda rudi wanasayansi wamekwama wapi?
Maji ya kawaida tu tumeshindwa kuyakusanya na kuyatumia, ndiyo tutaweza kutumia maji ya Bahari. Hiyo njia ya kutakasa na kuyatoa chumvi maji ya Bahari ipo, ila ni gharama sana na inatumika zaidi huko Uarabuni.
 
Kwa hiyo kaishia hapo. ....
Hawajali kwa sababu wanajua Rais hawezi kufanya kitu..
Maisha yangu yote sitakuja kumsahau JPM .....kwa hakika Makala angeshatumbuliwa asubuhi tu..hayuko serious...
Enzi ya JPM kulikuwa hakuna shida ya maji Dar es salaam? Au ngekuwepo yeye angefanya maji yaongezeke mto Ruvu ili uzalishaji upande toka 64% hadi 100%?
 
Kuanzia Aweso hadi Luhemeja wapo kimya kabisa...alafu unasema nchi ina viongozi hatari sana.
 
RC Makalla amesema wakazi wa Jiji la DSM watumie Maji kwa uangalifu mkubwa kwani uzalishaji umepungua huko Ruvu ambako wanazalisha 64% tu

Makalla amesema uhaba huo imesababishwa na mvua kuwa chache hivyo Dawasa wasilaumiwe kwa chochote

Source ITV habari
Ukiwa na mikono iliyopooza kila unachoshika kunapooza.
Ukame tulikuwa tumesha usahau. Mgao wa maji na umeme vilitoweka.
Sasa ameingia mwenye mikono yake iliuojaa mapooza
 
Hivi hamna mechanism yoyote kisayansi kutumia maji ya bahari na kuyageuza kuwa maji salama kwa matumizi ya mwanadamu,?

Miaka nenda rudi wanasayansi wamekwama wapi?
... kwa jiji kuu la kibiashara kama Dar es Salaam Serikali ilitakiwa iwe na reservoir ya uhakika ya maji bila kutegemea mvua. Wanashindwa nini kuchimba ziwa/bwawa kubwa likajazwa na Ruvu hiyo hiyo kipindi cha neema na kutumika wakati wa shida even for 3 consecutive years of 0 rainfall? Hatujielewi; kazi kutafuta visingizio sijui hakuna mvua sijui nini!
 
Back
Top Bottom