Rasmi Diamond aiwasilisha Komasava kwenye tuzo za Grammy. Tutatoboa?

Rasmi Diamond aiwasilisha Komasava kwenye tuzo za Grammy. Tutatoboa?

WCB wametangaza kuwa Diamond amewasilisha wimbo wa Komasava kuwania Tuzo za Grammy mwaka kesho.

Komasava imewasilishwa katika vipengele vya Best Music Video na Best African Music Performance.

Mnadhani atashinda mbele ya Burna Boy, Wizkid na magwiji wengine?

View attachment 3121644

Akae mbali tu na ccm then mambo yake yanakuwa mazuri, Bora wa Tanzania kuwa kimya na kutokupiga kura, kuliko kuendesha kampeni ya kuwapinga
 
Hii nina uhakika asilimia 100 tunachukua.

Kiukweli hili ngoma limebamba duniani kote. Beat ni kali, mistari imenyooka, vibe lake ni la asili pia chupa limekaa vizuri.

All the best Platnumz.

Sidhani mkuu. Ngoma imeenda ndiyo lakini kwa muundo wa grammy ulivyo sidhani kama atashinda
 
Back
Top Bottom