Rasmi kwa ridhaa yangu mwenyewe nimeamua kuacha pombe Eeeh Mwenyezi Mungu nisaidie

Habari za muda huu ndugu zangu.
Katika hali ya kawaida ni vigumu kunielewa kama hayajakukuta.

Pombe imeniharibia vingi sana kwenye maisha yangu zaidi ya kunipa faida.

- Pombe imemaliza fedha nyingi mno kiasi ambacho speed ya maendeleo yangu ni madogo ukilinganisha na kipato changu.

- Pombe imenipotezea marafiki wa maaana na kubaki na walevi ambao waliowengi ni wapumbavu.

- Pombe imenitenganisha na Mungu ni marachache sana kwa walevi kwenda ibadani maana jana yake ambapo Jumamosi wamekesha kwenye pombe wakifurahia weekend.

-Pombe imenifanya nipate ajali nyingi kwa mwaka huu tu, jana ilikuwa ajali ya 11 ambapo ilitaka kuchukua uhai wangu kabisa lakini Mungu hakuniacha aendelea kunilinda na kunipa muda wa kujibadilisha[emoji120]

-Pombe imenukutanisha na wanawake wa ajabu kwa ajili tu ya kujiridhisha kimwili ambapo na amini wamebeba laana na mkosi mingi mno, lakini Pia Mungu hakuniacha aliendelea kunilinda Afya yangu bado iko poa.

-Pombe imenifanya kutokuwa mwaminifu kazini, nimekuwa mwizi nguli ili mradi tu nipate hela ya kulewa.

-Pombe imenifanya hadi sasa nina miaka 33+ sina mke wala mtoto na sifikirii najiona mjinga sana katika hili.

Nina mengi mno yakustaajabisha na kutia simanzi sababu ya pombe, Nakiona kifo kipo karibu yangu kama nisipo badilika.

Namshukuru Mungu sana kwa kuendelea kua nami hali ya kuwa nimekuwa nikimkose, Namuomba Mungu sana Leo tarehe 01/07/2022 iwe mwisho wa mahusiano na pombe Maisha yangu yote Eeeh mwenyezi Mungu nisaidie.
Mungu akusaidie sana na utaweza usisikilize watu wanaokukatisha tamaa kua utarudia, amini kwamba umeacha na hutarudi nyuma.
 
Ndio maana nikakuambia ni kawaida hicho unachofanya kwa sasa. Ila ukishatengeneza uchumi wako ukaimarika utarudi kule kule, sasa tukuombee ili hata ukiimarika kiuchumi usijerudi kwenye pombe.
Bado sijafika kwenye hy stage boss ila nimeamua kuachana pombe
 
Mkuu hongera kwa kujitambua natumaini hujachewa mkuu.

inshort, Pombe na soda si njema kwa afya ni chanzo cha magonjwa sugu kama kisukari,figo, High BP. Watu wamepoteza maisha/uelekeo kwa sababu ya BIA

Nashauri wadau kutumia RED WINE badala ya pombe

Hongera mkuu 🤍
Pay hata Red wine ni pombe pia
 
12 Years Sober now.

Sio maamuzi mepesi ulioamua kuchukua boss. Vita vya mwili nw roho utavipigwa sana, cha muhimu msimamo na ustahimilivu.

Starehe zina nguvu sana, zinavuta sana na hazinogi bila kilevi. Misimamo yako itapimwa sana hapo! Be strong usitetereke.

Kuna muda utapata sana kiu na hamu ya kuonja japo "sip" moja, wakati huo simu za marafiki na babes zikiwa zinaita sana, na pengine mfukoni uko vyema sana. USITHUBUTU. Ukijaribu basi habari yako itakuwa bora ya jana.

Kila la kheri Boss. Mungu ni mwema sana atasimama na wewe
Ahsante kwa ushauri mzuri boss
 
Habari za muda huu ndugu zangu.
Katika hali ya kawaida ni vigumu kunielewa kama hayajakukuta.

Pombe imeniharibia vingi sana kwenye maisha yangu zaidi ya kunipa faida.

- Pombe imemaliza fedha nyingi mno kiasi ambacho speed ya maendeleo yangu ni madogo ukilinganisha na kipato changu.

- Pombe imenipotezea marafiki wa maaana na kubaki na walevi ambao waliowengi ni wapumbavu.

- Pombe imenitenganisha na Mungu ni marachache sana kwa walevi kwenda ibadani maana jana yake ambapo Jumamosi wamekesha kwenye pombe wakifurahia weekend.

-Pombe imenifanya nipate ajali nyingi kwa mwaka huu tu, jana ilikuwa ajali ya 11 ambapo ilitaka kuchukua uhai wangu kabisa lakini Mungu hakuniacha aendelea kunilinda na kunipa muda wa kujibadilisha[emoji120]

-Pombe imenukutanisha na wanawake wa ajabu kwa ajili tu ya kujiridhisha kimwili ambapo na amini wamebeba laana na mkosi mingi mno, lakini Pia Mungu hakuniacha aliendelea kunilinda Afya yangu bado iko poa.

-Pombe imenifanya kutokuwa mwaminifu kazini, nimekuwa mwizi nguli ili mradi tu nipate hela ya kulewa.

-Pombe imenifanya hadi sasa nina miaka 33+ sina mke wala mtoto na sifikirii najiona mjinga sana katika hili.

Nina mengi mno yakustaajabisha na kutia simanzi sababu ya pombe, Nakiona kifo kipo karibu yangu kama nisipo badilika.

Namshukuru Mungu sana kwa kuendelea kua nami hali ya kuwa nimekuwa nikimkose, Namuomba Mungu sana Leo tarehe 01/07/2022 iwe mwisho wa mahusiano na pombe Maisha yangu yote Eeeh mwenyezi Mungu nisaidie.
Ni ngumu sana ila naamini utaweza Mkuu.
 
Mkuu hongera kwa kujitambua natumaini hujachewa mkuu.

inshort, Pombe na soda si njema kwa afya ni chanzo cha magonjwa sugu kama kisukari,figo, High BP. Watu wamepoteza maisha/uelekeo kwa sababu ya BIA

Nashauri wadau kutumia RED WINE badala ya pombe

Hongera mkuu 🤍
Red wine sio pombe?? Mkuu
 
16567027343952308580236645427475.jpg

Punguza umama wewe jamaa.
Acha kuzikandia pombe tafadhali.

Pombe hazihusiki na wewe kutokumiliki gari, kutokujenga Wala kufanya Maendeleo.

Hebu niletee hao wasiokunywa halafu waniambia wanamiliki magari na nyumba ngapi??

#YNWA
 
Hongera mkuu Mimi nikiwa mbali na familia bila kuonja 2/3 siwezi Ila nikiwa home huwa sikumbuki hata means stress zinanifanya nijichanganye hapa naandika sms nipo km 800 toka kwa familia sijaonja hata nusu leo usingizi nitautafuta kwa manati
 
Hongera mkuu ila jaribu kubadili na marafiki ili usirudi huko,kua mtu wa ibada sana ili kuiimarisha imani yako na kukuweka karibu na Mungu,

Usisikilize maneno ya wanaokwambia utairudia pombe,ulikuja Duniani peke yako na utaondoka peke yako,

Ishi maisha uliyoyachagua wewe muhusika.
 
Back
Top Bottom