Rasmi kwa ridhaa yangu mwenyewe nimeamua kuacha pombe Eeeh Mwenyezi Mungu nisaidie

Rasmi kwa ridhaa yangu mwenyewe nimeamua kuacha pombe Eeeh Mwenyezi Mungu nisaidie

Habari za muda huu ndugu zangu.

Katika hali ya kawaida ni vigumu kunielewa kama hayajakukuta.

Pombe imeniharibia vingi sana kwenye maisha yangu zaidi ya kunipa faida.

- Pombe imemaliza fedha nyingi mno kiasi ambacho speed ya maendeleo yangu ni madogo ukilinganisha na kipato changu.

- Pombe imenipotezea marafiki wa maaana na kubaki na walevi ambao waliowengi ni wapumbavu.

- Pombe imenitenganisha na Mungu ni marachache sana kwa walevi kwenda ibadani maana jana yake ambapo Jumamosi wamekesha kwenye pombe wakifurahia weekend.

- Pombe imenifanya nipate ajali nyingi kwa mwaka huu tu, jana ilikuwa ajali ya 11 ambapo ilitaka kuchukua uhai wangu kabisa lakini Mungu hakuniacha aendelea kunilinda na kunipa muda wa kujibadilisha[emoji120]

- Pombe imenukutanisha na wanawake wa ajabu kwa ajili tu ya kujiridhisha kimwili ambapo na amini wamebeba laana na mkosi mingi mno, lakini Pia Mungu hakuniacha aliendelea kunilinda Afya yangu bado iko poa.

- Pombe imenifanya kutokuwa mwaminifu kazini, nimekuwa mwizi nguli ili mradi tu nipate hela ya kulewa.

-Pombe imenifanya hadi sasa nina miaka 33+ sina mke wala mtoto na sifikirii najiona mjinga sana katika hili.

Nina mengi mno yakustaajabisha na kutia simanzi sababu ya pombe, Nakiona kifo kipo karibu yangu kama nisipo badilika.

Namshukuru Mungu sana kwa kuendelea kua nami hali ya kuwa nimekuwa nikimkose, Namuomba Mungu sana Leo tarehe 01/07/2022 iwe mwisho wa mahusiano na pombe Maisha yangu yote Eeeh mwenyezi Mungu nisaidie.
Ngoja wenge likuishe na udake tena mkwanja wa maana kama hatutokukuta kiti kirefu kaunta
 
Lidhaa = Ridhaa
Pombe huwezi kuiacha kirahisi hivyo Kijana
Mdau anafikiri kuacha pombe ni sawa na kuacha chuo. Mziki wa pombe siyo wa kitoto kwani ingekuwa rahisi kila mnywaji angekuwa kaacha
 
Mimi bia zilikuwa zinanimalizia sana hela. Sasa hivi toka tarehe 13 juni sijagusa, nakunywa konyagi ya 8000 na soda ya 600 na simalizi.
Nikifika kwa mangi naagiza nyagi napiga, ikishapanda kichwani inayobaki naondoka nayo naitumia kama breakfast asubuhi.
Acha kunitia moyo kwa ninachokifanya.
 
kuna mwenzio kapigwa pumb kakimbia mjini.
Acheni kulewa kuna vijana washenzi sana.ukilewa TU wanakufanya
 
Issue siyo pombe, ni wewe. We use it, siyo ku-abuse. Wewe ndiyo tatizo usisingizie pombe
 
Kiongozi hizo beer ulikua unakunywa wapi mpaka unakutana na wanawake wa ajabu??
 
If it's coming from your intimacy, congratulations nakushauri uokoke then roho mtakatifu atakusaidia kuzishinda dhambi zote siyo ulevi tu!
 
Mdau anafikiri kuacha pombe ni sawa na kuacha chuo. Mziki wa pombe siyo wa kitoto kwani ingekuwa rahisi kila mnywaji angekuwa kaacha
Acha kutiisha watu simple way ya kuacha gambe Ni kumkili KRISTO YESU no kuwa Bwana na mwokozi wa maisha yako! Fanya hivyo kiu ya pombe inakatika from no where,kwa msaada wa roho mtakatifu!
 
Kiongozi hizo beer ulikua unakunywa wapi mpaka unakutana na wanawake wa ajabu??
Mwanamke yeyote anaejirahisi kwa namna yoyote ile ni waajabu....hakuna mwanamke naejiheshimu ukampata kurahisi hivyo kama tunaowapataga kwenye Mitungi
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Huwa uchumi ukiyumba tunapunguza vitu visivyo vya lazima, it's normal mkuu. Ninachojua tu, uchumi wako ukiongezeka tu utairudia pombe kwa speed kubwa mno.
 
Back
Top Bottom