Rasmi kwa ridhaa yangu mwenyewe nimeamua kuacha pombe Eeeh Mwenyezi Mungu nisaidie

Mungu akusaidie sana na utaweza usisikilize watu wanaokukatisha tamaa kua utarudia, amini kwamba umeacha na hutarudi nyuma.
 
Ndio maana nikakuambia ni kawaida hicho unachofanya kwa sasa. Ila ukishatengeneza uchumi wako ukaimarika utarudi kule kule, sasa tukuombee ili hata ukiimarika kiuchumi usijerudi kwenye pombe.
Bado sijafika kwenye hy stage boss ila nimeamua kuachana pombe
 
Pay hata Red wine ni pombe pia
 
Ahsante kwa ushauri mzuri boss
 
Ni ngumu sana ila naamini utaweza Mkuu.
 
Red wine sio pombe?? Mkuu
 


Punguza umama wewe jamaa.
Acha kuzikandia pombe tafadhali.

Pombe hazihusiki na wewe kutokumiliki gari, kutokujenga Wala kufanya Maendeleo.

Hebu niletee hao wasiokunywa halafu waniambia wanamiliki magari na nyumba ngapi??

#YNWA
 
Hongera mkuu Mimi nikiwa mbali na familia bila kuonja 2/3 siwezi Ila nikiwa home huwa sikumbuki hata means stress zinanifanya nijichanganye hapa naandika sms nipo km 800 toka kwa familia sijaonja hata nusu leo usingizi nitautafuta kwa manati
 
Hongera mkuu ila jaribu kubadili na marafiki ili usirudi huko,kua mtu wa ibada sana ili kuiimarisha imani yako na kukuweka karibu na Mungu,

Usisikilize maneno ya wanaokwambia utairudia pombe,ulikuja Duniani peke yako na utaondoka peke yako,

Ishi maisha uliyoyachagua wewe muhusika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…